comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,014
- 6,834
Akizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC Idhaa ya Kiswahili ambapo mwandishi alimuuliza kama kabla ya kumuita kwenye kikao aliwashirikisha watu waliomteua.
“Suala hilo lipo katika mamlaka ya spika,kumuita mtu ni kumpa haki ya yakusilizwa hivyo watu wanapaswa waelewe vizuri kwa sababu wahusika wanaweza wakachukua hatua za kinidhamu lakini bado wananchi wakawauliza kama tulimisikiliza na ili mtu umsikilize lazima aitwe,kwa hiyo kuitwa ni jambo la kawaida na ni kwa mamlaka ya spika.
“Atafika hapa atakwenda kukutana na wabunge wenziye ambao watamuuliza maswali yatakayokuwapo na yeye atapata haki ya kujielezea ndani ya bunge si nje,kama haki ni ya kwako ivi kwa nini wenzako wakuonee, ”alisema Ndugai.
Alisema hawajakurupuka kumuita mbunge huyo kwakuwa ameitwa kwa mambo ya hapa nyumbani ambayo yanahusisha utovu wa nidhamu na si hayo yanayoendelea katika bunge la Afrika.
“Yeye anaunganisha hilo na matendo ambayo anayafanya ambayo pia yanatudhalilisha kama nchi,lakini hatujamuita kwa mambo ya Afrika Kusini sisi tumemuita kwa mambo ya hapa nyumbani ya utovu mkubwa wa nidhamu,watanzania watulie baada ya muda suala hilo litaletwa bungeni wataelezwa anatuhumiwa nini na majibu yake yalikuwa ni nini kwa sababu lazima liletwe bungeni hilo suala,”alisema Ndugai.
mtanzania.co.tz

Spika Ndugai, Masele hapatoshi - Mtanzania
NA AZIZA MASOUD,DAR ES SALAAM SPIKA wa Bunge Job Ndugai amesema suala la kumuita Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Afrika(PAP) Steven Masele katika Kamati ya Maadili lipo katika mamlaka ya kiti chake hivyo hakuwa na sababu ya kujadiliana na wabunge wengine. Kauli ya Spika Ndugai imekuja wakati...
mtanzania.co.tz