Imani ya chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imani ya chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kajuni, May 14, 2011.

 1. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Jamani kwa kweli baba wa taifa alikuwa na malengo na nia nzuri sana kwa watanzania. Ebu tuziangalie imani za chama chetu cha Mapinduzi. Nita nukuu....

  Chama kinaamini kwamba:-

  Binadamu wote ni sawa.
  Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.

  Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.

  Kweli imani hizi zinatekelezeka? au zimepitwa na wakati? au ni nzuri kuzitamka mdomoni? Tafakari.
   
 2. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Je wenzetu imani ya chama chao ni nini? nikianza na CDM? au wame copy.... jamani hakika tuwape muda hawa jamaaa ndo wameaza kurejea kwenye misingi ya chama. Na ukubwa ni dawa pia zimwi likujualo.......
   
 3. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Kidumu chama cha mapinduziiiiiiiiii
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu Mwalimu Nyerere na waasisi wa taifa letu walikuwa vichwa. Fikra zao zitadumu vizazi na vizazi sio Tanzania tu bali duniani kote. Kwao ilikuwa UZALENDO kwanza, mengine baadaye. Kuna mijinga michache hapa JF inajaribu kuleta hoja za kumkebehi Mwalimu kwa njia mbalimbali eti kwamba "nchi hii inaendeshwa na mawazo ya MFU" na hasa inapojitokeza hoja ihusuyo muungano.

  Tatizo kuu tulilo nalo sasa hivi limeletwa, kama asemavyo (japo ni Marehemu lakini mawazo yake yanaishi) Prof. Chachage, na mibaka uchumi na makuwadi wa kisiasa vitu ambavyo vimezalisha UFISADI wa kutisha pasi na mwenye ujasiri wa kumnyoshea mwenzake kidole kwani wote wako hivyo hivyo. Badala yake UONGO, FITNA, na PROPOGANDA ZA KIZUSHI kama UDINI, UKABILA, UKANDA vimegeuka "sera" na mahubiri ya kila uchao. Badala ya kumtazama mnyonge (kama walivyofanya wasisi wetu watukufu), wamekazania USISI na FAMILIA ZAO na MAKUWADI wao.

  Mtazame yeyote wa wavua magamba usoni, kuanzia aliye Mkubwa kabisa mpaka mdogo kuliko wote, asimamapo jukwaani usoni yuko dhahiri; kwamba kile anenacho hakimtoki moyoni; UJASIRI huo watautoa wapi?

  Udumu UZALENDO wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Udumu UZALENDO wa Mzee wetu Mpendwa Abeid Karume, Udumu UZALENDO wa Kamanda wetu na Simba wa Vita, Mzee Rashid Mfaume Kawawa; wapumzike Amani - AMINA.

  Kwao ilikuwa Tanzania na Wanyonge kwanza.
  Ndugu zangu wa vyama vya upinzani ikiwamo CHADEMA tafadhali wala msione aibu kuwaenzi wazee hawa hata kama hawakuwa katika vyama vyenu lakini fikra, mawazo, na matendo yao (yaani UZALENDO) yako juu zaidi ya chama chochote.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,421
  Trophy Points: 280
  umetumwa?
   
 6. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Wewe ndo uliyetumwa hivi kweli embu tufaamisheni imani ya CDM? WEKENI HAPA TUZIONE?
   
 7. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Ivuga big up sana hama kwa hakika nimewaona wengi humu ni CDM sasa wanaziangalia hizo imani alafu wanazipotezea. Tunaitaji viongozi wa kweli wenye kusimamia misingi hii. Sasa jamani vipi mpo tayari kuchukua njiiii. Kama mpo tayari tufahamisheni kile mnacho kiamini?
   
 8. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Chama kimeanza kujivua MAGANBA na hakika kama tukirudi kwenye misingi hii sioni haja ya kwanini hii kadi yangu niirudishe? mpaka jamaa watakapo ni shawishi vya kutosha.
   
 9. m

  menny terry Senior Member

  #9
  May 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wizi mtupu fikra hizi ni nzuri but hazitekelezeki zipo theoretically mno mbona swiden ina ubepari lakini pengo kati ya maskini na tajiri ni dogo? China yenyewe imezishindwa hizi falsafa mi nadbani mkuu ametumwa na CHAMA CHA MAGAMBA kuja kuleta propaganda zake.
   
 10. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Najua itawauma wengi humu ndani lakini ukweli ndo huu tukatae tukubali kama CCM wakirudi kwa wananchi na imani hizi. Na ambavyo imekwisha onekana basi tena tanzania tunayo ipenda inakaribia. Nawashukuru sana CDM kwa kutufumbua macho kwani wana sema usimwamshe aliye lala..... sasa tumeamka na tunakwenda kurejea imani zetu za enzi zileeeeeee. CCM hOYEEEEEE.
   
 11. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu kuwa na imani, hata kama zingekuwa nzuri kushinda pepo, bila kuziamini na kuzifuata tena kwa matendo thabiti ni heri kutokuwa nazo. Ni ubatili tena ni utupu! Nilichoeleza kwenye mchango wangu wa awali (hapo) juu ni jinsi gani Mwalimu na waasisi wenzake walivyoweza kuziishi imani hizo kwa matendo tena kwa kumaanisha tofauti na magamba ya leo ambayo yamejaa maneno mengi midomoni huku imani hizo zikiwa zimefungiwa kwenye makabati! Inasaidia nini kuwa na imani ambazo huzifuati?

  Ninachosema ni hiki: UZALENDO uko juu kuliko chochote kile iwe imani, siasa, chama, au chochote kile isipokuwa Taifa lenyewe. Heri MZALENDO wa kweli asiyekuwa na IMANI yoyote kuliko kuwa na imani ilhali ni FISADI au mkosefu wa MAADILI. Hatuwapimi watu kwa kuwa au kutokuwa na imani bali tunawapima kwa UZALENDO wao kwa Taifa. Natumaini umeelewa.
   
 12. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Nimekupata mkuu lakini nafikiri lazima kwanza kama chama muwe na kitu mnacho kiamini then inakuja kuzitekeleza. Wazee wetu walijaribu kwa viwango vyao. Chama cha CCM kikachukuliwa na mafisadi na wemetufilisi mpaka basi! sana naogopa je hawa wenzetu wana weza kuwa na imani kama hizi au nao wanataja badilika. Nafikiri unafikiri nimesema wewe Chama Cha Magamba... wala usitishike na hiyo Avatar.... Tupo pamoja kwenye kujenga njiiii.
   
 13. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  TATIZO NI MATENDO YENU SIO VITABU VYENU, maana yote yaliyopo humo yameandikwa na nyerere na yeye alikuwa na uchungu na TAIFA ili lakini leo hii,
  mkurugenzi wa wilaya bajeti yake ya chai ni Tsh 8.7/= (kinondoni) mtanzania wa kawaida mshahara wake kwa mwezi ni Tsh 135,000 kwa mwaka tsh 1.4/=
  kuna usawa gani hapo MKUU
  JK sio sawa na sisi na mawaziri wake sio sana na sisi ndio maana hata nyumba zao wanaziona takataka sasa wanaishi hotelini kwa ghalama za serikali, uliza tunalipa shilingi ngapi kwa kichwa?
   
 14. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  HAPANA! Naomba nitofautiane na wewe. La msingi ni UZALENDO KWANZA. Imani ya Chama iwepo isiwepo hiyo si lazima. Kama nilivyosema, ukiondoa Taifa, UZALENDO ni zaidi ya kila kitu: MZALENDO ana MAADILI, MZALENDO si FISADI, MZALENDO hujali WANYONGE, MZALENDO hutenda HAKI ambayo matokeo yake ni AMANI, MZALENDO si MNAFIKI, MZALENDO husema KWELI DAIMA, MZALENDO kwake TAIFA KWANZA, n.k. n.k.

  Hivi kuwa na imani kama hii "Chama kinaamini kwamba: Binadamu wote ni sawa; Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake." bila kuwa na WAZALENDO wa kubadili IMANI hiyo katika MATENDO inasaidia nini?

  Kwamba CHADEMA (au vyama vingine) wana au hawana "IMANI ya CHAMA" kwangu si jambo la msingi. Kumbuka "UZALENDO unawezekana bila IMANI" na hili ndilo la msingi.

  Hakika CCM wangekuwa WAZALENDO wa KWELI naamini hata hao CHADEMA na Taifa zima lingekuwa nyuma yao; kila mtu angekuwa CCM "kindakindaki". Lakini jamaa wanakosa jambo moja tu - UZALENDO. Kwa wavua magamba, kama mashariki ilivyo mbali mno na magharibi vivyo hivyo na UZALENDO kwa CCM ya leo!
   
 15. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unatafuta kutukanwa wewe! Wenzio hawataki uwakosoe kwa lolote lile! Shauri yako!
   
 16. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #16
  May 14, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Acha propaganda wewe mchumia tumbo!
  Mnahangaika nini mbona nyie wenyewe wana magamba mbona hizi imani hamzitekelezi?
  Nilishasema chama cha mapinduzi amechukua mwenyewe baada ya aliyeachiwa (mkapa), alipokiuka masharti kwa kumwachia mkwele chama cha baba wa taifa ambaye alikuwa hamtaki hata kwa dawa hapo ndo kosa lenu wana magamba mtatafuta mchawi hamtakaa mmpate mpaka kinaingia kaburini.
  Ccm ya sasa ni yakina Ra,EL na mafisadi wengine ndo maana watu wasio jua kama akina Nape wanakurupuka wanadhani ni chama chao kumbe yeye ni vuvuzela tu. Nape akumbuke pia kuwa hata bosi wake hana veto sana kwenye hiki chama cha wenyewe ndo maana wamemnyoshea kidole tu akafyata mkia. Hiki ni chama kingine kabisa na wenyewe wameweka hata hisa zao humo. Mimi nilikuwa naipenda sana ccm ya baba wa taifa huwa ninatokwa na hata machozi nikisikia nyimbo zake za wakati ule na hotuba ya baba wa taifa.

  Mimi naamini hiki si kile chama cha mapinduzi cha baba wa taifa, wenye akili na ambao Mungu anaweza kuwafunulia watakuwa wananielewa kama hujanielewa mwombe Mungu atakufunulia.

  Mnaweza kuniona mchawi kwa maana nawakumbusha yaliyotabiriwa na yametokea sasa. Ninasema bila kusita kuwa ccm ya baba wa taifa ndiyo CHADEMA ya leo. Kumbukeni hata baba wataifa alikipa baraka chadema baada ya kufurahishwa na sera zake.

  Kwa mtanzania yoyote mwenye hisia atakubaliana na mimi kwamba hamna namna ya kuisimamaisha CDM tena katika harakati zake za kuiongoza hii nchi.

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CDH!
   
 17. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  CDM kama chama kipya tunatarajia kitoke kivingine, pamoja na kushahihisha yale wanayodhani ni fikra mgando za chama wanachotaka kukiondoa madarakani. Swali halijajibiwa. Itikadi ya CDM ni nini wandugu? Mbona kigugumizi?
   
 18. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #18
  May 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  Ni UZALENDO kwa Taifa, watu wake, na rasilimali zake. Hata matendo yao (na sio maneno) yanadhihirisha hivyo.
   
 19. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #19
  May 14, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Umeona heee wanapiga kelele sana na maandamano je itikadi yao ni nini haswa kabla hatujajiunga lazima tukijue chama kina amini nini haswaaa!!
   
 20. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #20
  May 14, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Toa mifano kama vile kuuziana magari mabovu bila kanuni! wanaopiga kelele jukwaani leo wanamiliki Mavogue? Mshahara wa Katibu mkuu ukichanganya na marurupurupu sawa na Katibu wangu wa chama cha Magamba? jamani tusidanganyane sijaona chama mbadala zaidi ya CCM.
   
Loading...