Imejirudiarudia

Imejirudiarudia

D ya nkola

New Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
3
Reaction score
1

Adaiwa kuwa bilionea kwa mgongo wa Ikulu
Na Mwandishi wetu - Tanzania Daima.


RAIS Jakaya Kikwete anakabiliwa na kashfa nzito kutokana na utajiri wa mtoto wake, Ridhiwani. Sasa anatuhumiwa kuitumia Ikulu kumtajirisha mwanawe, ambaye anasemekana ni bilionea.
Kwa nyakati mbalimbali, ukwasi wa mtoto huyo wa rais uliibuliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila.
Katika moja ya mikutano yake ya hadhara hivi karibuni mkoani Tabora, Dk. Slaa alisema Ridhiwani amemaliza shule miaka michache iliyopita, lakini hivi sasa ni tajiri bilionea na kwamba ameupata utajiri huo katika mazingira ya kutatanisha.
Jana Mtikila alizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Travertine, akidai Ridhiwani amegeuka bilionea kwa muda mfupi ?kwa mgongo wa baba yake.?
Akibainisha zaidi uwezo wa kifedha wa kijana huyo, Mtikila alisema hivi karibuni mtoto huyo ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), aliingiza magari makubwa ya mizigo aina ya ?semi trailer? zaidi ya 100 na kudai kuwa yanafanya kazi ya kusomba mizigo DRC na mengine ameyauza.
Alidai pia mtoto huyo wa rais anamiliki makampuni ya ujenzi wa barabara na maeneo mengi ya ardhi kwa lengo la kujenga maghorofa ya kupangisha.
?Huyu ni mtoto mdogo, kamaliza shule juzi, pesa za utajiri wote huu kazipata wapi?? alihoji Mtikila.
Hata hivyo, wiki iliyopita, Ridhiwani alikaririwa na moja ya vyombo vya habari akisema kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano kwa Dk. Slaa kuonyesha kila anachomiliki.
Kutokana na tuhuma hizo, Mtikila alimtaka Rais Kikwete naye ajivue gamba kwa kuonyesha mfano, vinginevyo ni uendawazimu kujivua gamba bila mkuu huyo wa nchi kujiuzulu urais na uenyekiti wa CCM.
Huku akionekana kuwatetea Edward Lowassa (Monduli), Andrew Chenge (Bariadi Magharibi) na Rostam Aziz (Igunga), Mtikila alisema Kikwete an​
 
Back
Top Bottom