Imenichukua miaka 10 kujenga chumba na sebule , na kunua gari aina ya terrios kid - kweli ajira nyingi hazilipi zama hizi

Kazi ya mwajiri ni kukulipa mshahara ila ni wajibu wako kuwa tajiri pale inapobidi.
Kama utaweza kupanga bajeti yako wisely na kuishi within your means Basi Hakuna pesa ndogo hata Kama unalipwa 20k kwa mwezi.

Ninachokiona hapo ulishindwa ku transform passive income ili kutengeneza mirija ya mingine ya pesa Hilo ni kosa kubwa.

Mshahara wa 1.3 mil ni mkubwa sana Kama ungeweza kutengeneza vyanzo vingine vya mapato.Ila Yote kwa Yote bado nafasi bado unayo unaweza kufanya masahihisho kabla ya kufikia miaka 30
 
Hongera mkuu wenzako wana miaka zaidi ya hiyo kazini still wanakaa kwenye Nyumba ya taasisi kwangu Mimi ni mafanikio.
 
habari wadau..

leo ilikuwa tarehe niliyomaliza chuo kikuu mwaka 2009...

nilibahatika kupata ajira ya kwanza mapema sana mwezi mmoja baada ya kuhitimu chuo mwaka 2009..

toka mwaka huo mpaka leo nimebadili waajiri zaidi ya mara 5 kutafuta greaner pasture...

na katika harakati zote hizo mshahara wa juu kuwahi kulipwa ni milioni moja na elfu 30 net...

najaribu kupima mafanikio ya kufanya kazi miaka 10..

siyaoni makubwa zaidi ya chumba na sebule nilichojenga tabata segerea napoishi..na gari ndogo nayoitumia.. na hapo mimi ni mbahili vibaya mno hata buku naithamini

vijana ambao hamjapata ajira... msisikitike sana kukosa ajira jitumeni kwenye ujasiriamali.. ajira nyingi hazilipi.. ni ajira chache sana ambazo zinalipa na zina mizengwe sana kuzipata maana wanaweka watu wao.

ila yote ya yote nashukuru kiasi japo mafanikio hayaendani na stress nazozipata kwa muajiri..

hali mbaya sana kwa kweli
Tuko wengi mkuu,hizo nyumba unazoziona zinasimama wengi hela zao wanajua wanakozipata,ingawa pia wachache ni hela za halali,vumilia utafanikisha tu siku moja maisha ni safari ndefu sana,hili ni funzo pia kwa wale wanaocheka baadhi ya watu kukuta anastaafu nyumba haijakwisha...
 
Acha kudanganya watu wewe, Taasisi gani wanaotoa ongezeko la mshahara kwa karibu ASILIMIA 100? Bila uongo na kutaka kujisifu kwa jambo usilokuwa nalo, maisha hayaendi?
Umeharibu uzi hapo tu, sawa sawa?
Kilichofanyika ni " recategorization" yaani wameniweka kwenye kiwango nnachostahili kulipwa. Watumishi wanajua hii kitu
 
Naona wengi hawajamuelewa mleta mada sijui ni stress au ni ugumu wa kuelewa,

All in All, hongera mleta mada kwa ulipofikia jaribu pia kufanya biashara ili ukuze kipato chako.
 
Sina cha kukushaur lakin kwa salary hiyo ningelipwa kwa miaka mi 3 tu ningea mbali zaid hapoulipo...
 
Thanks God baada ya kutoka chuo nilipata kazi flani hivi ya mkataba, nilifanya marekebisho katika nyumba ya wazazi wangu kwa kweli inakapendza, ilinicost karibu million 3 na Zaid, baada ya hapo nkanunua eneo langu kwa kiasi cha shilingi MIilion sita, mkataba ukaisha,
Ni kaingia katika biashara nikaweka msingi wa nyumba karibu na lenta, biashara I kaenda vibaya nashukuru Sana Mungu nkapigwa tafu na Baba mzazi hadi nikahamia kwangu,.
Pamoja na biashara ndogo ndogo lakini pia najifugia vikuku vyangu.
 
habari wadau..

leo ilikuwa tarehe niliyomaliza chuo kikuu mwaka 2009...

nilibahatika kupata ajira ya kwanza mapema sana mwezi mmoja baada ya kuhitimu chuo mwaka 2009..

toka mwaka huo mpaka leo nimebadili waajiri zaidi ya mara 5 kutafuta greaner pasture...

na katika harakati zote hizo mshahara wa juu kuwahi kulipwa ni milioni moja na elfu 30 net...

najaribu kupima mafanikio ya kufanya kazi miaka 10..

siyaoni makubwa zaidi ya chumba na sebule nilichojenga tabata segerea napoishi..na gari ndogo nayoitumia.. na hapo mimi ni mbahili vibaya mno hata buku naithamini

vijana ambao hamjapata ajira... msisikitike sana kukosa ajira jitumeni kwenye ujasiriamali.. ajira nyingi hazilipi.. ni ajira chache sana ambazo zinalipa na zina mizengwe sana kuzipata maana wanaweka watu wao.

ila yote ya yote nashukuru kiasi japo mafanikio hayaendani na stress nazozipata kwa muajiri..

hali mbaya sana kwa kweli
Chunga matumizi yamo mkuu,mi kwa mshahara huo nimejenga nyumba kubwa ya 45mil, nina viwa ja vingine 2, nimenunua gari mara mbili, yaan natumia nauza naongeza hela nanunua tena. Usisahau mm ni mwalimu
 
um

Tatizo la kukurupuka na hesabu za mezani ni ugonjwa mkubwa sana miongoni mwa wa Tanzania wengi. Hio ajira ukute ndio aliyoipata mwishoni ina maana kuna uwezekano alisota zaidi ya miaka mitano akiwa na kipato cha chini ya laki 5!
Ukumbuke kabla hajajenga its obvious alipanga apartment kama sio geto ambalo lilikuwa linakula pesa, nauli za

Dsm kama mnavyojua wengi kazi wanapofanyia na maeneo wanayoishi ni kama usiku na mchana ila muajiri anataka uwepo ofisini on time. Kuna kula na kuumwa pia. Bado mama hajapiga simu umtumie kahela ka mdogo wako anayeenda shule umchangie mahitaji, bado starehe and trust me hata uwe bahili kiasi gani kwa Dar ukiwa na kazi starehe lazma ufanye tu hata kama ni kuvuta sigara.

Sasa unapoongela 120M kizembe sidhani kama hata mtoa mada ameshakifikisha hiko kiwango katika mishahara yake yote.
Kwa kweli hata kwenda kula nyama choma weekend. Na hamna maana ya kufanya kazi kama hujipi nafasi ya kutumia pesa yako. Unajibana tu mpaka damu ya mwisho.
 
Tuseme kwamba ulikua unalipwa wastani wa 1,000,000 kwa mwezi hiyo 30,000 tuitoe.

Kwa 1000,000 kwa mwezi ni sawa na 12,000,000 kwa mwaka, kwa miaka 10 ni sawa 120,000,000. Ujenzi wa nyumba wa vyumba 3 na sebule, choo ina cost 35,000,000.

120,000,000 - 35,000,000 = 85,000,000. Je ulishindwa kutumia 85,000,000 matumizi mengine iliyobaki ukajenga nyumba?
Hesabu hizi tuna assume other factor is constant.

Hebu tafakari haya mawazo.
Hizi hesabu zako sio realistic ndugu
 
Unalipwa Million Cash?

Duh mim namshkuru Mungu okota okota zangu 5yrs nilishakamilisha makubwa zaid...
 
Tuseme kwamba ulikua unalipwa wastani wa 1,000,000 kwa mwezi hiyo 30,000 tuitoe.

Kwa 1000,000 kwa mwezi ni sawa na 12,000,000 kwa mwaka, kwa miaka 10 ni sawa 120,000,000. Ujenzi wa nyumba wa vyumba 3 na sebule, choo ina cost 35,000,000.

120,000,000 - 35,000,000 = 85,000,000. Je ulishindwa kutumia 85,000,000 matumizi mengine iliyobaki ukajenga nyumba?
Hesabu hizi tuna assume other factor is constant.

Hebu tafakari haya mawazo.
Ingekuwa hayo mahesabu yanakubali kukaa kwenye uhalisia, watu wengi wangeishi maisha mazuri kiasi. Hata hivyo, kufanya mahesabu ni muhimu sana kws mtu yoyote maana ukibugi kidogo tu baaaasiii.

Mfano, watumishi wa umma wanapenda sana kukopa mkopo wa miaka mitano, ukifanya mahesabu vibaya tu ukakosea mkopo wa kwanza! Inakubidi usubiri miaka mingine mitano ya kujipanga unless una vyanzo vingine vya fedha
 
Back
Top Bottom