Imei namba moja, serial namba tofauti

Imei namba moja, serial namba tofauti

Boiker

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2015
Posts
349
Reaction score
470
Habarini,

Nimeona nilete hili swala kwenu maana limenipa utata sana ili nipate mawazo yenu.

Nmepoteza simu yangu iphone 12 pro, sasa katika kuitafuta kwa kushirikiana na polisi(cyber unit) tumefanikiwa kuipata, sasa cha kushangaza imei namba iliyopo kwenye box lake na ya simu ipo sahihi kwa kila kitu ila serial namba ni tofauti.

Nachouliza inawezekanaje imei namba iliyopo kwenye box la simu iwe sawa na ya simu alafu serial namba iwe tofauti pia ukiangalia rangi ya simu kwenye internet kwa imei namba ile ile ni tofauti na rangi ya simu iliyoandikwa kwenye box mfano kwenye box simu ni black alafu kwenye internet simu ni gold.

Wenye uelewa zaidi wa haya mambo karibuni tupeane darasa
 
Sasa kama umeshaipata unahangaika nini. Si ushaipata?
 
  • Thanks
Reactions: Mu7
Imepatikana lakini bado kuna mkanganyiko na utata mkubwa sana kwa tuliye mkuta nayo,ndo maana nkaja kuuliza huku
 
Imepatikana lakini bado kuna mkanganyiko na utata mkubwa sana kwa tuliye mkuta nayo,ndo maana nkaja kuuliza huku
ingiza login details za iCloud Account (kama iko logged in, log out then log in again), iyo itakupa majibu
 
Hiyo simu ni refub. itakuwa ishabadilishwa hata cover ya nje nk. acha kunua vitu used
 
Hiyo simu ni refub. itakuwa ishabadilishwa hata cover ya nje nk. acha kunua vitu used
Mkuu simu ni mpya kabsa wala sio refub maana hizi simu sijaanza kuzitumia leo ila nahisi jamaa watakua wamefanya mchezo mchafu sehem
 
Mkuu simu ni mpya kabsa wala sio refub maana hizi simu sijaanza kuzitumia leo ila nahisi jamaa watakua wamefanya mchezo mchafu sehem

jamaa gani wamefanya mchezo mchafu?? simu ni mpya ulinunua wapi?? ki msingi uliuziwa simu refub.

Chunguza emei na uangalie uhalisia wa simu.

Usijekua ulinunua makumbusho au Kko useme ni mpya
 
Ukute Wamebadilisha board. [emoji3526][emoji3526] lakini wakibadilisha board serial number haziwezi kubadilika, kama Imei zinaendana basi hiyo ndo simu yako. Serial number sio kitu cha kuzingatia sana ndo maana ukienda polisi hawaombi serial number bali huomba Imei number, so kikubwa hapo ni Imei number.
 
Kinacho onekana kwenye simu ndio sahihi, box si sticker tu Wana andika?
 
jamaa gani wamefanya mchezo mchafu?? simu ni mpya ulinunua wapi?? ki msingi uliuziwa simu refub.

Chunguza emei na uangalie uhalisia wa simu.

Usijekua ulinunua makumbusho au Kko useme ni mpya
Najua nnachokisema mkuu then mm sio wa kununua simu kkoo wala makumbusho twende polepole tu
 
Ukute Wamebadilisha board. [emoji3526][emoji3526] lakini wakibadilisha board serial number haziwezi kubadilika, kama Imei zinaendana basi hiyo ndo simu yako. Serial number sio kitu cha kuzingatia sana ndo maana ukienda polisi hawaombi serial number bali huomba Imei number, so kikubwa hapo ni Imei number.
Hili nna waswas nalo sana,ujue ile simu ina imei namba mbili yan imei1 na imei2 sasa hapa issue ilivo naomba unisikilize kwa makini bro ukiingiza imei1 kwenye ile imei check inakuletea details tofauti kabsa na details zilizopo kwenye box ambalo ndo nilichukulia simu mfano simu kwa box ni black bt ukiangalia kwenye imei check inasema ni gold

Then ukitumia imei2 kwenye imei check inakuletea details halisi za simu kama inavoonekana kwenye box mfano simu ni black hadi kwenye imei chek inaonesha black

Swali la msingi hapa ni kwann imei namba mbili za simu moja zilete majibu tofauti

Pia nmejaribu kuangalia kwenye simu ya jamaa angu 11promax ina imei namba mbili but inaleta majibu yaleyale kama inavoonekana kwenye box na kwenye imei check

Sasa kwann hii yangu inakua tofauti
 
Mkwawa haya mambo unayaelewa kwel[emoji16][emoji16][emoji16]

Unatumia simu gani kwanza
Simu ninayo tumia mimi ina mahusiano gani?

Iphone si kama simu za mediatek kwamba utaingia engineering mode na kuanza kubadili system, itahitaji kujailbreak and possibly kubadili hardware.

1.Kama kabadili board ina maana tayari hiyo ni simu nyengine, kama wanataka kufuatilia zaidi fundi ata husika.

2. Kama wame jailbreak pia ni rahisi kuitrace wametumia nini, exploit iliotumika itaelezea method.
 
Back
Top Bottom