Imezidi haijazidi biashara mtindo mmoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imezidi haijazidi biashara mtindo mmoja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Alnadaby, Sep 2, 2008.

 1. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mizani zetu zinazopima uzito ma magari ni mradi bora zaidi kwa wenye kutamani utajiri wa haraka haraka.Mafisadi vidagaa watarajiwa jiungeni katika wizara husika ili mkusanye hela ya bure.

  Jana tanki la mafuta lenye uwezo wa kubeba lita 10,000 lilikuwa likisafirisha mafuta na lilipofika Nyanguge likakuta mzani wa mkeka.Tanki limefanyiwa calibration na watu wa vipimo lina capacity ya 10,000 litres basi hakuna zaidi.

  Sasa kasheshe ya Nyanguge hiyo jana ati gari ikwa imezidi uzito.Dereva maskini hana hela.Anajua kuwa watozaji wa mzani wanataka wapewe chakula lakini hana.
  Na maskini hakujua taratibu za pale mahali.Kumbe hapo ni sehemu ya biashara na iwe gari imezidi au hakuizidi biashara ni kuwaona wapimaji kwanza.

  Poor guy alipoteza muda mwingi akampigia simu tajiri naye akamtosa,na mwisho mwa yote kaambiwa alipe faini shs.800,000/-

  Faini hana,mfukoni alipewa allowance shs 20,000 ili aweze kula safarini na kulaza ubavu wake.Anajua kuwa uzito haukuzidi lakini hana jeuri ya kupambana nao na wao ni ma expert wa kucheza na mzani.

  Mwisho wa yote sijui alifika au hakufika.Mimi nilijipitia hapo kimya lakini moyoni nikawa najiuliza....hivi haya mamizani yao yakiwa sawa au si sawa nani anajua huko Nyanguge?

  Hawa jamaa wa Tanroads nao si ni katika ile familia ya mafisadi?Gari ile ile imepita mizani zote lakini ikifika hapo..inaongezeka uzito..Jamani!!! he..!!

  Maisha bora kwa kila fisadi troup...na wasiokuwa wanachama tutaishi vipi?
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hivi karibuni nilipanda basi la kwenda mikoani, ambapo hawa wana uzoefu sana na wapimaji wote wa hizo mizani, Hadi kufika mwisho wa safari basi hilo lilipimwa mara tatu. Kwa kuwa Konda na Dereva wa basi hiyo wanatambua usumbufu mkubwa wa hao wapimaji walituomba abiria wote waliokaa nyuma ya baada ya matairi ya nyuma kuhamia mbele. Kadhia hii ilirudiwa mara tatu. Basi lenyewe halikuwa lemejaa, kila abiria alikuwa amekaa kwenye kiti chake raha mustarehe.

  Nilipopata nafasi ya kuongea na Konda, nilimuuliza ni kwanini abiria walikuwa wakipangwa kila basi linapokaribia mizani? Jibu lake alisema kuwa mabasi mengi yenye bodi zilizotengenezwa Kenya ni mazito, hivyo ukichanganya na uzito wa abiria, mizani usomeka kama umezidisha uzito.
   
  Last edited: Sep 2, 2008
 3. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Safari ya Dereva iliokolewa na na tajiri aliyeyanunua,ambaye alitoa shs.100,000 kama chakula na tank hilooo likaendelea na safari.Lorry hilo la mafuta ni mmoja tu ya mfano lakini kero inaendelea hapo Nyanguge.

  Hii ndiyo hali halisi.
   
Loading...