Imegundulika, kisa cha mtoto wa Fred Lowassa kutogombea Monduli, Lowassa hataki familia yake iteseke

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Baada ya Mtoto wa Edward Lowassa, Fredy Lowassa kujitoa katika kinyang'anyito cha kugombea Ubunge wa Monduli kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imegundulika kuwa Fredy alijitoa kwa shinikizo la Baba yake kwa sababu kubwa kwamba Mzee Lowassa hataki familiq yake iteseke sababu ambayo hata hivyo bado haijaeleweka kwa wananchi wa Monduli.

Hata hivyo Wachunguzi wamebaini kuwa hatua hiyo inathibitisha mawazo ya wengi na hasa wakazi wa Monduli kuwa ndani ya Chadema kuna figisu figisu nyingi kwa viongozi wake hususani Wabunge. Aidha zipo taarifa kuwa zaidi ya Madiwani wanane waliokuwa wa Chadema kuchukua hatua ya kujiondoa katika chama hicho na kurudi CCM ni Maandalizi ya Lowassa ama kurudi CCM au kuachana na SIASA na hivyo haoni sababu ya familia yake kujihusisha na siasa wakiwa CHADEMA.

Upepo wa kisiasa kwa chama hicho kikuu cha Upinzani jimboni Monduli siyo mzuri na kuna dalili kuwa huenda Mgombea wa CCM ambaye pia alijiengua kutoka CHADEMA, bwana Julius Kalanga hatapata upinzani mkali.
Ikumbukwe kuwa Madiwani wote waliojiengua CHADEMA na kugombea tena kupitia CCM tayari wameshinda na kurudi katika nafasi zao za Udiwani.
 
Wana roho mbaya hao watoto wa huyo mzee!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hahahhahahaa maccm bwana yana shida.Ni kwamba wanaogopa miccm itaanza kuwachunguza uraia.wana uwezo wa kusema ni wakenya hawa,si raia wa Tanzania.walihamia Tanzania 1931. Hivyo warudi kenya.Maadui wa Tanzania ni maccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Freddy ni bora tu amejiondoa...maana hata angeshinda ni lazima angerudi kuunga mkono juhudi...

Hata baba yake ni suala la muda tu.
 
Back
Top Bottom