Imeniuma sanaa!

 

Usitoe mimba acha na amini usiamini mtoto akizaliwa ajileta mwenyewe na hapo ndio utamfunza adabu
 
 
Yaani i was just about to.......si unajua zile za kunyatia?yaani am shocked hadi mwisho!...

let me see kama naweza lea hivyo hivyo wa watu!
nilidhani hata kama kuna ishu labda angeniambia as niko hapahapa karibu yani!dah!

Life is full of surprises u don have to be shocked

talk to her muelewane anachohitaji kwa sasa ni support
 
Queen Kan unacho takiwa kujua kuwa mwanaume akiamua kukukana au kuku kataa haangalii historia kabisa sijui mambo tumetoka mbali,sijui tuna miaka minne hakuna.

Na bahati mbaya linapo kuja swala la kutumia kinga ni wanawake wachache sana wana weza wakawa na maamuzi ya kutumia au kutotumia! Maamuzi ya kutumia au kuto tumia kinga yapo kwa mwanaume.


Na katika somo ambalo pengine wanawake wengi na wasichana wamekuwa wakifeli ni hili la uwezo wa kuamua linapo kuja swala la kinga.

Queen Kan usinge andika kuwa huko chuoni yani nilikuwa nifikiri ni mdogo wangu kabisa.

Maana nina Mdogo wangu amemaliza diploma fulani majuzi tuu na mpango ulikuwa mwaka huu afanye application kwajili ya kuanza chuo, sasa niliishiwa nguvu na kusononeka mpaka leo
baada ya kupewa taarifa kuwa ana mimba,yaani kwakweli nime kosa la kusema hadi sasa na aliye niambia ni rafiki yangu na kinacho shangaza amekuwa akiniambia kuhusu kushughulikia yeye kwenda chuo na sasa ni mwezi wa pili hajaniulizia tena wala kunipigia simu kama kawaida yake na hilo ndilo limenifanya niamini kweli kanasa.

Kwakweli ina sikitisha sana maana nafikiri sijui nae kakanwa kama wewe na shule?

Aiseeee kuna mambo yana changanya sana, na mimi nimenyamaza na wala sito muuliza kabisa, kwakeli nina hasira.

Na huyu katika wadogo zangu niliona ndio anaelewa sana somu juu ya sisi wanaume kuwa huwa hatutofautiani sana lakini daaa kaniacha kwenye wakati mgumu sana tena sana.......

Najiuliza kama na yeye ana fikiria kutoa kama wewe sijui na sina mpango wa kumuuliza.

Hila Queen Kan usitoe mimba, we waeleze wazazi lakini ujue ina kwaza na kufedhehesha sana tena sana.

Ni wanaume wachache wanaoa mwanamke walio mpa mimba nje ya ndoa.

Jipange.
 
Last edited by a moderator:

thats what these kids shuld be told...well said
 
Last edited by a moderator:
Kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe.
 
Pole dear,hongera pia.Lea mimba yako ,Mungu anazo njia zaidi ya elfu hatakupungukia.
 
Hivi huko mwaka wangapi hapo chuoni?
 
Huyo hakutaki kukataa ujauzito kwa kisingizio hicho ni utoto. Lea ujauzito na umlee mwanao he/she atakuwa fahari yako.
 
Mshukuru upo chuo utalea mwanao;pata picha wale wasichana wa viijijini hawana mbele wala nyuma mbona wana lea.Simama imara,omba mungu yataisha hayo.
 
Amini wewe ni strong woman,naushukuru Mungu walao chuo umefika. Unaweza kulea vizuri mwanao bila msaada wa huyo mwanaume. Usikaribishe mawazo ya kushindwa my dia.
 

Usikate tamaa na wala usitoe ujauzito wewe jifungue kwanza kisha endelea na masomo yako, mbona wengi wamefanya hivyo na wamefanikiwa kimaisha.

Muhimu uwe umejifunza kosa lako na uachane na mambo ya uhusiano/mahusiano mpaka utakapomaliza masomo nina uhakika utakuja pata kazi ya maana(yenye masilahi) itakayokusaidia kumkuza mwanao na kuendesha maisha yako ya kila siku na pengine utakuja mpata mwenza ambae nae atakua na msimamo wa kimaisha
 
Jamani wanaume wengine wanafikiria kwa makalio kweli, hivi kama hutaki mtoto nje ya ndoa si angevumilia mpaka kufunga ndao!!? Usitoe mimba we lea mwanao mungu atakusaidia, pole sana
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…