Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,285
- 33,881
Mzee hii historia yako ina ukweli kiasi gani na inaweza kuthibitishwaje??Abuu,
Wazee wetu waliona balaa lililoikumba India kwa kuingia katika kudai uhuru vyama vyao viwili Congress Party kikiwa chama cha Wahindu na Islamic League kikiwa chama cha Waislam.
Kila chama kinamtazama mwengine kama adui mkubwa.
Usiku 1947 wanashusha bendera ya Muingereza wanapandisha bendera ya India huru asubuhi vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaanza.
Vikamalizika kwa kugawana ardhi kila mtu na kwao.
Ilikuwa Abdulwahid Sykes achukue uongozi wa TAA kama President 1953 na 1954 waunde TANU na wadai uhuru.
Hamza Mwapachu akamwambia Abdul chama cha TANU kitakuwa kama Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) kwani Waislam tumejazana katika siasa Wakristo wako pembeni.
Njia ya kuwavuta Wakristo watuunge mkono ni Julius Nyerere atiwe kwenye uongozi wa juu wa TAA 1953 na 1954 TANU inaundwa na Nyerere anaongoza harakati za kudai uhuru.
Wakristo wataingia TANU kwani hawataiona TANU kama chama cha Waislam.
Kinyume cha hivi Waingereza watawaambia Wakristo waunde chama chao kupambana na TANU chama cha Waislam.
Tanganyika ingeingia kudai uhuru ikiwa na vyama viwili hasimu vilivyojikita kwenye dini.
Bahati mbaya mno Nyerere akiogopa sana kueleza ukweli vipi juu ya ugeni wake Abdul Sykes alimshika mkono hadi kuwa kiongozi wa TAA 1953 na TANU 1954 na 1955 akazungumza UNO.
Leo Tanzania hali ndiyo hii ingekuwaje kama tungeingia kudai uhuru tumegawanyika kwa misingi ya Uislam na Ukrist
Mwezi June, 1953 Makao Makuu ya TAA, New Street ilitangaza Kamati yake ya Utendaji: J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Katibu wa muhtasari; Wajumbe wa kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.
Mzee hii historia yako ina ukweli kiasi gani na inaweza kuthibitishwaje??
Sipendi...Ningeshangaa mada iishe bila mzee kuweka udini wa Nyerere na Sykes
Historia ni kwamba Nyerere alimzidi kura huyo Sykes kwenye uchaguzi pale kwenye ukumbi wa Anatouglo. Tena alikuwa hapewi nafasi kubwa ila ushawishi wake ndio uliwabadilisha wajumbe kumpigia kura Nyerere.Ndio nikawa nashangaa inakuwaje mtoto wa kikijini Butiama akamshinda mtoto wa mjini A.Sykes. kumbe kulikuwa na makubaliano/maoni ya namna. Kuna sehemu historian yetu hailezei vizuri haya mambo.
Economist,Acha uongo wewe Mzee. Sykes na Nyerere walishindanishwa kwenye uchaguzi wa chama Nyerere akashinda. Tena kura zilipigwa kwenye ukumbi wa Anatouglo. Punguza uongo.
Nyerere alishinda kwa kumzidi huyo kura na huo ndio ukweli...nikama leo tu Kuna watu wanaamini lowasa alishinda uchaguzi 2015 ila ilitumika busara tu na wapo wanaamini magufuli alishinda kihalali..kwahiyo utasimuliwa kutokana na ushabiki wa msimuliajiEconomist,
Ungepunguza hamaki ukauliza ungeongeza maarifa yako.
Nyerere hakika alishinda uchaguzi ule lakini uchaguzi ulikuwa umepangwa kuwa uongozi wa TAA apewe Mwalimu ili kuepusha TANU iliyokuwa inatayarishwa isiwe na viongozi walewale wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika).
Nyerere alishinda kwa kura chache sana.
Unaweza kusoma historia ya uchaguzi huu katika kitabu cha Judith Listowel, "The Making of Tanganyika," (1965).
Wazee wangu walitaka TANU iwe na sura ya chama cha siasa ambacho hakionyeshi kutawaliwa na Waislamu katika viongozi na wanachama wake:
View attachment 3618456
Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU akimsindikiza Nyerere Mahakamani 1958.
Nyerere alishinda kwa kumzidi huyo kura na huo ndio ukweli...nikama leo tu Kuna watu wanaamini lowasa alishinda uchaguzi 2015 ila ilitumika busara tu na wapo wanaamini magufuli alishinda kihalali..kwahiyo utasimuliwa kutokana na ushabiki wa msimuliaji
Unaniwekea video yako mwenyewe wakati nawewe ulisimuliwa tu
Mnachihanguuu,Unaniwekea video yako mwenyewe wakati nawewe ulisimuliwa tu
Wewe mzee hebu acha kutuona sisi ni vilaza. Sasa hapo ndio umeongea kitu gani?Abuu,
Wazee wetu waliona balaa lililoikumba India kwa kuingia katika kudai uhuru vyama vyao viwili Congress Party kikiwa chama cha Wahindu na Islamic League kikiwa chama cha Waislam.
Kila chama kinamtazama mwengine kama adui mkubwa.
Usiku 1947 wanashusha bendera ya Muingereza wanapandisha bendera ya India huru asubuhi vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaanza.
Vikamalizika kwa kugawana ardhi kila mtu na kwao.
Ilikuwa Abdulwahid Sykes achukue uongozi wa TAA kama President 1953 na 1954 waunde TANU na wadai uhuru.
Hamza Mwapachu akamwambia Abdul chama cha TANU kitakuwa kama Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) kwani Waislam tumejazana katika siasa Wakristo wako pembeni.
Njia ya kuwavuta Wakristo watuunge mkono ni Julius Nyerere atiwe kwenye uongozi wa juu wa TAA 1953 na 1954 TANU inaundwa na Nyerere anaongoza harakati za kudai uhuru.
Wakristo wataingia TANU kwani hawataiona TANU kama chama cha Waislam.
Kinyume cha hivi Waingereza watawaambia Wakristo waunde chama chao kupambana na TANU chama cha Waislam.
Tanganyika ingeingia kudai uhuru ikiwa na vyama viwili hasimu vilivyojikita kwenye dini.
Bahati mbaya mno Nyerere akiogopa sana kueleza ukweli vipi juu ya ugeni wake Abdul Sykes alimshika mkono hadi kuwa kiongozi wa TAA 1953 na TANU 1954 na 1955 akazungumza UNO.
Leo Tanzania hali ndiyo hii ingekuwaje kama tungeingia kudai uhuru tumegawanyika kwa misingi ya Uislam na Ukrist
Mwezi June, 1953 Makao Makuu ya TAA, New Street ilitangaza Kamati yake ya Utendaji: J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Katibu wa muhtasari; Wajumbe wa kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.
Huyu mzee analipwa kama sio kutumika kutuletea hizi story za kipuuzi.Acha uongo wewe Mzee. Sykes na Nyerere walishindanishwa kwenye uchaguzi wa chama Nyerere akashinda. Tena kura zilipigwa kwenye ukumbi wa Anatouglo. Punguza uongo.
Wewe ni muongo haya maneno yako sio kweli na unalenga kupotosha.Economist,
Ungepunguza hamaki ukauliza ungeongeza maarifa yako.
Nyerere hakika alishinda uchaguzi ule lakini uchaguzi ulikuwa umepangwa kuwa uongozi wa TAA apewe Mwalimu ili kuepusha TANU iliyokuwa inatayarishwa isiwe na viongozi walewale wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika).
Nyerere alishinda kwa kura chache sana.
Unaweza kusoma historia ya uchaguzi huu katika kitabu cha Judith Listowel, "The Making of Tanganyika," (1965).
Wazee wangu walitaka TANU iwe na sura ya chama cha siasa ambacho hakionyeshi kutawaliwa na Waislamu katika viongozi na wanachama wake:
View attachment 3618456
Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU akimsindikiza Nyerere Mahakamani 1958.
Mzee kilaza sana huyu. Analeta ushahidi akitumia maneno yake mwenyewe. Hapa ndipo hawa wazee wa kiislamu huwa wanafeli. Kupenda kuongea uongo na vitu vya kutengeneza kisha kuwajaza vijana ujinga wao.Unaniwekea video yako mwenyewe wakati nawewe ulisimuliwa tu
Zemanda,Wewe mzee hebu acha kutuona sisi ni vilaza. Sasa hapo ndio umeongea kitu gani?
Kumbe unayajua madhara ya udini sasa mbona umekazania sana kuutengeneza huo huo udini?
TANGANYIKA ya sasa imeuwa misingi yote ya udini wewe unakazana kupamba harakati za uhuru kuwa zilikuwa ni za kidini?
Una shida gani wewe mzee mbona hekima hauna?
Sisi unaotuhadithia haya mambo kila uchao hatukuelewi kwasababu maudhui yao ni ya udini mtupu ni kama unataka au shida yako TANGANYIKA igeuzwe kuwa taifa la kiislamu? Halafu baada ya hao ndio utakuwa umepata faida gani?
Kwanini unakuwa na akili na mawazo mpunyuko kiasi hiki kwa faida ipi haswa?
ACHA UDINI ,ACHA UDINI WEWE MZEE.