Wana-CCM, mtateswa na kuwa watumwa wa hii ripoti hadi lini?

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
396
1,377
Wanabodi, tahadhima kwenu.

Nianze kwa kuwauliza, hivi ni kwa nini viongozi waandamizi wa CCM wastaafu na walioko madarakani hawathubutu kumkosoa Rais Magufuli Mwenyekiti wao? Hivi ni kweli Magufuli yuko kwenye right track kiuongozi kiasi kwamba hatakiwi kukosolewa kwa lolote?

Mara ya mwisho kigogo wa CCM kumkosoa Rais Magufuli ni Mzee Ben Mkapa aliyemwambia hadharani, "usiseme kila kila kitu Serikali yangu, Serikali ni ya CCM". Lakini pia Jakaya alipojaribu kumkosoa Magu aliambiwa "kuna wazee wanawashwa-washwa", Jakaya akakaa kimya hadi leo.

Swali, Mwenyekiti Magufuli ni mkubwa kuliko CCM? Je, anaogopwa kwa kiwango gani? Kwa nini wazee wa chama wako kimya hata pale Magu akikosea? Wanamuogopa?

Mwaka mmoja au miwili iliyopita waliobaki kumkosoa Magufuli hadharani ni vijana wa upinzani pekee pengine na yule kada wao Bollen Ngetti ambaye naye baada ya kutekwa mara kadhaa akapotea. Sasa ameibuka lakini kwa staili ya kusifia uongozi wa Rais Magufuli. Bado, tunahoji, Rais Magufuli anaogopwa na makada wa CCM?

Ukweli ni huu hapo nilioupata katika korido za Lumumba. Ni kwamba mtakumbuka baada ya kukabidhiwa rungu la Uenyekiti wa chama Magufuli aliunda tume ya kuchunguza mali za CCM nchi nzima ikiongozwa na Dk. Bashiru Ally.

Ripoti ya tume hiyo iliyompa Bashiru cheo cha Katibu Mkuu imewaanika wana-CCM na hasa makada wa kitaifa. Nimefanikiwa kusoma kitabu cha ripoti hiyo ikiwa na kurasa 300. Ripoti hii ilioneshwa jalada mara moja tu alipokabidhiwa M/kiti Magufuli na baada ya hapo ilibaki kuwa siri kubwa na nzito huku ni Magufuli, Bashiru na Polepole pekee wakiwa na nakala.

Habari kutoka korido za Lumumba zinasema kwamba, ripoti hiyo imejaa madudu na ufisadi wa kutisha uliofanywa na wana-CCM kiasi cha kukufanya chama hicho kuwa Mhimili wa Shetani (devil axis).

Mwenyekiti wake Rais Magufuli anatumia ripoti hiyo kama nyundo na rungu vichwani mwa wanaotaka kumkosoa. Kwamba ukijaribu kumkosoa unaitwa na kuoneshwa ukurasa wako na kisha kuulizwa, "vipi mzee twende Kisutu kwa uhujumu uchumi au ukae kimya?". Jibu ni kukaa kimya.

Rungu hili lilimkuta Nape, January Makamba, Kinana, Kikwete, Salma Kikwete, Yusuf Makamba, Ridhiwan, Amos Makalla, Diallo, Sofia Simba, Lowassa, Sumaye, Rostam na wengine wengi. Hii ni silaha hatari anayotumia Magu kuwaangamiza wenzie.

"Sio Siri, ripoti hii itatumaliza hasa tulio na njozi ya kugombea Urais. Tuna taarifa kuwa ikibaki mwaka mmoja kabla ya 2025 kama utaonekana tishio na si chaguo la namba moja (JPM) basi utafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na kupelekwa Keko na huo ndio mwisho wako kisiasa, inaumiza!" anasema kijana mwenye ndoto ya kugombea Urais 2025 kupitia chama hicho.

Mimi ninashauri, Wana CCM jitoeni ufahamu. Fyatukeni kudai ripoti hiyo kuwekwa hadharani kila mtu asome ili kuwapa muda wa kujisafisha mapema. Msiwe watumwa wa ripoti hii. Na kinachofurahisha ni kwamba hata namba moja naye anayo ukurasa wake unaohusu ufisadi. Sasa mnaogopa nini? Kuweni jasiri, chama ni chenu si ya mtu. Msikwamishe ndoto za vijana wanaotaka uongozi. Acheni woga na unafiki. Chama ni kikubwa na maarufu kuliko Magufuli na yeyote.

#MitanoTena
 
Kuna wakati wazungu wakituita sisi si binadamu halisi kuna watu Wanatoa maneno kama wamekatwa kichwa?

Ukweli ni kwamba hakuna mzungu anayemtea mzungu wenzake na hapo hapo ukute wazungu wana wanafurahi kwa kitendo hicho.

Ngoja waje vijana kutoka lumumba wakiwa wamechiba ubwabwa wakutukane mpka kesho.
 
Wewe mkuu pambana tu. Usitafute msaada. Kama ulifanya ufisadi,uvumilie tu spana zake zikianza kupigwa.
 
Back
Top Bottom