Imenichukua miaka 10 kujenga chumba na sebule , na kunua gari aina ya terrios kid - kweli ajira nyingi hazilipi zama hizi

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,585
2,000
habari wadau..

leo ilikuwa tarehe niliyomaliza chuo kikuu mwaka 2009...

nilibahatika kupata ajira ya kwanza mapema sana mwezi mmoja baada ya kuhitimu chuo mwaka 2009..

toka mwaka huo mpaka leo nimebadili waajiri zaidi ya mara 5 kutafuta greaner pasture...

na katika harakati zote hizo mshahara wa juu kuwahi kulipwa ni milioni moja na elfu 30 net...

najaribu kupima mafanikio ya kufanya kazi miaka 10..

siyaoni makubwa zaidi ya chumba na sebule nilichojenga tabata segerea napoishi..na gari ndogo nayoitumia.. na hapo mimi ni mbahili vibaya mno hata buku naithamini

vijana ambao hamjapata ajira... msisikitike sana kukosa ajira jitumeni kwenye ujasiriamali.. ajira nyingi hazilipi.. ni ajira chache sana ambazo zinalipa na zina mizengwe sana kuzipata maana wanaweka watu wao.

ila yote ya yote nashukuru kiasi japo mafanikio hayaendani na stress nazozipata kwa muajiri..

hali mbaya sana kwa kweli
 
jajuu

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
325
500
Sawa mkuu...
FB_IMG_15640751856760575.jpeg
 
mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
2,638
2,000
Mkuu ulikaa mwezi 1 tu wenzako mwaka 3 yaani siku 1000+ hawana la kufanya,kilimo hola,mifugo hola,biashara hola yani hali mbaya.ukimaliza kufanya mengine waza namna ya kupata ajira ambayo itakuwa indirect yaani uingize passive income.Nunua bodaboda mpya au za zamani mpe kijana kwa wiki atakupa 40 elfu au 50 elfu.itakusogeza kimtindo maana mshahara utakuwa hauugusi kwa mambo madogomadogo.
 
kichekoh

JF-Expert Member
Sep 19, 2015
810
1,000
Tuseme kwamba ulikua unalipwa wastani wa 1,000,000 kwa mwezi hiyo 30,000 tuitoe.

Kwa 1000,000 kwa mwezi ni sawa na 12,000,000 kwa mwaka, kwa miaka 10 ni sawa 120,000,000. Ujenzi wa nyumba wa vyumba 3 na sebule, choo ina cost 35,000,000.

120,000,000 - 35,000,000 = 85,000,000. Je ulishindwa kutumia 85,000,000 matumizi mengine iliyobaki ukajenga nyumba?
Hesabu hizi tuna assume other factor is constant.

Hebu tafakari haya mawazo.
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,585
2,000
nimependa ulivyosema other factor is constant.... maana hapo umekadiria ajira ya kwanza tu nililipwa milioni na hata ajira zote mpaka leo nalipwa milioni... makadirio yako hayapo sahihi...

na umehisi sitegemewi na mtu yoyote kitu ambacho sio sahihi kwa familia za ki Tanzania

Tuseme kwamba ulikua unalipwa wastani wa 1,000,000 kwa mwezi hiyo 30,000 tuitoe.

Kwa 1000,000 kwa mwezi ni sawa na 12,000,000 kwa mwaka, kwa miaka 10 ni sawa 120,000,000. Ujenzi wa nyumba wa vyumba 3 na sebule, choo ina cost 35,000,000.

120,000,000 - 35,000,000 = 85,000,000. Je ulishindwa kutumia 85,000,000 matumizi mengine iliyobaki ukajenga nyumba?
Hesabu hizi tuna assume other factor is constant.

Hebu tafakari haya mawazo.
 
sinajinasasa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
2,286
2,000
habari wadau..

leo ilikuwa tarehe niliyomaliza chuo kikuu mwaka 2009...

nilibahatika kupata ajira ya kwanza mapema sana mwezi mmoja baada ya kuhitimu chuo mwaka 2009..

toka mwaka huo mpaka leo nimebadili waajiri zaidi ya mara 5 kutafuta greaner pasture...

na katika harakati zote hizo mshahara wa juu kuwahi kulipwa ni milioni moja na elfu 30 net...

najaribu kupima mafanikio ya kufanya kazi miaka 10..

siyaoni makubwa zaidi ya chumba na sebule nilichojenga tabata segerea napoishi..na gari ndogo nayoitumia.. na hapo mimi ni mbahili vibaya mno hata buku naithamini

vijana ambao hamjapata ajira... msisikitike sana kukosa ajira jitumeni kwenye ujasiriamali.. ajira nyingi hazilipi.. ni ajira chache sana ambazo zinalipa na zina mizengwe sana kuzipata maana wanaweka watu wao.

ila yote ya yote nashukuru kiasi japo mafanikio hayaendani na stress nazozipata kwa muajiri..

hali mbaya sana kwa kweli
Mkuu una matumizi mabaya ya fedha, unalipwa hela nyingi lakini huna maendeleo ya maana, mimi niliajiriwa mwaka 2008, nilianza kulipwa 150,500/= kama basic salary.
Nikapanda mshahara hadi kufikia basic salary ya 505,000/= mwaka huu
Nikapanda tena mwaka huu hadi kufikia 1,000,000/=
Lakini mafanikio ni kuwa na nyumba ya thamani ya zaidi ya 50,000,000,/= na pia kuwa na kagari ka Mitsubishi ambako nilikaagiza Japan mwaka 2012.
Hata hivyo nina kabiashara ka reja reja kiosk cha mtaani ndo kamenifikisha hapo.
Jitahidi kuongeza strategy za pesa
 
Pyaar

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
14,821
2,000
Tuseme kwamba ulikua unalipwa wastani wa 1,000,000 kwa mwezi hiyo 30,000 tuitoe.

Kwa 1000,000 kwa mwezi ni sawa na 12,000,000 kwa mwaka, kwa miaka 10 ni sawa 120,000,000. Ujenzi wa nyumba wa vyumba 3 na sebule, choo ina cost 35,000,000.

120,000,000 - 35,000,000 = 85,000,000. Je ulishindwa kutumia 85,000,000 matumizi mengine iliyobaki ukajenga nyumba?
Hesabu hizi tuna assume other factor is constant.

Hebu tafakari haya mawazo.

Toka mwaka huo mpaka leo nimebadili waajiri zaidi ya mara 5 kutafuta greaner pasture...

na katika harakati zote hizo mshahara wa juu kuwahi kulipwa ni milioni moja na elfu 30 net...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom