MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Moja ya changamano kubwa inayoikabili serikali ya Rais Magufuli ni kuweka mizani sawa/urari kwa wananchi katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Ikumbukwe kuwa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii huwa yanasadifu mabadiliko ya kisiasa.
Tatizo linaloikabili serikali ya Rais Magufuli ni sawa kwa karibu na lile lililoikabili serikali ya chama cha Conservative chini ya Waziri Mkuu, David Cameron nchini Uingereza baada ya kuingia madarakani mwezi wa May 2010.
Serikali ya Cameron baada ya kuchaguliwa ilikuta matumizi ya serikali yalikuwa ni makubwa naya hovyo ukilinganisha na mapato, wakati huo huo serikali ya Labour ikiwa imeacha deni kubwa la kiasi cha £1.2 Trillion. Kwa kutumia takwimu za kisiasa ambazo hazina msingi kiuchumi, kila mwingereza alikuwa anadaiwa kiasi cha paundi 18,600 kupitia deni la taifa.
Serikali ya Rais Magufuli imekuta matumizi ya serikali yalikuwa ni makubwa na mengi ya hovyo hovyo huku serikali ikiwa ameacha deni kubwa la kiasi cha trilioni 43 huku uhimilivu wa deni ukiwa asilimia 19 ya pato la taifa. Kwa kutumia takwimu za kisiasa, kila Mtanzania alikuwa anadaiwa zaidi ya shilingi 900,000 kupitia deni la Taifa.
Serikali mpya ya Cameron ikaja na sera ya kubana matumizi ya serikali ili kukabiliana na changamoto za kukua kwa deni la Taifa na kupunguza uwiano wa nakisi ya Bajeti na Pato la Taifa.
Ikumbukwe kuwa ni wanasiasa wachache sana wanaofanya maamuzi ya kiuchumi yanayoitwa contractionary fiscal policy badala ya expansionary fiscal policy. Wanasiasa wa aina hii wanaitwa statesman kwa sababu hawafikirii uchaguzi bali wanafikiria nchi endelevu kwa kizazi kijacho.
Kama ilivyokuwa kwa serikali ya Cameroon, Serikali ya Rais Magufuli imekuja na sera ya kubana matumizi ya serikali na pesa zilizobaki kwa kiwango kikubwa kupelekwa kwenye maendeleo ili kukabiliana na changamoto za kukua kwa deni la taifa na kupunguza nakshi ya bajeti na kuwekeza kwenye miundo mbinu.
Sera ya kubana matumizi ya serikali ya Camerron iliongeza matatizo zaidi kwa wananchi kwa sababu kipindi hicho UK ilikuwa kwenye mdororo wa uchumi (Economic recession). Ukata ulipelekea kwa kiasi kikubwa machafuko nchini Uingereza kwa zaidi ya wiki moja ambapo maduka sehemu mbali mbali yalichomwa moto huku mengine yakivunjwa na bidhaa kuchukuliwa/ kuibwa kwa nguvu.
Sera ya serikali ya Rais Magufuli ya kubana matumizi ya serikali na kupambana na ufisadi imeanza kuleta matatizo kwenye uchumi wa mtu mmoja mmoja kwa sababu pesa nyingi za kifisadi zinaondoka kwenye mzunguko wakati huo huo hakuna pesa safi zingine ambazo zinaingia kwa haraka kwenye mzunguko wa uchumi ili kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja kutokana na sera ya contractionary fiscal.
Hali hii ikiendelea kwa muda mrefu tunaweza tukajikuta yaliyotokea Uingereza yanatokea nchini na kama hayatatokea basi matukio ya utapeli, ujangili na wizi yataongezeka sana nchini.
Machafuko nchini Uingereza yalipelekea Serikali kuunda kamati ya uchunguzi na kugundua moja ya chanzo cha machafuko ni msuguano wa kijamii kati ya wenye nacho na wasio nacho ( inequalities) huku kichocheo kikiwa ni sera ya kubana matumizi katika kipindi cha mdororo wa uchumi (economic recession) ambayo imeumiza masikini wengi wanaotegemea government benefits.
Matokeo ya Kamati Maalum ya uchunguzi yalipelekea serikali ya umoja iliyokuwa inaongozwa na chama cha Conservative kwenda kukopa £91.5bn ili kukabiliana ukata unaosababisha kukosekana kwa kiwango kikubwa cha usawa kiuchumi na kijamii.
Pesa hizi zilitumika kuanzisha benki iliyoitwa British Business Bank kwa ajiri ya kukopesha wafanyabiashara wadogo wadogo katika mlengo wa kuamsha uchumi na mzunguko wa pesa. Serikali pia ilianzisha miradi mikubwa ya miundombinu yenye thamani ya pound bilioni 100. Mkakati huo wa serikali ya David Cameron uliwezesha kuchochea uchumi na kuzalisha ajira.
Ikumbukwe kwa uchumi wetu, Serikali ndiyo mlaji mkubwa wa bidhaa na huduma mbali mbali. Serikali inapotumia inalipa wazalishaji wa bidhaa na huduma mbali mbali ambao nao hulipa wafanyakazi wake ambapo wafanyakazi hao huenda kuzitumia mitaani na hatimaye pesa huingia kwenye mzunguko wa fedha. Matumizi haya ya serikali ni muhimu sana katika kuchochea shughuli za kiuchumi na kibiashara.
Tatizo la uchumi wetu tuliingia kwenye soko huria kwa zaidi ya 24 lakini bado serikali ni mlaji mkubwa wa bidhaa na huduma wakati sera za soko huria zinataka sekta binafsi ndiyo iwe mlaji mkubwa wa bidhaa na huduma. Hali inaongeza zaidi tatizo ukilinganisha na tatizo lililokuwepo nchini Uingereza ambapo sekta binafsi ni mlaji mkubwa wa bidhaa na huduma mbali mbali.
Tuna taifa lenye uchumi ambalo serikali ikipata mafua ya kiuchumi basi nchi nzima pia inaugua. Serikali ikiwa fujaji basi na wananchi wanakuwa fujaji. Serikali ikiwa legelege na wananchi wanakuwa legelege.
Serikali kuamua kubana matumizi kunawalazimisha hata wananchi kubana matumizi kutokana na muundo wa uchumi wetu.
Tatizo linaloikabili kwa sasa serikali ya Rais Magufuli katika kipindi hiki cha mpito ni namna ya kupata mizani sawa/urari kati ya mapato na matumizi ya serikali ambayo pia yatachochea shughuli za kiuchumi na wakati huo huo kukuza uchumi kwa sababu mazingira ya kiuchumi yaliyopita yalijenga Tanzania ambayo uchumi halisi wa wananchi wake ulikuwa haufahamiki na matokeo yake kukawepo tabaka kubwa la wenye mali ambao hawapo katika vitabu vya serikali huku wasio na mali wakiongezeka kwa kasi kwa sababu serikali ilikuwa haitoa huduma za kuwasaidia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Je, serikali ifanye nini ?
Serikali inatakiwa ipeleke pesa kwa wananchi ili kuamsha matumizi na mzunguko wa pesa. Kuna njia nyingi za kupeleka pesa kwa wananchi lakini nitataja tatu katika mazingira ya Tanzania.
1) Serikali kukopa pesa kwenye mabenki au jumuiya za Kimataifa.
2) kukopesha sekta binafsi na vikundi vya uzalishaji.
3) Serikali kunzisha miradi mikubwa yenye kuajiri watanzania wengi.
Kuhusu namba 1, tumeona na kusikia juzi Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akieleza jinsi ambavyo serikali ina mpango wa kukopa kutoka jumuiya ya kimataifa.
Namba 2 inawezekana kwa kupitia kwenye Ilani ya Uchaguzi kuhusu milioni 50 kwa kila Mtaa na Kijiji. Hii italeta tija kubwa kwa sababu walengwa watakuwa Watanzania hapa nchini ambao akaunti zao zipo kwenye mabenki nchini.
Serikali vile vile ilipe madeni ya ndani kwa wazabuni wadogo wadodo ambapo pesa hizo zitazidisha mzunguko wa pesa kwa jamii.
Kuhusu namba 3, Uanzishaji wa miradi mikubwa ambayo itaajiri watanzania wengi unakabiliwa na mapungufu/mapengo kwenye sekta nyingi. Miradi mikubwa kama ya ujenzi wa barabara na reli ingepaswa kuchochea uchumi iwapo tu magari/magreda/vijiko/vishindiliaji/matairi n.k. yanayofanya kazi yangekuwa yanatengenezwa hapa hapa nchini, hivyo fedha hiyo ya ujenzi inatoa mwanya wa kiwanda cha magari/magreda/vijiko/vishindiliaji/matairi n.k. kuzalisha zaidi na kuajiri zaidi, na hivyo kustawisha na sekta nyingine. Kwa sasa niaamini makampuni makubwa yatakayopata tenda yatakuwa ya kigeni ambayo akaunti zake ziko nje ya nchi, mbaya zaidi hata vifaa vyote vya ujenzi vitatoka nje. Hata vyakula vya wafanyakazi vitatoka China, South Africa na Kenya.
Nina wasiwasi na solution ya tatu kama italeta tija sana katika kuamusha uchumi kwenye matumizi.
La mwisho, tunapaswa kuwepo na juhudi za dhati za kutengeneza muingiliano katika sekta zetu za uzalishaji (Inter-sectoral linkages) ili kulahisisha mzunguko wa pesa nchini. Kundi kubwa la watanzania ambao hawana akaunti katika mabenki linasababisha muingiliano katika sekta zetu za uzalishaji kuwa mgumu.