Imegundulika kwenye sakata la Askofu Gwajima!

Imegundulika kwenye sakata la Askofu Gwajima!

Status
Not open for further replies.
Imetusikitisha sana kumbe nyuma ya kashfa alikuwa akidaiwa Askofu Gwajima juu ya Kardali Pengo ilikuwa ni ufunguo tu wa serikali kuingilia Imani na Utendaji wa Viongozi wa kidini (Askofu Gwajima) Iweje kashfa iliyokuwa inamuhusisha Kardinali Pengo na Askofu Gwajima ipelekee kuhojiwa na Kudaiwa alete nyaraka zinazohusiana na mapato na matumizi ya Kanisa la ufufuo na uzima, Kwani makanisa huwendeshwa na ruzuku kutoka serikalini !?, Je!

Kuna kanisa au dhehebu lolote la kidini wawe waislam au wakristo wameisha wahi kuhojiwa kuhusu mapato na matumizi ya madhehebu(makanisa/misikiti) yao!?

Wanapohoji nyaraka za helicopter kwani! Iliingia nchini kwa uficho!?.... Kwanini wasiene kuuliza TRA kama helicopter hiyo haikulipiwa ushuru !?

Kumbe tumegundua serikali na wanasiasa walioko madarakani wanaajenda ya siri juu ya Askofu Gwajima. Nchi yetu ina mambo mengi ya kushughulikiwa na serikali ili kutatua matatizo ya wananchi kama vile vifo vya albino, migogoro ya wakulima na wafugaji, matumizi mabaya ya fedha(ESCROW) na mikataba mibovu isiyo na manufaa kwa mtanzania mmoja mmoja .

Mambo kama haya yangekuwa yanafuatiliwa kwa karibu kama anavyofuatiliwa Askofu Gwajima ingeleta tija kwa uongozi uliopo madarakani na Imani kwa wananchi juu ya serikali yao.

NIA YA WAZI YA SERIKALI IMEJULIKANA

  1. WANAKUSUDIA KUMUANGAMIZA ASKOFU GWAJIMA KWA GHARAMA YEYOTE KABLA YA KAMPENI YA URAIS, WABUNGE NA MADIWANI KUFANYIKA.
  2. ASKOFU GWAJIMA AMEINGIZWA KATIKA ORODHA YA VIONGOZI WA KIJAMII WASIOTAKIWA KUWA HAI HAPA TANZANIA, AKIWEMO DR. SLAA NA LOWASA .
  3. NI KUCHOCHEA VURUGU KATI YA WAISLAMU NA WAKRISTO.

Kaa ukijua msajili wa kanisa au mosque ni serikali, kaa ukijua fedha yoyote inayotumiwa na mtu yoyote serikali inawajibu wa kujua ameipataje? Wewe na gwajima mlifikiri mkifika pale mtaulizwa kwa nini ulimtukana pengo basi na mimi ningeshangaa sana ingeishia hapo, mimi ni muumini wa pengo nimeumia kwa kiongozi wangu wa kanisa kufedheheshwa hadharani na huku watu wakishangilia anavyofedheheshwa kama wewe muumini wake endelea kutazama na kusikia uovu utakaofichuriwa na polisi juu ya gwajima na kisha utakuja kusema Kumbeeee
 
Nichukue nafasi hii kuwashauri walio busy kumtetea Gwajima.

1. Hakuna anayeweza kumtetea Gwajima. Mungu anayemwamini ndiye pekee atamtetea. Na kama itakuwa kupitia wewe then ni kwa magoti yako mbele za Mungu. Haitasaidia kushinda ukitishia watu hapa JF kuwa watapata laana! Tena wakati mwingine unayemwambia atalaaniwa bado yuko chini ya laana! Kumbuka Kristo ndiye alitukomboa chini ya laana! Sasa km unayemwambia utalaaniwa hata Yesu hajampokea ndio unafanya nini?

2. Wengi huingia kumtetea Gwajima ki mwili na ki-akili! Na wengine kufikia hata kusema maneno yasiyopaswa kutolewa na mtu aliyemwamini Yesu! Hatupigani vita vya kiroho kwa jinsi ya akili! Kwa sababu aliyesema yuko JF na wewe unakimbia kujibu JFf?! Hatupaswi kupambana na matokeo, tunapambana na chanzo! na chanzo HAKIKO JF wala polisi wala popote macho yetu ya damu nyama yanapoona. Unapambana kumtetea Gwajima JF Facebook au youtube? Unawaza kurudisha heshima ya Gwajima JF as if aliipata JF!? Heshima yake haikutoka huku... hivyo huwezi kuitengenezea huku!

3. Viongozi wa kanisa hasa msemaji wa kanisa (not sure km ni Pastor Eng. Y. Bihagaze ) unapaswa kutoa muongozo kwa washirika wanaotumia JF km platform ya kumtetea Senior Pastor. Please please! Hii si picha ya kanisa la Mungu! na hasa ukiongelea Glory of Christ Church! Si wakati wa kila mtu kusema na watu au JF, ila ni wakati wa kila mtu kusema na Mungu!

Nikianzia kwangu mwenyewe, nisingependa kuendeleza discussion hii lakini naamini ushauri wangu utafanyiwa kazi.

Kwa upendo wa Kristo,

Bwire.

c.c Eng. Y. Bihagaze
...................

c.c @ Nazjaz Angelo007 Head prefect BAOBAO geomos Precise Pangolin mjukuum rackel Fandre Hunyu Chesty Ta Muganyizi gfsonwin TAMKO hasason Fandre Asante
 
Last edited by a moderator:
Halafu umeandika kiupande mmoja:kwa nini usiandike wanaomtetea Gwajima na wanaomtuhumu?
 
Yaani umeandika kwa kujihesabia haki sijapata ona. Mara nyingine imani ina brain wash. Hivi nikuulize ; kusema Pengo yuko kama kavaa PAMPAZ sii tatizo ! kweli ni maneno tunayotarajia kutolewa na kiongizi wa dini mkubwa ! nyie endeleeni kubeba sadaka kwenye vikapu kumpelekea Gwajima afu yeye ananunua helkopta. Gwajima SIO malaika ! afu bado tuhuma za Flora Mbasha hazijaisha tayari kaleta jingine !
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom