Imagine Membe angekuwa Rais toka 2015?

Imagine Membe angekuwa Rais toka 2015?

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,262
Reaction score
18,706
Kuna mambo ambayo wanadamu tumefichwa. Pamoja na utawala huu kulalamikiwa hasa juu ya haki za binadamu na maslahi kwa wafanyakazi, lakini Tanzania ya membe ingekua ya ajabu zaidi.

Tofauti ya Membe na Magufuli ni kwamba mmoja anaamini Tanzania ya mendeleo bila wazungu na mmoja ana amini bila wazungu hakuna maendeleo.

Hivyo kwa utaratibu huu Tanzania ya Membe ingekua ya ni Tanzania ya wageni na wakuu kula bata.

Mtwara ingekuwa muda huunimejaa wazungu, Bagamoyo ingekua imeshika kasi huku bandari za dar, mtwara, na tanga zikiwa hoi.

Reli ingekuwa imeshikwa na wachina kama wenzetu Kenya japo naamini ingekua imesha isha muda huu.

Miuundo mbinu kama afya, barabara, shule , bandari, meli kwenye maziwa makuu hali ingekua mbaya sana.

Tanzania ingekua ni nchi moja wapo inayo hudhuria vikao karibia vyote vya UN na taasisi nyingine.

Kwa ugonjwa wa corona hadi muda huu tungekua tumefungiwa home, na shule na vyuo zingeambiwa hadi 2021.


FB_IMG_1595167837868.jpeg
 
Imagine Magufuli ndiye alikuwa best option iliyobaki kwa CCM. Kipindi anachaguliwa kupeperusha bendera ya chama chake hakuna aliyekuwa na shaka nae kuliko wale wengine. Hii ndo offer pekee ambayo CCM waliitoa ikaonekana kidogo inauzika mbele ya wananchi.

Waliobaki kina Lowassa, Membe na wengine walionekana kama watakuwa mwendo uleule wa CCM. Kwanza Lowassa asingetoka CCM angekuwa anaitwa fisadi hadi leo.

Sidhani kama Lowassa au Membe kupitia CCM wangefanya lolote la ziada. Wale wamezoea mfumo uliowalea na wangeendelea vilevile bila mabadiliko makubwa. Huyo Lowassa kupitia UKAWA sijui angefanya nini zaidi ingawa angepewa support kubwa mwanzoni.

Magufuli sio the best lakini wala sio mbaya sana kama tunavyodhani. Sioni mtu yeyote wa kuleta maajabu hapa nchini. Kila mgombea ninayemuona naamini ana uwezo wa kawaida tu.

Kupata mtu wa kufumua kila kitu na kukiweka sawa kwa nchi inachukua miaka mingi sana. Mtu kama Mustafa Kemal Atatürk wa Turkey miaka hiyo, ni nadra na hajirudii.
 
twiga wasingekuwepo hata mmoja.
wapigaji wangeongezeka maradufu.
tatizo la kukatika kwa umeme lingeongezeka badala ya kupungua.
madon wa ngada wangejiachia na kujimwambafai zaidi.
kuna wale jamaa wa mtaani anakwambia nakupiga kisha nakufunga, wangefanya kufuru zaidi.
 
Nchi ingekua ya hohyo sana japo kuna watu wangelula bata balaaa.
twiga wasingekuwepo hata mmoja.
wapigaji wangeongezeka maradufu.
tatizo la kukatika kwa umeme lingeongezeka badala ya kupungua.
madon wa ngada wangejiachia na kujimwambafai zaidi.
kuna wale jamaa wa mtaani anakwambia nakupiga kisha nakufunga, wangefanya kufuru zaidi.
 
Kwani MAGUFULI NA KIKWETE NANI ALILETA UNAFUU WA MAISHA KWA WATANZANIA? UWEZO WA WÀNANCHI KUJENGA, KUMILIKI MAGARI, MASHAMBA NK.

Kwangu mimi maisha yangekuwa nafuu sana. Mishahara juu, miundombinu ya barabara na bandari ingekuwa safi, uhuru wa bunge na mahakama ungekuwa juu.

Ajira zingetolewa kama haki ya raia sio hisani ya rais kama afanyavyo kwa vijana wa JKT. Tusingepata Spika wa hovyo wala wakuu wa mikoa wa hovyo kama MAKONDA.

Lkn tusingekuwa na Ndege zile, reli ya kati ingekuwa hoi. Pia asingetembea na mabegi ya pesa kugawa hovyo makanisani na njiani, Mabeyo asingekuwa CDF wala SIRRO kuwa IGP, isingetokea mtu kufukuzwa kazi hadharani nk.
 
Naona tayari mmeanza kumruka kimanga "Jasusi Mbobezi" baada ya kutimkia ACT na kujiridhisha hakuna tena muungano.
 
Jasusi Mbobezi angekuwa rais,
nchi ingekuwa mbali hii
Ben Saanane, Azory Gwanda na Kanguye huenda tungekuwa nao mtaani

Na huu ukatili wa kuweka weka wapinzani ndani, kufungia fungia magazeti na kuchezeachezea uchaguzi wa serikali za mitaa, kuvuruga zao la korosho, kufanya biashara ya kununua watumwa na malaya wa kisiasa visingekuwepo
 
Back
Top Bottom