Tafuta Quraan umsome Allah utapata jibu
Haya tunayo kusomea ni katika Aya na ukumbusho wenye hikima. Qur'an 3:58
Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi mungu ni kama mfano wa Adamu; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: kuwa! Basi akawa
Qur'an 3:59
Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako mlezi. Basi usiwe miongoni wanaofanya shaka. 3:60
Watakao kuhoji katika haya baada kukufikilia ilimu hii waambie: njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wake zetu na wake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe,kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi mungu iwashukie waongo. 3:61
Hakika haya ndiyo maelezo ya kweli. Na hakuna Mungu ila Mwenyezi mungu tu, na hakika Mwenyezi mungu ndiye mwenye nguvu na mwenye hikima. 3:62
Na kama wakigeuka basi Mwenyezi mungu anawajua waharibifu
3:63
Sema: Enyi watu wa kitabu! Njooni kwenye neno lillilo sawa baina yetu na nyinyi: ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola walezi badala ya Mwenyezi mungu. Na wakigeuka basi semeni: shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu. 3:64
Enyi watu wa kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati Injili hazikuteremshwa ila baada yake? Basi hamzingatii?
3:65
Angalieni! Nyinyi mlibishana katika yale mliyo yajua. Mbona sasa mnabishana katika yale msiyo yajua? Na Mwenyezi mungu ndiye ajuaye,na nyinyi hamjui.3:66
Ibrahimu hakuwa Yahudi wala Mkristo,lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.3:67
Watu wanao mkaribia zaidi Ibrahim ni wale walio mfuata yeye na Nabii huyu na walio amini. Na Mwenyezi mungu ndiye mlinzi wa waumini.3:68
Wala msimuamini ila anaye fuata dini yenu. Sema: hakika uwongofu ni uwongofu wa Mwenyezi mungu,kuwa apewe mtu mfano wa mlio pewa nyinyi au wakuhojini mbele ya Mola wenu mlezi. Sema hakika fadhila zimo mikononi mwa Mwenyezimungu. Humpa amtakaye. Na Mwenyezi mungu ni mwenye wasaa na mjuzi. 3:73
Na miongoni mwa watu wa kitabu yupo ambae ukimpa amana ya mrundi wa mali atakurudishia, na miongoni mwao yupo ambae ukimpa amana ya dinari moja hakurudishii isipo kuwa ukimsimamia kumdai. Haya ni kwa kuwa wakisema: Hatuna lawama kwa ajili ya hawa wasio jua kusoma. Na wanamzulia uwongo Mwenyezi mungu,hali nao wanajua.3:75