Imekuwaje Kiss FM kuanza kutumia Kiswahili?

Ukisikiliza radio free wanadai wapo africa nzima kumbe kuna mahali hapo hapo mwanza hawapatikani kwa frequency za fm malofa tu.
FM - Frequency Modulation ni masafa ambayo yanahitaji mtambo kurusha matangazo sehemu husika na kwa umbali flani, Kuna mtambo wa kurusha umbali wa Km 50, km 150 na mpaka km 300, Ndio maana unaona Redio stations wana mitambo kila mkoa na inarusha kwenye Frequencies tofauti na mkoa mwingine ili kuzuia muingiliano wa mawimbi na pia mawimbi hayo yanaweza kua affected na mazingira na uasili wa eneo kama joto (Ndio maana ikinyesha mvua radio zinashika sana waliosoma Physics wanaelewa ni kwanini inakuaga hivyo), milima na miinuko, mabonde na umbali... Asa Mwanza ni jiji lenye milima na miamba hivyo tegemea madhaifu ya usikivu kwa mtu anaekaa vijijini...

Pia Radio Free Africa inarusha matangazo kwenye masafa ya Automatic Modulation (AM) hii haiitaji hata Eria ya radio yako iwe ndefu mpaka juu ya nyumba wala haina zile kelele za chaaaaaa! Na kama radio iko kwenye hii Modulation hivyo unaweza kuswitch na kuisikiliza popote ulipo ndio maana Radio Free Africa hata ukiwa Libya, Mauritius, Mali, South Africa n.k unaweza iskiza tu ukiweka AM, hata TBC Taifa, KBC Radio Taifa (Kenya) ziko huko na unaweza kuziskiza popote Africa.... Nafikiri umeelewa kwanini wanasema hivyo kusikika Africa nzima..
 
nilianza sikiliza choice kuanzia 2013 akina vanessa mdee, baby kabae , tandy , big O, Chris na Abby ( yule dada wa Nirvana/big brother)
ghafla mwaka jana August nikaanza sikia singeli, na watangazaji wa Tandale

wakahamia classic fm
akina Seba the warrior, Dee Andy, Abby na Jimmy Kabwe
wakaa miezi miwili tu nikaanza skia singeli tena, ikawa ndio mwisho wa kusikiliza FM Radio
uame na nchi kabisa😈
 
Ume
Acha kabisa Kiss Fm ilikuwa moto Tob the Splash,D7 ,Karan Dj dev ,maliz ,Jeff Jelly ,Eyo criss men ,Claudia Mayanka na Marehemu Joakim Mungaligulu .
Kisss Fm Kiss Fm ...tyu..tyu...tyu afu katikati ya milazo unasikia DD..dj Maliz
Umemaliza mkuu ,kiss hakika ilikuw bomba enzi hizo.
 
Ndo ujue kuwa soko la kiingereza bongo ni gumu mno. Contents za kiingereza audience ya kiswahili ni mtihani huo, yaani hapo Advertisers watawapita tu kama hawawaoni vile. Same to East Africa Radio ilikua inaendeshwa kiingereza + Kishua shua walivoona wadhamini wanawakimbia wakarudi wenyewe kwenye kiswahili.

Media zenye contents za kiingereza Tanzania hazina faida zinakula hasara everyday.
Generation ya watoto wako going forward mnaowapeleka English Medium ambao ni wengi actually,watazungumza Kingereza...

Na wao watoto wao (ambao watakua wajukuu zako) watakua wanazungumza Kingereza more often...

Is the matter of time,na rais serious kama Lissu,nchi itageuzwa ya Kingereza kama Kenya....wait and see!
 
Generation ya watoto wako going forward mnaowapeleka English Medium ambao ni wengi actually,watazungumza Kingereza...

Na wao watoto wao (ambao watakua wajukuu zako) watakua wanazungumza Kingereza more often...

Is the matter of time,na rais serious kama Lissu,nchi itageuzwa ya Kingereza kama Kenya....wait and see!

Maybe baada ya miaka 25 hivi ndo kiingereza kitashika hatamu kwenye vyombo vya habari.
 
Acha kabisa Kiss Fm ilikuwa moto Tob the Splash,D7 ,Karan Dj dev ,maliz ,Jeff Jelly ,Eyo criss men ,Claudia Mayanka na Marehemu Joakim Mungaligulu .
Kisss Fm Kiss Fm ...tyu..tyu...tyu afu katikati ya milazo unasikia DD..dj Maliz
Bila kusahau na kipindi cha Kiss in Araab kilikuwa jpili, hapo ngoma kali za kina Diana Karlazon, Nancy Ajram na musicians wengeni wakali toka mashariki ya Kati, fm ilikuwa ni
 
Kitu kingine KISS fm ni tune yake tu, sijui walikuwa na mitambo ya aina gani yaani ukifungulia tu Ina tune nzuri sana na sauti kwa ujumla. Big up kiss fm... TBT
Sio Kiss fm pekee ata Radio free nayo ilikuwa na tune ya kipekee sauti inatoka kama vile anaetangaza upo nae karibu
 
Nakumbuka miaka ya 2006,7 mpaka na 10 mwanzoni Kiss Fm alikuwepo jamaa akiitwa somebody Kim au Kimattare jamaa alikuwa anaendesha kipindi flani kikipiga ngoma Old School kuanzia saa 14:00 mpaka 16:00 alaasiri aisee jamaa alikuwa anajua,hiyo lugha aliyokuwa anapandisha nadhani hakuishi bongo maana alikuwa anaongea ile slang yenyewe.

Pia alikuwepo sister mmoja akiitwa nadhani Farida/Waridi walikuwa vizuri sana walipohama na mimi nikaachana nayo.
Swali;huyu jamaa Kim yupo wapi/station gani siku hizi?
Kama nakumbuka vema hicho kipindi mi nilikifahamu kama hip hop dungeon kilikua kinapiga ngoma za hatari kwa mpangilio. Kilichokua kinavutia ni yule mtangazaji wake nakumbuka jina kama sheyza mungirwa (sina hakika sana) ila alikuwa mzimbabwe….alikuwa anaongea sleng nzuri na sauti tamu sana...Nakumbuka alikuwa anaruhusu kutuma sms na hata kupiga simu….kuna jamaa alikua anapiga sana simu akijiita suwaside president....Wakati umeenda wapi jamani
 
Yeah! Weekend Top 30 pia kilikua kinaendeshwa na Radio Express ya Marekani chini ya mtangazaji mmoja jina limenitoka ila pia DJ PUP DAWG huwa ni HOSt wa hiki kipindi mpaka sasa...

Radio Express Inc. Ikishirikiana na Coca-Cola. Inatangazwa kote Afrika kupitia Local stations ikiwemo Kiss FM yetu (Saivi ndo ivo tena hakipo), Homeboyz FM ya Kenya, XFM ya Uganda, Malawi, Zambia na Mozambique, Nigeria n.k hizo ni baadhi tu ya nchi ambazo waliingia nazo partnership na lengo ni kuwafikia vijana wa Kiafrika kwa kusisitiza juu ya vitu chanya kwenye maisha yao na "kiburudisho" Pia kupiga muziki wa zamani na kisasa hasa Hip-Hop na R&B kutoka America na Afrika, hadithi za wasanii, habari na exclusive interviews.

Hii Radio Express pamoja na Coca-Cola Ndio iliyokua inaendesha kile kipindi cha Coca-Cola Open Happiness Mix Show chini ya DJ A-1 na Dj Sway-Z siku za Jumapili asubuhi, Zilikua zinapigwa ngoma za hatari si unajua tena muziki wa nyuma kidogo ulikua muziki kweli na radha ake yenye vibe...
Asee jamaa umenigusa kinoma mtangazaji vocal yake ilikuwa yakipekee nilikuwa nakipenda sana hicho kipindi yani mdudu alieingia Kiss na RFA alaaniwe kabisa.
 
Dah nimemkumbuka D7 na mwenzake nimemsahau, nikiwa msingi na sekondari, 2006 hivi kuendelea, Ni lazima kipindi chake nikisikilize had nikanunua redio shuleni, ilikua kuanzia mida ya SAA 12 jion hadi kwenye SAA 2 hiv usiku, tupo bwenini nimefungulia sauti hadi mwisho,zinapigwa ngoma za ukweli..
Those days nilikua na amani sana huyu mwamba, kama sikosei jina kamili anaitwa Hassani Wibonela, aka D7 na hata marehem mabovu alipitia kiss pia, John karani enzi zake aka JK na binti Farida ilikua nyoko
 
Kiss fm ya kipindi hicho kwa kweli ilikua poa sana aiseeh! Nlkua nakikubari kipindi cha Kiss Collabo MixShow chini ya DJ Alleco na wengine wengi walikua wanapiga hiki kipindi, The Most Wanted chini ya DJ Simba na Afro beats chini ya DJ Maliz na D7 au The Voice Character/Mbaba VC (Huyu jamaa alihamia Jembe FM akawa na NATT E ila aliondoka... Mnaoskiza Wasafi FM ile Jingo ya DJ Delvick ni ya Mababa VC na yale matangazo ya sauti nzito nzito hivi kuhusu frequencies mpya za Wasafi FM za Mbeya na Arusha ndio sauti ya Mbaba VC alitoka Jembe FM na DJ Jecko wote hawa wamepita Kiss FM miaka kadhaa nyuma! Kipindi kingine The big fuse chini ya DJ Jeff Jerry/rapper huyu mchizi ni DJ ila ni rapper pia, alikua anapiga zile Hip-hop konki za kibongo na za majuu pia japo sio sana....

DJ Simba kutoka kipindi cha The Most Wanted alihamia kwenye TV ya Star Muzik akawa anamix videos huko.. Pia alikua ni mwl wa chuo cha uDJ hapohapo Mwanza na hao ma DJ wanafunzi ndo walikua wanakuja kufanya field hapo Kiss FM, So kama ulkua unasikia ma DJ wapya wengi wasio wa kudumu pale Kiss fm na RFA ambao kama wanajifunza ni wanafunzi wake!

Dj Dev aliacha u DJ akaokoka.. Dj Maliz mtoto wa Mbeya huyu, kuna siku alikuja likizo kwao Mbeya akapata mwaliko Access FM akapiga show kali kama enzi zake pale Kiss FM...

Dj John Lyatu wa RFA sijui yukogo wapi hata, japokua umri ulkua umemtupa mkono...

Kuna huyu Alleco sijui yukogo wapi tu, maana Kiss walikua na DJs wanaofit kwenye vipindi vya enzi hizo...

Kichaka kichwa cha kazi nae sijui aliendaga wapi tu...

D7 mkali wa kumix reggae alitokaga akaenda Abood FM ya Moro ila tena nlmsikia karudi Kiss FM... Wapo wengi sana, wengine nmewasahau ambao walikua wanaifanya Kiss kua kweli Redio nzuri sana..

R.I.P Old Kiss FM
................................................................................................................
Dj John lyatuu nahisi amesepa unyamwezini, kama sikosei last time nilipokua home kwa mzee wake akaniambia familia imerud chuga
 
Back
Top Bottom