In link Wana CCM wataacha unafiki

leonaldo

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
2,584
Reaction score
3,185
Ugonjwa wa Wana CCM kuwa wanafiki na kushindwa kukisaidia chama kustawi nauliza utaisha lini?
Mfano wa unafki uliopitiliza ni huu wa Mr polepole kutaka kumwadhibu Nape kwa kuwaambia ukweli, sasa ni wakati mwafaka kuwakumbusha hawa jamaa matamko yao ya nyuma ili asiyekuwa na dhambi CCM ndie aanze kutupa jiwe kwa Nape.
 
Nape Nnauye nae apunguze Kiherehere na Sifa halafu atambue kuwa kuna Watu wameihangaikia na kuitumikia CCM kwa nguvu zao zote hadi alipoikuta Yeye na wamenyamaza tu ila nchi inawatambua na kuwaheshimu. Hivi Nape wenu ana nguvu au uchungu na CCM kama alionao Mzee Philip Mangula?

Msihi Nape wako kuwa akazane sasa kulihangaikia tu Jimbo lake ambalo hata hivyo nina uhakika wa 100% kuwa 2020 hapiti na ataanguka tena Kifo kibaya mno na hatoamini. Madhambi au Faulo iliyofanywa 2015 hadi akaibuka Mshindi inajulikana na hata Yeye anaijua hivyo mwambieni afunge bakuli lake kwani tumeshachoka sasa ngojera zake zisizo na mwisho.

Nadhani badala ya kusema CCM ni Wanafiki ni dhahiri kuwa kwa haya maelezo yako Wewe ndiyo Mnafiki uliyetukuka Mkuu.
 


Kama unampenda sana Nape kamtambulishe nyumbani kwenu!
 
Unafiki na CCM ni kama, SIMBA na POINT ZA MEZANI, yaani ni damu damu.
 
Hivi huyu bwana taratibu ni kijana au mzee? Nashindwaga nimueweke kundi lipi?
 
Unafiki wangu ni nini hapo mkuu, Mimi hoja yangu ni kuwa hata polepole hana hiyo sifa ya kutokuwa mnafiki kwani tuna kumbuka sana alichokuwa akikinena kuhusu CCM,Hivyo hawezi kuwa wa kwanza kutupa jiwe
 
Hivi huyu bwana taratibu ni kijana au mzee? Nashindwaga nimueweke kundi lipi?
Kutokana na utafiti wa hivi karibuni, ilishindikana kujulikana kama huyu bwana ni Mzee au kijana.
 
Unafiki wangu ni nini hapo mkuu, Mimi hoja yangu ni kuwa hata polepole hana hiyo sifa ya kutokuwa mnafiki kwani tuna kumbuka sana alichokuwa akikinena kuhusu CCM,Hivyo hawezi kuwa wa kwanza kutupa jiwe

Nape alikuwepo na ataondoka akitaka ila CCM itabaki Milele. Kuna mwana CCM aliyekuwa tishio na ana mvuto wote kama Augustino Mrema miaka ile ya 90? Je alipoondoka na kuhamia NCCR - Mageuzi CCM ilitetereka au kukumbwa na msukosuko wowote wa kukitishia Chama? Jifunzeni kufanya thorough analysis mnapokuja humu JF ili mkamilishe usemi mzuri wa jamvi kuwa ni home of Great Thinkers.
 
Njaa ni mbaya sana ...... ukiunganisha na elimu za kuunga unga ni shida. Hii nchi haitaweza kundelea mbele chini ya CCM kwa sababu hawataki ukweli katika mambo ya msingi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…