Elections 2010 Imani ya Andrew Chenge kuhusu demokrasia ya vyama vingi inatia kichefuchefu

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Nimesoma kwa masikitiko makubwa juu ya kile ambacho Chenge anataja kuwa sababu yake ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha 2010-2015.
Chenge anasema hivi kuhusu bunge la 9 lililokuwa chini Sam Sitta... "Kilichotokea wabunge wote wa chama tawala na upinzani waliungana dhidi ya serikali... hii si sahihi," alisema Chenge. "Chama tawala kimepewa fursa ya kutoa maagizo kwa serikali... chama kilichopata ridhaa ya wananchi kupitia kura zao, lazima kipewew fursa ya kwanza ya kutekeleza programu zake bila ya kuathiri haki za wachache kutoa maoni yao."

Kwa mujibu wa Chenge chama kinakuja kwanza, na maslahi ya taifa baadaye. Uongozi wa namna hii ndio ulituletea madudu ya IPTL, EPA. Uongozi unaozuia mijadala inayolisaidia taifa kwa manufaa ya chama ni hatari sana, hatutaki kurudi kwenye enzi za kudharau hoja za msingi ambazo zinaletwa bungeni na kambi ya upinzani na kupuuzwa kwa sababu tu zimeletwa na wapinzani.
Tunaomba Chenge na mafisadi wenzake watafute namna ya kutuibia, wajue sasa tunaweza kupata habari zaidi kuliko enzi za Msekwa na Mkapa, na kama wanataka turudi huko wajue kuwa hatutakubali na wawe na uhakika kuwa wataondoka kwa nguvu ya umma.. PEOPLES' POWER!
Tunawaomba wabunge wa CCM wawe makini juu ya uteuzi wa Spika, vinginevyo sioni namna Bunge la namna anayoitaka Andrew Chenge litamaliza mhula wake bila kuwa vurugu na umwagaji wa damu.
Chonde CHONDE ndugu zangu wabunge wa CCM kuweni makini msipate dhambi ya kuangamiza maisha adimu ya watanzania
 
Sio siri baada ya kuisoma hii habari kwene gazeti la Mtanzania, Nipashe nako nikaikuta, Habari Leo nako nikaikuta.

Nilijikuta najiuliza swali moja, hivi Chenge angekuwa baba yangu ningefanya nini?

Manake hapana, Duuuuuuuuuuuuuuuuu, Vijisenti, Vijingombe.

Hebu kwanza Chenge nakuomba muache huyo Sita.
 
Back
Top Bottom