Imekuwaje Kiss FM kuanza kutumia Kiswahili?

Mr. Marangu

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,564
1,512
Na declare interest nina muda kama miaka 6 sijawa msikilizaji ama mfuatiliaji wa Kiss Fm, by the time nilipokua nawafuatilia 2014 kurudi nyuma vipindi vingi viliendeshwa kwa lugha ya Kiingereza isipokua cha African beats. Back to mwezi huu wa tisa 2020 nilisearch mara paah Kiss hiyo hapo, ilikua majira ya saa12 asubuhi nikastaajabishwa na kipindi wanakiita Dimba dogo kilikua kinaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, baada ya hapo nimekua nikifuatilia nakugundua vipindi kama sio vyote basi vingi vinaendeshwa kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

Swali langu nini kiliwapata mpaka wakarudi kwa lugha ya taifa, ni watangazaji wabobevu kwenye lugha kuondoka? Vibali vya TCRA au?
 
Ndo ujue kuwa soko la kiingereza bongo ni gumu mno. Contents za kiingereza audience ya kiswahili ni mtihani huo, yaani hapo Advertisers watawapita tu kama hawawaoni vile. Same to East Africa Radio ilikua inaendeshwa kiingereza + Kishua shua walivyoona wadhamini wanawakimbia wakarudi wenyewe kwenye Kiswahili.

Media zenye contents za kiingereza Tanzania hazina faida, zinakula hasara everyday.
 
Hapa umegusa ki commercial nimekupata boss
Ndo ujue kuwa soko la kiingereza bongo ni gumu mno. Contents za kiingereza audience ya kiswahili ni mtihani huo, yaani hapo Advertisers watawapita tu kama hawawaoni vile. Same to East Africa Radio ilikua inaendeshwa kiingereza + Kishua shua walivoona wadhamini wanawakimbia wakarudi wenyewe kwenye kiswahili.

Media zenye contents za kiingereza Tanzania hazina faida zinakula hasara everyday.
 
Nakumbuka miaka ya 2006,7 mpaka na 10 mwanzoni Kiss Fm alikuwepo jamaa akiitwa somebody Kim au Kimattare jamaa alikuwa anaendesha kipindi flani kikipiga ngoma Old School kuanzia saa 14:00 mpaka 16:00 alaasiri aisee jamaa alikuwa anajua, hiyo lugha aliyokuwa anapandisha nadhani hakuishi bongo maana alikuwa anaongea ile slang yenyewe.

Pia alikuwepo sister mmoja akiitwa nadhani Farida/Waridi walikuwa vizuri sana walipohama na mimi nikaachana nayo.
Swali;huyu jamaa Kim yupo wapi/station gani siku hizi?
 
Nilikuwa sikosi hiko kipindi chao cha African Beats na American top 30
American Top 30 ilikuwa balaa, nakumbuka kipindi hiko kina Fid Q, hawa watoto wa Arusha Nako 2 Nako ndio wanawika town basi ilikuwa kawaida sana kuwasikia studio waki-free style kimalkia.

Ule ubunifu nadhani aliyeuanzisha walimdhulumu akaacha laana akaondoka na vipaji vyote.
 
Ndo ujue kuwa soko la kiingereza bongo ni gumu mno. Contents za kiingereza audience ya kiswahili ni mtihani huo, yaani hapo Advertisers watawapita tu kama hawawaoni vile. Same to East Africa Radio ilikua inaendeshwa kiingereza + Kishua shua walivoona wadhamini wanawakimbia wakarudi wenyewe kwenye kiswahili.

Media zenye contents za kiingereza Tanzania hazina faida zinakula hasara everyday.
Hata Passion Fm ndugu yake Clouds wameinua mikono,sasa hivi ni Kiswahili tu.
 
Back
Top Bottom