Ilivyo ngumu kumlinda mateka!

nnachoshangaa siku nne kupita ndo wanatangaza dau nene hivo ni kwamba watekaji wasalitiane au?
maana kwa utekaji si sawa na kupotea!
Walikuwa wanasikilizia kwanza... Kama nia ilikuwa kudai kikomboleo basi hilo lingefanyika ndani ya saa 72 tangu tukio.... Sasa familia ikiona kimya inaamua kuchokoza mada
 
.
IMG-20181020-WA0060.jpeg
 
as I was reading, kuna mambo flani nilikua nayafikiria nikajikuta napata maswali ya kjinga. hivi thread kama hii si jamaa waisome wajue mambo yanavyofanywaga?😂😂
 
niruhusu nijibu hapa hapa
Zipo njia nyingi za kupata kikomboleo salama....lakini vilevile watekaji huwa na mtandao mkubwa ukiwajumuisha watu muhimu ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama ambao sio waaminifu
.Kikomboleo daima hulipwa kwa fedha tasilimu...kutumia miamala kama bank nk kunahitaji maandalizi makubwa na ya gharama.
.Kikomboleo huelekezwa kikawekwe mahali ambako visibility iko vizuri kuepuka kufuatiliwa ama kuwekewa mtego
.Mara nyingi mpeleka kikomboleo hufuatiliwa kwa karibu na watekaji bila kujijua
. Mtekwaji huwa haachiwi mpaka kikomboleo kipokelewe salama
.Mara nyingi kikomboleo hulipwa eneo tofauti kabisa na alipo mtekwaji. Mfano mtu yuko Dar kikomboleo kinalipwa Mwanza ama nje ya nchi kutegemea na ukubwa wa mtandao
.Mara nyingi watekaji hutumia simu za satellite ama zisizosoma location...simu maarufu ni thuraya
.Mara nyingi watekaji hutega vifaa vya mawasiliano sehemu zote muhimu kama nyumbani au ofisini kwa mtekwaji, baadhi ya vyombo vya usalama, makazi na vyombo vya usafiri vya ndugu na wafanyakazi muhimu...vifaa hivyo ni kama camera za siri, video na voice notes devices...
.Walipa kikomboleo wakizingua tu...wanakuwa wameshaonywa Kabla ,pesa inaweza kuchukuliwa na wakamkosa ndugu yao....
. kwa baadhi ya watekaji katili kadiri kimomboleo kinavyozidi kuchelewa kutolewa ndivyo subira huwaisha watekaji na kuanza kumtesa mateka na kutumiwa video zake..
. Watekaji hujificha kwenye mwamvuli wa biashara halali
Mshana Jr Duuhhhh Upo vizuri Mkuuu...vipi ile stor za wachina hapa daresalama na biashara yao haramu uliikatisha ghafla kwa nini Mkuuuu???
 
Ni rahisi sana kulinda mzigo ama mfu wakati mkifanya michakato mingine ili kuweka mambo sawa! Ni ngumu mno kulinda mtu aliye hai hasa akiwa mateka ama mfungwa....kwa muktadha wa mada hii tutayaacha makundi yote na kujadili kundi la mateka tu....
Turejee simulizi ya Dr. Shika Urusi na jinsi alivyoweza kutoroka!
Mipango yote ya kufanikisha utekaji na hatimaye zoezi kukamilika ...huja kipengele kigumu mno...kumlinda mateka....ni ngumu kwakuwa unamshikilia hivyo kuna siku utakuja kumwachia banda ya muafaka kufikiwa na pande zote mbili (mteka na mtekwaji)
Ni hatari kukaa na mateka muda mrefu kwakuwa pamoja na ulinzi wa kila aina lakini utahitaji watu halisi wa kupokezana zamu ...na kwa jinsi unavyokaa naye kwa muda mrefu ndio jinsi anvyojifunza jambo jipya kila uchao na kila uchwao...hivyo ni lazima mission iwe ya muda mfupi zaidi na ajue machache kadiri iwezekanavyo kuhusu wewe kwakuwa kuna siku atakuwa raia huru .......
Mateka wa namna hii hutekwa kwa ajili ya kulazimishwa kufanya jambo fulani....hasa kulipa fidia (ransom/kikomboleo)....mara nyingi baada ya kufanikiwa utekaji mtekaji hutoa taarifa kwa familia yake ndani ya masaa 72....hapa wasiwasi na sintofahamu kwenye jamii pamoja na mamlaka husika vikiwemo vyombo vya ulinzi hupungua kwakuwa lengo la utekaji linakuwa tayari limeshajulikana
Watekaji ni watu wenye IQ ya juu mno na huchora mchoro wao mapema na kuufanyia mazoezi said ya mara tatu ili kutathmini ufanisi na kuepuka makosa yatakayopelekea mission kufeli....hawa jamaa hutumia muda wa kutosha na kudodosa mpaka vitu visivyofikirika kama hali ya hewa, tairi za gari, mavazi muda wingi na uchache watatu, majengo ya jirani shughuli zinazoendelea nk

Mfumo wa ulinzi wa eneo watakalofanyia kazi pia ni muhimu sana kwao,aina ya ulinzi ,nguvukazi , ufanisi wa kupeleka habari kwenye vyombo vya ulinzi baada ya tukio ,barabara za kupita, shortcut,traffik lights nk
Chukulia mfano wa CCTV camera ,huu mfumo huweza kuchanganywa database yake kwa remote tu ,tena toka mbali ama cameras kugeuziwa kwingine ....wanachohitaji kujua ni aina tu ya mfumo wa camera na mashine yake....
Kuacha alama moja ndogo ni kosa kubwa ambalo linaweza kumgharimu mhusika maisha yake..hivyo mission hurudiwa mara nyingi (rehearsal)

Kwenye mfumo wa utekaji ni lazima kuwe na makundi haya
1. Boss mkubwa (mfadhili)
2. Mkuu wa operation(kutoa amri zote na maelekezo yote muhimu)
3.wasoma ramani (utaalam wa kutengeneza mchoro wa kazi)
4. Wabeba silaha(hawapapasi macho wakiambiwa piga wanapiga)
5. madereva (hawajui kifo ninini, wajuzi wa barabara na mwendokazi ,akishakutangulia sahau)
6. Walinzi , watesaji wapishi na wahudumu wengine (hawa huishi nyumba alimo mateka)
Makundi yote haya yamefunzwa nidhamu, ukimya kasi na usiri..pamoja na uwezo wa kuhimili mateso
Yote kwa yote kuna makosa yasiyoepukika (fatal errors )...mwandishi aliyeuawa ndani ya ubalozi wa Saudia, kumbe SAA aliyokuwa kavaa ilikuwa na link na simu yake aliyoiacha nje na mpenzi wake..wakati anaingia kwenye jengo husika aliminya kitufe cha kurekodi na akajirekodi mauaji yake mwanzo mwisho ....kosa kama hili ni nani angejua?
Mateka hatakiwi kukaa matekani muda mrefu
Mateka kama ni wa kuachiwa hatakiwi kuteswa ...kwa jinsi unavyokaa naye muda mrefu ndio risk za kutoroka ,usaliti na hata kukamatwa zinavyozidi kuwa kubwa...

Mateka wa kulipa kikomboleo kwa mukatadha wa mada hii wakikubaliana na watekaji wao hulipa na kuachiwa salama salimini.....mateka wengine kwa ajili ya ishu za kibiashara , mitandao ya pesa haramu, biashara haramu , mahusiano na makundi ya kigaidi na kimafia....watamfanya mateka atoe pesa wanazotaka ama nyaraka fulani ikiwemo mikataba nk na mwishowe kuishia pipa la tindikali.........Ama kubanikwa mpaka uive, uungue mpaka ubaki jivu
Mkuu intake ya wanafunzi wapya itakuwa lini tuje utujuze mambo ya usalama wa familia na wapendwa wetu?Kwenye haya mambo wewe Mshana uko vizuri,ulienda kule nanii kule..........au umejifunza kutoka kwenye movies za investigation na crime scene?Tusaidie basi ikitokea umetekwa waweza fanya nini kujikomboa au kusaidia upatikanaji wako?Yule alidondosha funguo za gari lakini yamkini waliokuwepo hawakuelewa au the other way round.
 
N
Ni rahisi sana kulinda mzigo ama mfu wakati mkifanya michakato mingine ili kuweka mambo sawa! Ni ngumu mno kulinda mtu aliye hai hasa akiwa mateka ama mfungwa....kwa muktadha wa mada hii tutayaacha makundi yote na kujadili kundi la mateka tu....
Turejee simulizi ya Dr. Shika Urusi na jinsi alivyoweza kutoroka!
Mipango yote ya kufanikisha utekaji na hatimaye zoezi kukamilika ...huja kipengele kigumu mno...kumlinda mateka....ni ngumu kwakuwa unamshikilia hivyo kuna siku utakuja kumwachia banda ya muafaka kufikiwa na pande zote mbili (mteka na mtekwaji)
Ni hatari kukaa na mateka muda mrefu kwakuwa pamoja na ulinzi wa kila aina lakini utahitaji watu halisi wa kupokezana zamu ...na kwa jinsi unavyokaa naye kwa muda mrefu ndio jinsi anvyojifunza jambo jipya kila uchao na kila uchwao...hivyo ni lazima mission iwe ya muda mfupi zaidi na ajue machache kadiri iwezekanavyo kuhusu wewe kwakuwa kuna siku atakuwa raia huru .......
Mateka wa namna hii hutekwa kwa ajili ya kulazimishwa kufanya jambo fulani....hasa kulipa fidia (ransom/kikomboleo)....mara nyingi baada ya kufanikiwa utekaji mtekaji hutoa taarifa kwa familia yake ndani ya masaa 72....hapa wasiwasi na sintofahamu kwenye jamii pamoja na mamlaka husika vikiwemo vyombo vya ulinzi hupungua kwakuwa lengo la utekaji linakuwa tayari limeshajulikana
Watekaji ni watu wenye IQ ya juu mno na huchora mchoro wao mapema na kuufanyia mazoezi said ya mara tatu ili kutathmini ufanisi na kuepuka makosa yatakayopelekea mission kufeli....hawa jamaa hutumia muda wa kutosha na kudodosa mpaka vitu visivyofikirika kama hali ya hewa, tairi za gari, mavazi muda wingi na uchache watatu, majengo ya jirani shughuli zinazoendelea nk

Mfumo wa ulinzi wa eneo watakalofanyia kazi pia ni muhimu sana kwao,aina ya ulinzi ,nguvukazi , ufanisi wa kupeleka habari kwenye vyombo vya ulinzi baada ya tukio ,barabara za kupita, shortcut,traffik lights nk
Chukulia mfano wa CCTV camera ,huu mfumo huweza kuchanganywa database yake kwa remote tu ,tena toka mbali ama cameras kugeuziwa kwingine ....wanachohitaji kujua ni aina tu ya mfumo wa camera na mashine yake....
Kuacha alama moja ndogo ni kosa kubwa ambalo linaweza kumgharimu mhusika maisha yake..hivyo mission hurudiwa mara nyingi (rehearsal)

Kwenye mfumo wa utekaji ni lazima kuwe na makundi haya
1. Boss mkubwa (mfadhili)
2. Mkuu wa operation(kutoa amri zote na maelekezo yote muhimu)
3.wasoma ramani (utaalam wa kutengeneza mchoro wa kazi)
4. Wabeba silaha(hawapapasi macho wakiambiwa piga wanapiga)
5. madereva (hawajui kifo ninini, wajuzi wa barabara na mwendokazi ,akishakutangulia sahau)
6. Walinzi , watesaji wapishi na wahudumu wengine (hawa huishi nyumba alimo mateka)
Makundi yote haya yamefunzwa nidhamu, ukimya kasi na usiri..pamoja na uwezo wa kuhimili mateso
Yote kwa yote kuna makosa yasiyoepukika (fatal errors )...mwandishi aliyeuawa ndani ya ubalozi wa Saudia, kumbe SAA aliyokuwa kavaa ilikuwa na link na simu yake aliyoiacha nje na mpenzi wake..wakati anaingia kwenye jengo husika aliminya kitufe cha kurekodi na akajirekodi mauaji yake mwanzo mwisho ....kosa kama hili ni nani angejua?
Mateka hatakiwi kukaa matekani muda mrefu
Mateka kama ni wa kuachiwa hatakiwi kuteswa ...kwa jinsi unavyokaa naye muda mrefu ndio risk za kutoroka ,usaliti na hata kukamatwa zinavyozidi kuwa kubwa...

Mateka wa kulipa kikomboleo kwa mukatadha wa mada hii wakikubaliana na watekaji wao hulipa na kuachiwa salama salimini.....mateka wengine kwa ajili ya ishu za kibiashara , mitandao ya pesa haramu, biashara haramu , mahusiano na makundi ya kigaidi na kimafia....watamfanya mateka atoe pesa wanazotaka ama nyaraka fulani ikiwemo mikataba nk na mwishowe kuishia pipa la tindikali.........Ama kubanikwa mpaka uive, uungue mpaka ubaki jivu
Niliusoma huu Uzi kikore !! Inauma sana
 
Back
Top Bottom