Imani tofauti katika ndoa

illuh

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2014
Posts
1,254
Reaction score
701
Kwanini pale panapotokea Wawili waliopendana Mwanamke na mwanaume ambao wanaimani tofauti (Christian & Muslim) wazazi wanakuwa wanaingilia katika suala la kupinga wawili hawa kuwa kitu kimoja?

Je hawaoni kuwa hii inapelekea mwanao kuja kumpenda asiye mpenda sababu aliyekuwa amempenda ni yule wa imani tofauti nae?

Je hawaoni kuwa wanalazimisha uzinifu?

Wazazi, Je nivibaya wawili hawa wakawa kila mmoja anaabudu dini yake ikiwa tunajua kuwa Muumba ni mmoja na makatazo yote yaliyokatazwa katika Biblia na Quran ni sawa?

Je Dini ndio inampeleka mtu pema au matendo?

Sielewi kwanini hasa wazazi huwa wanakuwa wakali sana inapofikia katika suala hili !!!
Kwa mimi mawazo yangu naona haina shida kwani hata ikifikia katika upande wa watoto nao watachagua wapi wanataka waabudu ....

Naombeni mawazo yenu nanyi wanajamii kwani tuko kwaajili ya kuelimishana...Mnachukuliaje suala hili wewe kama mzazi, kijana
 
This issue is so confusing,esp pale unapoona hata wa dini moja wanasumbuana kwenye ndoa...napo kuoana dini tofauti sijui watoto mtawafundisha waelekee upande upi enewei...muda wa ndoa ukifika ntajua
 
Dini ni chaguo la mtu binafsi haswa akishafikia balekhe,huwezi kumuamulia imani ya mtu mwengine…wazazi hawahusiki…ila ni mila na desturi zetu tu kwamba wazazi na familia ni part ya maisha yetu
 
inachanganya sana, hasa ikitokea wa dini yako hakuna anaeeleweka walau ujilazimishe na huyu umpendae kwa dhati waogopa hata kulitaja jina lake mbele ya familia.
It hurts tena sanaaaaaa
 
HIYO INAWASUMBUA NINYI WAISLAMU NA WAKRISTO,KWA SISI HATUNA NOMA,PEACE AND LOVE.:mvutaji:
 
Kama wazazi wagumu kuelewa, mtu unajua ukimwambia hatokubali, munafunga ndoa ya serikali bila kuwafahamisha. Mke na mume munakua chama kimoja, wengi ukimbilia mkoa mwingine mbali na kwa wazazi wao, wakiona mumeishi miaka 10 na kuzaa mumezaa, wanagive up.
 
mmmmmh sisemi inauma sana pale unaposhindwa kuoana kutokana na utofauti wa dini afu ukute mnapendana
 
Imani ni kitu kingine kabisa na vijana wengi wa siku hizi hatufuatilii mambo ya dini ndiyo maana tunayaona hayana msingi na kurahisisha kuwa Mungu ni yule yule yanayokatazwa na dini zote ni yale yale sijui kama hii iko sawa,mnapokuwa sini tofauti hata watoto wanashindwa kujua wasimame wapi kwa mama au kwa baba na mara nyingi watakimbilia kwa mama kwa sababu ndiyo yuko karibu sana,watoto watakuwa hawana msimamo kiimani hivyo suala la wao kusali linaweza kuwa ndoto wakikua,lakini pia misimamo tofauti ya dini zetu,kwa ushauri wangu kwakuwa hili linaonekana ni tatizo na linaletwa na sisi watoto wenyewe kwa sababu upendo hauji kama mvua unatengenezwa mpaka unakomaa,kama unajua wazazi wako hawawezi kukubali wewe kuwa na mtu wa dini nyingine kwanini uingie kwenye huo uhusiano? si kweli kwamba utakosa mtu wa dini yako utakaye mpenda,kuna watu walisema siwezi kuishi bila wewe na mmeachana lakini bado wanaishi bila wewe kwa hiyo upendo hutengenezwa ndo maana huanza taratibu na baadaye hukomaa ni ile hali ya kupuuzia misimamo ya wazazi ndiyo inatuletea shida katika mahusiano.
 
Dini ni swala zito sana. Ukiona mtu anakuwa tayari kubadili dini kwa ajili ya mtu basi ujue yuko shalo kwenye imani. Mtu anayejua anachokiabudu kwa roho na kweli wala hahitaji wazazi kuingilia kati. Mungu wetu si mmoja na kama ni mmoja hatumuoni sawasawa, tunamtafsiri tofauti. Hata watu wa dini moja kama viwango vyao vya imani ni tofauti wanapata migongano (mfano, mlutheri jina na mlutheri mlokole) ingawa migongano yao haiwezi kuwa mikubwa kama baina ya wenzi wa dini mbili tofauti. Kama mna hakika mnapendana mapenzi ambayo yatabaki kuwa mahaba milele basi oaneni tu, lakini kama ni mapenzi haya haya tunayoyajua basi kabla hamjafunga ndoa mkubaliane kabisaa hapo kwenye dini itakuwaje, ikiwa ni pamoja na kukubaliana watoto watalelewa kwa misingi ya dini ipi toka wakiwa wadogo. Haiwezekani kulea watoto kihayawani halafu eti wakiwa wakubwa ndo wachague. Hapa ni lazima mzazi mmoja akubali kujishusha, na sijui ni nani atakayeweza kuthubutu kuona mwanae anaabudu kitu ambacho yeye hakiamini, labda awe shalo kama nilivyosema awali. Mkiwa shalo hata mhindu na mkatoliki mjaluo mnaoana tu maana hamna mizizi, ukija upepo kama wa mapenzi unawazoa tu.

Mchumba akikataliwa na wazazi na wazazi wakisisitiza hawamtaki hata baada ya kutumiwa ujumbe wa marais wastaafu aisee using'ang'anie. Hawa watu kuna wakati tunawaona wamepitwa na wakati, hawajui raha na karaha za kupenda lakini amini tu kwamba ukiwakaidi unaweza usifanikiwe kwenye hiyo ndoa. Kuna kitu wamekiona na wanajaribu kukulinda. Vitu vidogodogo kama makabila na sura na mali baada ya muda wakishawishiwa wengi hubadilika, ukiona hawabadiliki kuwa mpole. Kuna familia zina imani na maagano yao flani, ukipeleka mchumba lazma wacheki compatibility. Uking'ang'ania usishangae mmoja wenu akafa mapema, au watoto wenu kufa au kutowapata kabisa au kukosa amani kwenye ndoa kwa sababu mbalimbali. Nimeyaona haya majanga kwa ndugu/jamaa/marafiki zangu waliolazimisha kama wanne hivi. Bado naendelea na utafiti wangu juu ya hili jambo maana ni vigumu kulithibitisha kisayansi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…