iNine9
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 4,240
- 7,818
FM - Frequency Modulation ni masafa ambayo yanahitaji mtambo kurusha matangazo sehemu husika na kwa umbali flani, Kuna mtambo wa kurusha umbali wa Km 50, km 150 na mpaka km 300, Ndio maana unaona Redio stations wana mitambo kila mkoa na inarusha kwenye Frequencies tofauti na mkoa mwingine ili kuzuia muingiliano wa mawimbi na pia mawimbi hayo yanaweza kua affected na mazingira na uasili wa eneo kama joto (Ndio maana ikinyesha mvua radio zinashika sana waliosoma Physics wanaelewa ni kwanini inakuaga hivyo), milima na miinuko, mabonde na umbali... Asa Mwanza ni jiji lenye milima na miamba hivyo tegemea madhaifu ya usikivu kwa mtu anaekaa vijijini...Ukisikiliza radio free wanadai wapo africa nzima kumbe kuna mahali hapo hapo mwanza hawapatikani kwa frequency za fm malofa tu.
Pia Radio Free Africa inarusha matangazo kwenye masafa ya Automatic Modulation (AM) hii haiitaji hata Eria ya radio yako iwe ndefu mpaka juu ya nyumba wala haina zile kelele za chaaaaaa! Na kama radio iko kwenye hii Modulation hivyo unaweza kuswitch na kuisikiliza popote ulipo ndio maana Radio Free Africa hata ukiwa Libya, Mauritius, Mali, South Africa n.k unaweza iskiza tu ukiweka AM, hata TBC Taifa, KBC Radio Taifa (Kenya) ziko huko na unaweza kuziskiza popote Africa.... Nafikiri umeelewa kwanini wanasema hivyo kusikika Africa nzima..