Imani ya ushirikina unavyotawala 90% ya uchimbaji dhahabu

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2013
Posts
9,116
Reaction score
8,662
Naamini hapa jukwaani kuna wadau wanaotamani siku moja kujiingiza katika uchimbaji mdogo na pia naamini kila mtu hapa ana imani yake kupitia makanisani ama misikitini.

Binafsi mimi ni muumini wa mungu aliye hai kupitia Ukristu (Kanisa)

USHIRIKINA MACHIMBONI
Nikiwa nimejiingiza katika uchimbaji nyumbani nikiwezeshwa na mwenyeji wangu ng'ambo,kwa kuanzisha mashapo mawili baada ya Geologist kuonyesha sehemu za kuchimba nilifanya kikao na wachimbaji na kuwaonya kutoshiriki imani yoyote ya ushirikina ikiwemo kwenda kwa waganga ukweli siku hiyo nilijikuta nikiwa peke yangu na hilo wazo pamoja na kijana mmoja mwenyeji wa Mbeya ambaye ndiye pekee aliniunga mkono. Nilitafakari sana aidha niwafukuze kazi hao wote waliokataa wazo langu la kumwabudu mungu pekee katika kazi hii ya uchimbaji.
Nilitafuta ushauri kwa marafiki zangu lkn kati yao wote niliowafuata kuchukua ushauri waliungana na wazo la wachimbaji kuwa ni lazima walete mtaalamu wao wa ramani na kumbuka kazi ilikuwa inaendelea.

NAWAPA RUHUSA YA IMANI YAO BILA MIMI KUSHIRIKI
Nilipoona siwezi kuwa control imani yao niliamua kuwapa ruhusa kwa masharti kuwa sitashiriki katika ibada zao ama masharti yao na walikubali.

BAADA YA MTAALAMU WAO KUJA
Mganga alikuja na bahati zuri nilikuwa namfahamu kwa vile anajulikana sana tangu nikiwa sijazamia nje nilimfahamu kwa matukio mbalimbali

MASHARTI ALIYOYAACHA
Alikaa na kufanya kazi kwa siku mbili akitambikia na nilichokifanya ni kumkarimu kwa chakula na sehemu ya kulala huku nikimwambia kabisa kuwa anisamehe kama takuwa nimemkwanza kwa kutoshiriki ibada zake na wachimbaji na namshkru aliniambia hata katika familia yao wana imani tofauti na kuna hadi walokole na yeye anaheshimu imani yao kama nilivyo Mimi

Alitoa masharti ikiwemo uelekeo wa mwamba wa madini ambapo maelezo yake yalilingana na Geologist ambaye mimi pekee ndiye aliniambia kipindi ananionyesha sehemu za kuchimba,aliwapatia maelekezo ya dawa za kuvukiza na mambo mengi tu ambayo ukweli siwezi kuyaweka yote hapa lakini aliwajulisha kuwa patatokea mambo makuu matatu:

1: Mvua (japo ni kiangazi kimeshaanza)
2: Watu wawili warefu (usiku)
3: Nyoka kwenye shimo

Baada ya siku nne nikiwa nimekaa karibia na shimo na kazi ya kutoa kifusi kutoka kwenye shampo ikiendelea alipanda mfabyakazi mmoja akiwa kasi na kutoa taarifa ya kuwemo nyoka mweusi. Binafsi nili suspect mambo mawili:

A: Atakuwa ameangukia humo kwa bahati mbaya
B: Aidha mganga kamleta ili niamini/tuamini

Lakini nilishindwa kabisa kupata jibu sababu asubuhi aliyekuwa zamu huko chini ni yule kijana wa Mbeya mlokole anayesimamia imani yake na hakumuona!!!

Nilijawa na ujasiri na kuamua kushuka huko chini lakini ajabu wakati mimi nimefika huko chini nilimuona akiwa ukutani huku niliyenae akiwa ananiambia simuoni. Wakati nikiwa huko chini mchimbaji mmoja alikuja na maji ya mtama uliosagwa ambao mganga aliwapa maelezo ya awali kuwa wakimuona wasimue wala kumfanyia fuji ispokuwa wammwagie maji hao ya mtama yakitokea mdomoni huku ukitaja mahitaji yako (Tuletee dhahabu!!). Nikiwa huko ilibidi nichukue simu yangu huku nikiwa natetemeka kupiga picha. Kwanza nilianza na mchimbaji akiwa anashuka na bakuli la hayo maji na nikapiga picha ya ukutani ya hili tukio.

BAADA YA TUKIO
Nimejifunza kuwa ni kweli uchimbaji umegubikwa na mazingaombwe sana (ushirikina) na huenda ni sababu kuu kuwa mali inayopatikana katika madini huwa mara nyingi haidumu

NB: NILITAMANI SANA KUIWEKA HILI JAMBO KAMA SIRI lakini kwa sababu ya usalama wa uliopo hapa jamii forum naamini sitasumbuliwa na mtu yoyote yule sababu bado naamini kuwa ninachokisimamia moyoni mwangu (imani yangu kwa mungu aliye hai) ndicho kinachompendezesha mungu.

Picha ya mchimbaji sitaiweka kwa sababu ya kanuni za hapa jamii forum. Atakayekuwa haamini "Nikipenda tamtumia private

IMG_20180528_111036.jpg
 
...Kaka ukisema hujashiriki kwenye huo ushirikina kutokana na maelezo yako nakataa. Kwanza wewe kumruhusu huyo mganga kuwepo kwenye mradi wako . ndo ushirika huo
Ni kweli mkuu lkn sikutaka kusimamisha kazi kwa imani za kipuuzi kama hizo
 
Kwahiyo kama una mafanikio?
nani alikudanganya mafanikio huwa yanatosha?
Nimesema mafanikio "kidogo" niliyoyapata hayakutegemea nguvu za giza na imani ya waganga wa jadi. Kama neno mafanikio limekukera pole
 
Hapo hukutakiwa waingilia wao ungewaachia wafanye wafanyalo wewe upate tu chako
 
Hii ni riwaya nzuri, una uwezo mzuri wa kutunga hadithi, nakushauri kamilisha hadithi yako uanze kuuza vitabu
 
Naamini hapa jukwaani kuna wadau wanaotamani siku moja kujiingiza katika uchimbaji mdogo na pia naamini kila mtu hapa ana imani yake kupitia makanisani ama misikitini.

Binafsi mimi ni muumini wa mungu aliye hai kupitia Ukristu (Kanisa)

USHIRIKINA MACHIMBONI
Nikiwa nimejiingiza katika uchimbaji nyumbani nikiwezeshwa na mwenyeji wangu ng'ambo,kwa kuanzisha mashapo mawili baada ya Geologist kuonyesha sehemu za kuchimba nilifanya kikao na wachimbaji na kuwaonya kutoshiriki imani yoyote ya ushirikina ikiwemo kwenda kwa waganga ukweli siku hiyo nilijikuta nikiwa peke yangu na hilo wazo pamoja na kijana mmoja mwenyeji wa Mbeya ambaye ndiye pekee aliniunga mkono. Nilitafakari sana aidha niwafukuze kazi hao wote waliokataa wazo langu la kumwabudu mungu pekee katika kazi hii ya uchimbaji.
Nilitafuta ushauri kwa marafiki zangu lkn kati yao wote niliowafuata kuchukua ushauri waliungana na wazo la wachimbaji kuwa ni lazima walete mtaalamu wao wa ramani na kumbuka kazi ilikuwa inaendelea.

NAWAPA RUHUSA YA IMANI YAO BILA MIMI KUSHIRIKI
Nilipoona siwezi kuwa control imani yao niliamua kuwapa ruhusa kwa masharti kuwa sitashiriki katika ibada zao ama masharti yao na walikubali.

BAADA YA MTAALAMU WAO KUJA
Mganga alikuja na bahati zuri nilikuwa namfahamu kwa vile anajulikana sana tangu nikiwa sijazamia nje nilimfahamu kwa matukio mbalimbali

MASHARTI ALIYOYAACHA
Alikaa na kufanya kazi kwa siku mbili akitambikia na nilichokifanya ni kumkarimu kwa chakula na sehemu ya kulala huku nikimwambia kabisa kuwa anisamehe kama takuwa nimemkwanza kwa kutoshiriki ibada zake na wachimbaji na namshkru aliniambia hata katika familia yao wana imani tofauti na kuna hadi walokole na yeye anaheshimu imani yao kama nilivyo Mimi

Alitoa masharti ikiwemo uelekeo wa mwamba wa madini ambapo maelezo yake yalilingana na Geologist ambaye mimi pekee ndiye aliniambia kipindi ananionyesha sehemu za kuchimba,aliwapatia maelekezo ya dawa za kuvukiza na mambo mengi tu ambayo ukweli siwezi kuyaweka yote hapa lakini aliwajulisha kuwa patatokea mambo makuu matatu:

1: Mvua (japo ni kiangazi kimeshaanza)
2: Watu wawili warefu (usiku)
3: Nyoka kwenye shimo

Baada ya siku nne nikiwa nimekaa karibia na shimo na kazi ya kutoa kifusi kutoka kwenye shampo ikiendelea alipanda mfabyakazi mmoja akiwa kasi na kutoa taarifa ya kuwemo nyoka mweusi. Binafsi nili suspect mambo mawili:

A: Atakuwa ameangukia humo kwa bahati mbaya
B: Aidha mganga kamleta ili niamini/tuamini

Lakini nilishindwa kabisa kupata jibu sababu asubuhi aliyekuwa zamu huko chini ni yule kijana wa Mbeya mlokole anayesimamia imani yake na hakumuona!!!

Nilijawa na ujasiri na kuamua kushuka huko chini lakini ajabu wakati mimi nimefika huko chini nilimuona akiwa ukutani huku niliyenae akiwa ananiambia simuoni. Wakati nikiwa huko chini mchimbaji mmoja alikuja na maji ya mtama uliosagwa ambao mganga aliwapa maelezo ya awali kuwa wakimuona wasimue wala kumfanyia fuji ispokuwa wammwagie maji hao ya mtama yakitokea mdomoni huku ukitaja mahitaji yako (Tuletee dhahabu!!). Nikiwa huko ilibidi nichukue simu yangu huku nikiwa natetemeka kupiga picha. Kwanza nilianza na mchimbaji akiwa anashuka na bakuli la hayo maji na nikapiga picha ya ukutani ya hili tukio.

BAADA YA TUKIO
Nimejifunza kuwa ni kweli uchimbaji umegubikwa na mazingaombwe sana (ushirikina) na huenda ni sababu kuu kuwa mali inayopatikana katika madini huwa mara nyingi haidumu

NB: NILITAMANI SANA KUIWEKA HILI JAMBO KAMA SIRI lakini kwa sababu ya usalama wa uliopo hapa jamii forum naamini sitasumbuliwa na mtu yoyote yule sababu bado naamini kuwa ninachokisimamia moyoni mwangu (imani yangu kwa mungu aliye hai) ndicho kinachompendezesha mungu.

Picha ya mchimbaji sitaiweka kwa sababu ya kanuni za hapa jamii forum. Atakayekuwa haamini "Nikipenda tamtumia private

View attachment 788220
Nipe namba ya huyo "mtaalamu" [emoji3][emoji3]
 
Vipi sasa dhahabu ilitema?
 
Mimi nataka ninunue mawe ya dhahabu ( makinikia) then nisage nipe pure gold nipe shule kidogo, huko shimoni niwaachie washirikina sipawezi.
Hapa unatakiwa uwe na ma crusher yako moja au mbili za kuanzia. Unaposaga unakuwa na mwalo wako wa kuosha na kukamatisha (lugha za machimboni) dhahabu kwa mercury. Uchimbaji una gharama na mambo ya ovyo kama haya ya kuamini dhahabu utaipata kwa ushirikina huku huyo mganga akiwa na ndugu na marafiki maskini na fukara lkn kashindwa kuwatajirisha. Wachimbaji imani yao ni ngumu sana kuwashawishi kumwamini mungu pekee na ukiwa against nao wanaweza hata kukuachia shimo bila wafanyakazi. Cha msingi ukianza uchimbaji baki na imani yako tu
 
Ungeendelea basi tujue uliipata na ulifanikiwa kuuza kwa imani ipi maana 😱😱😱

Na kwa wewe kuwasubiria wakupatie mali hapo nami naona ulikubali kwa kupitia wao na rohoni hadi ukajua waliambiwa nini na nini 😱

Mshana Jr njoo huku usome
 
Back
Top Bottom