Ilikuwa ni siri nzito kati ya Zitto Kabwe na Bernard Membe dhidi ya CHADEMA

Huyo mpumbavu karudi tena humu? Ujinga wake apeleke fb huko.
Kuna harufu ya ukweli:
1. ATC Wazalendo ilipoanza, kwa watu wanajua kusoma alama, inaonyesha kabisa kulikuwa na nguvu ya watu walioko serikalini wanaisaidia kifedha na kuiondolea vikwazo vya kidola. Bila shaka hii ilikuwa ni project ya Membe (akidhani ataupata urais) na JK akisawapa ushauri.
2. Zitto ni mbinafsi na mwanasiasa hatari sana. Hii inajionyesha tangu akiwa Chadema na sasa baada ya huo mkakati kufeli.
 
Kama uliapa kutoyatoa mliyoyajadili kwanini umekiuka kiapo chako? Inaonekana wewe sio mtu wa kuaminika, Sasa kwanini tukiamini katika haya? Umetumwa na CCM au siyo? Umeona Zitto na Lissu wanayajenga umeamua kuua ndege wawili kwa jiwe moja, unamuharibia Zitto at the same time unamuharibia Membe.... Umefeli aisee
 
Siasa ni propaganda...

Huenda hata jamaa anapiga porojo ili kumzamisha Zitto aonekane mamluki...

Ikija 2020, ACT ya Zitto isiwe na meno tena
 
Jamaa hao ndo waliokuwa vipyoto kwenye kambi za upinzani!! Narudia kusema kuwa hakuna tena chama chochote chenye uwezo wa kupata wabunge wawili Tz Bara kwani 2015 walifanya kitendo hatari kwani wote walimpigia kampeni Dr Magufuli ambaye ndiye Rais wa Tz na watendaji wote wakuu wamerudi kundini(CCM)
Kwa kutumia boksi la kura au polisi? Ukitoa polisi kwa hali ya Siasa ya sasa CCM ndio hawapati Hata mbunge mmoja! Maana Jamii inawachukulia kama ni mijutu yenye roho mbaya, ila wanasemea blanketini huku wanawachekea! Poleni
 
Kaka engineer, hebu subiri kwanza; kama lengo la kuanzishwa ACT ni kuidhoofisha Chadema na wewe unaamini katika upinzani, imekuaje tena umeenda kujiunga CUF badala ya Chadema kinacho pigwa vita? Huoni kama umehamia tawi nyingine badala ya kwenda tu kwenye shina kama walivyo fanya wenzio?
 
HII NI SIRI NZITO YA BENARD MEMBE NA ZITTO KABWE MKAKATI HARAMU DHIDI YA CHADEMA NA UPINZANI HADHARANI

Na David Maphone.

Soma mwenyewe,

KWA UKWELI HUU SIONI SABABU YA KUWA KWENYE TAWI, BORA NIRUDI KWENYE SHINA KUU : PROF. KITILA (JANUARI 9, 2017)

Ni zaidi ya miezi 30 sasa tangu Siri ilipofichuka na kupelekea tukutane Kebby's Hotel kuanzia saa 01:20 jioni na kutafakari juu ya Hatma zetu Kisiasa. Pamoja nami walikuwepo Maingu Samson Mwigamba, Prof. Kitila Mkumbo na Ally Mwinyi. Tulikuwa tukimsubiri KC wa ACT- WAZALENDO ( Zitto Kabwe) ambaye tulikubaliana kukutana hapo muda huo.

Hata hivyo, ilitulazimu kusubiri hadi saa 02: 07 usiku ndipo Zitto alitokea na kutuomba radhi kwa kuchelewa kwa maelezo kwamba alikuwa anatafuta mwanya wa kumkwepa Msafiri Mtemelwa (Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho) aliyekuwa na shida zake binafsi na kwamba hakupenda ajue kwamba tulikuwa na mpango wa kukutana hapo kwa kuzingatia 'unyeti' wa suala lililopelekea tukutane hapo na kwa kuzingatia ukweli kwamba Mtemelwa ' hana kifua' cha kuhimili taarifa nzito bila kupayuka.

NINI KILITUKUTANISHA KEBBY'S?:
Mwaka 2015 Chama Cha ACT-Wazalendo kilishiriki Uchaguzi Mkuu kwa Mara ya kwanza, kikisimamisha Mgombea Urais (Mama Anna Elisha Mghwira), wagombea Ubunge, na wagombea Udiwani nchi nzima. Ili kufanikisha kupata angalau 5% za Kura za Ubunge na Urais na kukiwezesha Chama hicho cha zamani kupata Wabunge Viti Maalum, kila Mgombea Ubunge aligharamiwa mabango (picha ya Mgombea iliyowekwa pamoja na picha ya Zitto) nakala 500 kwa gharama ambazo awali zilidaiwa kufanywa na Zitto kutokana na Akaunti yake binafsi. Hata hivyo, Zitto, Kitila na Mwigamba walikuwa wanafahamu kwamba kulikuwa na Mfadhili aliyekuwa akikisaidia Chama kwa SIRI KUBWA na ni Zitto tu aliyekuwa na Taarifa Sahihi zilizokamilika juu Ufadhili huo na Malengo ya Mfadhili.

Tarehe 06/01/2017 ikafumwa barua yenye kurasa mbili (2) na inayojibu barua ya ukurasa mmoja ambayo iliwekewa Kiambatanisho chenye kurasa saba (7) zenye Mchanganuo wa Matumizi katika Uchaguzi Mkuu 2015. Nyaraka hizi kwa Muhtasari zilikuwa na taarifa zifuatazo ( nikizipanga kwa mtiririko):

1. Kulikuwa na Mchanganuo wa Matumizi ya Uchaguzi uliobainisha kwamba jumla ya bilioni 2.3 zilitumika kwenye Majimbo yaliyotajwa kwamba ni Majimbo ya Mkakati. Kwa Dar as Salaam Majimbo yaliyotajwa ni Ukonga (Milioni 43), Kibamba (Milioni 28), Kawe (Milioni 40) na Mbagala (Milioni 7). Tukitoa Majimbo ya Kigoma, jimbo lililotengewa Kiasi kikubwa zaidi cha Fedha ni jimbo alilogombea Mtemelwa huko Tabora lililotengewa Milioni 62. Majimbo yaliyobaki Dar es Salaam hayakuonekana kwenye Mchanganuo huo kwa kuwa hayakupewa chochote kwa kuwa hayakuonekana ya Mkakati ( Ingawa Kura alizopata aliyekuwa Mgombea wa Temeke Eng. Mohamed Ngulangwa zilizidi jumla ya kura zote za Mtemelwa, Ng'hilly (Kibamba), Janeth Rite (Kawe) na Ally Kifu (Ukonga) zikichanganywa).

2. Kulikuwa na barua iliyoandikwa na Zitto kwenda kwa Mfadhili iliyoomba Ufadhili wa Awamu ya NNE (4) ya Kuimarisha Chama ambayo pia iliambatanisha Mchanganuo wa Matumizi ya Uchaguzi yaliyotajwa hapo juu.

3. Kulikuwa na barua iliyomtaka Zitto abainishe ni kwa jinsi gani Mchanganuo huo wa Matumizi unaakisi 'MAKUBALIANO YA MWISHO YA HOLLIDAY INN' kabla ya kuzungumzia Awamu ya NNE ya Ufadhili.

Nyaraka hizi ambazo zilizofumwa kwa bahati mbaya, zilisababisha TAHARUKI Ofisi Kuu ya Chama hicho Makumbusho na kupelekea Mama Anna Mghwira asusie kufanya Majukumu ya Uenyekiti na kwenda kupumzika Singida kwa maelezo kwamba ALIFANYA KAMPENI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU YA KUTELEKEZWA NA KUACHA MADENI MENGI BILA KUJUA KWAMBA KUNA WALIOPEWA MILIONI 62 WAKAISHIA KUPATA KURA 500 TABORA. Hali hii ya Sintofahamu ndiyo iliyopelekea wengine pia tung'amue kwamba kuna Ufadhili na Malengo ya Mfadhili.

Baada ya kusikika kwamba mimi nilikuwa sehemu ya walalamikaji kwa kuwa Temeke ilitengwa kwenye Uchaguzi huo na hata Viongozi Wakuu wa Chama hicho hawakukanyaga Temeke muda wote wa Kampeni, ndipo nikaitwa Kebbys na nikatakiwa niongozane na aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho na Katibu wa Jimbo la Temeke, ndugu ALLY MWINYI ili ' tukawekane sawa'. HILI NDILO LILILOTUKUTANISHA KEBBY'S.

MAELEZO YA ZITTO YACHAFUA HALI YA HEWA KEBBYS:
Zitto aliwasili KEBBY'S saa 02:07 usiku na kutuomba radhi kwa kuwa amechelewa katika jitihada za kumkwepa Mtemelwa. Tukahama tulipokuwepo awali na kujitenga Pembeni na Kitila akaongelea sababu ya kuwepo pale na kilichojiri kwenye Chama na namna ya kudhibiti hiyo hali. Kwanza alisisitiza kwamba Chama hakina Fedha na si vema MTU kulalamikia mgawanyo wa senti ndogo inayotoka kwenye mfuko wa MTU binafsi. Kabla hajafafanua zaidi, Zitto akadakia:

" Actually Mimi simshangai wala kumlaumu Engineer katika hili. Anayeniumiza ni mama Mwenyekiti. Yeye anajua vitu vingi na sehemu ya Siri ya sisi kuanzisha Chama. Anajua hata namna yeye alivyodhaminiwa nchi nzima kugombea Urais wakati jina lake lilipitishwa pungufu ya siku moja kabla ya deadline.... Mama alishindwa nini kunikabili Mimi au wewe Prof. ili umfafanulie kwa nini hatukutenga fedha zaidi kwenye Urais..." Zitto akatoa waraka wa Makubaliano baina yake na Mfadhili na kumkabidhi Mwigamba na kumwambia " Brother naomba uwasomee jamaa kipengele cha 3 (d) maeneo niliyopigia mstari"

Mwigamba anasoma : " Ili kutimiza Lengo Kuu la kuipindua Chadema na kuifanya ACT-Wazalendo kuwa Chama Kikuu cha Upinzani, Majimbo ya Mkakati kwa Mujibu wa Makubaliano haya ni yale Majimbo yanayoshikiliwa na Chadema na wabunge wasumbufu. Mabadiliko ni lazima yafanyike Arusha Mjini, Iringa Mjini, Singida, Kawe, Ubungo (upande wa Mnyika), Mbeya Mjini, ....." ...." Inatosha...." (Zitto akamkatisha Mwigamba) na akaendelea:

" Comrades naomba mtambue kwamba Ufadhili huwa unatolewa kwa kuzingatia Matashi ya Mfadhili. Maagizo ya Mfadhili hayakuitaja Temeke kwa kuwa haiongozwi na Chadema wala haikuwa chini ya Upinzani wakati Makubaliano haya yanafanyika. Hivyo, si Kipaumbele cha Mfadhili...Nadhani Engineer tuko pamoja hapo..." (Akaweka kituo na kunisikiliza).

Nikauliza maswali mawili:

1. "Temeke na Tabora kwa Mtemelwa au Kibaha Mjini ni Majimbo yaliyokuwa na Status inayofanana, ilikuwaje hayo mengine ambayo hayakuwa chini ya Chadema yalitengewa fungu?"

2. " Ina maana ACT-Wazalendo kulikuwa tunapambania Majimbo ya Chadema na si kuing'oa CCM Madarakani.? Je Mfadhili kapokea vipi Matokeo baada ya Chadema kufanya vizuri zaidi na sisi kuambulia Jimbo moja tu na kushindwa kufikia 5% na kukosa hata Viti Maalum "?

Zitto akajibu:
1. Ngulangwa kwanza utambue kwamba Mchange kabla hajatuacha alikuwa ndiye ' link' kuu na Mfadhili kuanzia Awamu ya Kwanza ya Kuanzisha na Kueneza Chama nchi nzima wakati mimi bado nipo Chadema. Kitila na Mimi ingawa tulijikung'uta mifuko lakini Mahitaji ya Chama ni Makubwa zaidi. Isingewezekana kuteua Majimbo ya Mkakati bila kujumuisha Kibaha kwa Mchange. Pia Mtemelwa ni Naibu Katibu Mkuu, Mimi nilitetea Jimbo lake ili kujaribu kulinda status na pia kuepusha Vurugu zake endapo angekosa...Kuhusu Kigoma, hilo ni eneo Maalum kama 'Base' ya Chama na Mfadhili analijua hilo, hivyo tusiliingize kwenye Mjadala..."

2. Kuhusu Swali la pili naomba tusidanganyane - hakuna asiyejua kwamba kama kusingetokea mgogoro Chadema basi ACT isingekuwepo na huenda wewe Ngulangwa usingekuwa mbele ya Zitto Leo na kuhoji hayo. Anguko la Chadema kama lingetokea ingekuwa ni Faraja Kubwa kwetu na kwa wanachama wetu ambao zaidi ya 60% naamini wametoka Chadema. Pia tuondoe matumaini kwamba kuna Chama kitakachoing'oa CCM Madarakani bila ya ' mchoro' kuandaliwa na Vigogo wa CCM.

Kushindwa kwetu hakujamshughulisha Mfadhili kwa kuwa Mafanikio yetu yalitegemea yeye kuwa Mgombea Urais na hatimae Rais kupitia CCM. Kama Membe angekuwa Rais Leo basi Mimi ningekuwa Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni- NEC ingefuata Maelekezo tu na basically hata Fedha ya Kampeni ingetumika tu kuformalize Mchakato ili watu wasishangae sana..."

MWIGAMBA NA KITILA WAONGEA:
Maingu Samson Mwigamba alilaumu kwamba inawezekana Mchakato wa kumuengua ulianza muda mrefu.

" Nikiwa ni Katibu Mkuu wa Kwanza wa Chama niliyelala vumbini muda mrefu nashangaa kusikia Leo kwamba Ufadhili ulikuwa documented na kuna details ambazo kwa kweli zingine zilihitaji Mjadala. Nilisikia kuna Fedha ya Mabango ilitoka kwa KC na Kitila na kuna muda nililazimika kuhangaika kutafuta senti kwa wafadhili wadogo wadogo ili kumuwezesha Mgombea Urais angalau kumaliza Kampeni. Sikujua kwamba tulikuwa na akina " Mcharo" ndani ya ACT " ( Alitania na kuhitimisha Mwigamba).

"Mimi kwa upande wangu ningependa kuongea yafuatayo: " Aliongea Prof. Kitila na kuongeza:
1. Kama details ziko hivi basi waliolalamika wametusaidia kujua ambayo hata Mimi ninayejinasibu kuwa Msiri wako wa Karibu KC hukutaka niyajue. Kimsingi sikuwahi kujua kwamba Ufadhili wa Membe ulikuwa una masharti magumu hivi. Mwanzoni tulikuwa tunaambiana kwamba Mfadhili wetu alikuwa ni Makongoro na kwamba mpango wake ulikuwa agombee Urais kupitia ACT-WAZALENDO na hata tulipoona

Na hata tulipoonana naye Tabora ndicho nilichokuwa nakifahamu. Baada ya Mchange kuamua kukaa pembeni ndipo ukaniambia ukweli kwamba Mfadhili ni Membe na pia hukunipa hizi details kwamba angetaka tuwe ni Chama Mbadala wa Chadema wakati yeye ni Rais. Nakubali kwamba Ufadhili ni Muhimu kwa Chama Kichanga kama chetu, ila kuwa na Chama kilichojifunga kwenye Masharti yasiyoruhusu kuenea kwa Chama hicho siafiki. ACT wakati tunakianzisha binafsi sikuwa na mawazo kwamba ni CHAMA KITAKACHOTUMIKA KUPAMBANA NA WAPINZANI WENZETU PALE AMBAPO CCM NI CHAMA CHA UPINZANI. Kwa dhati kabisa, kama huo ndiyo utakaobaki kuwa Msimamo wa Mfadhili na tukakosa namna nyingine ya kujikongoja zaidi ya kukubaliana naye, binafsi sitoona MANTIKI YA KUTUMIKA KAMA TAWI LA CCM. NI BORA KUWA SHINA KUU KULIKO TAWI"...Alimali za Kitila bila Kufafanua.

Baada ya mazungumzo hayo niliwaomba Viongozi wangu hao nijiuzulu vyeo vyangu vyote na kukaa pembeni kama mwanachama wa kawaida. Zitto akasisitiza kwamba yeye amekuja Dar Mara moja kwa kuzingatia Umuhimu wa Kikao hicho na kwamba angesafiri usiku huo. Akanisihi nisifanye maamuzi yoyote ya kujiuzulu wala kuyatoa nje hayo tuliyoyaongea Kikao hicho. Nikampa nakala zote za nyaraka zilizotukutanisha KEBBY'S na kumuahidi yafuatayo:-

1. Nikaapa kutosambaza Chochote katika nakala ya Nyaraka hizo mitandaoni au kwa wanachama hata kama ningejiuzulu;

2. Nikaapa kutoitoa hadharani Siri hii ndani ya muda kamili wa juu wa mtoto kunyonyeshwa, tangu kuzaliwa mpaka kuachishwa kunyonya ( Kwa Mujibu wa Maneno ya Mwenyezi Mungu).

Tukaaga Mimi na Ally Mwinyi (ambaye alikuwa kimya muda wote) kwa makubaliano ya Zitto kututafuta ndani ya wiki mbili akirudi Dar es Salaam kufuatilia Mchakato wa Uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki, na kwamba tungemwita pia Mheshimiwa Anna Mghwira.

Binafsi nilichokipata KEBBYS kilinikinaisha na kamwe sikuwa na haja ya kukutana na yeyote kuzungumzia hayo ya ACT- WAZALENDO na MKAKATI WA MEMBE ULIOFELI. Nilitumia mwezi nzima nikitafakari HALI YA UPINZANI na nikawa najisikilizisha yale maongezi ambayo nilikuwa nimeyarekodi vipande vipande.

Ilipofika tarehe 13/03/2017 nikaandika barua ya kujiuzulu nafasi zote na hatimae nikajiunga na CUF - CHAMA CHA WANANCHI siku chache baadae, uamuzi ambao mwanzoni ulionekana wa haraka mno na ulibezwa na Mwigamba na Kitila kwa kuamini kwamba nafasi ya kumpinga Zitto kwa huo Mpango wa Unafiki ilikuwepo na huenda Zitto angeacha kubeba MAAGIZO YA MEMBE KIBUBUSA. Leo hii Kitila, Mwigamba, Ally Mwinyi, Edna Sunga, Mwantum Ally na Ernest Kalumuna ambao ni miongoni mwa waliokuwa Viongozi wa ACT-WAZALENDO walichukizwa na kuhama kwangu Mzambarauni, wapo CCM kutafsiri Kauli ya Kitila kwamba NI BORA KUWA SHINA KUU KULIKO TAWINI.

Leo 09/09/2019 ni zaidi ya miezi 30 tangu tukio la KEBBY'S. Nipo salama CUF-CHAMA CHA WANANCHI, nikiwa na nafasi kubwa kwenye Chama Kikubwa kuliko Chombo cha Membe.

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!

Eng. Mohamed Ngulangwa
N/Mkurugenzi Mambo ya Nje, Bunge na Sera,
CUF - CHAMA CHA WANANCHI

NB: Muda Kamili wa Kumnyonyesha mtoto ni miezi 30 kwa anayetaka Kutimiza Unyonyeshaji.(Kwa Mujibu wa QURAN).
Mwandishi David Maphone .
0714304970

Acha ujinga wewe.

Yaelekea ukiachana na mkeo utakuja kutuambia jinsi ulivyokuwa unaishi nae.
 
kwa hiyo unataka kuwachonganisha ACT vs Chadema vs Membe siyo?

watu wameombana misamaha baada ya kukashfiana huku ushahidi wa audio clips upo seuze hii michoro yako kwenye makaratasi?

jipange ndugu!!
 
Zito akili nyingi usri mwingi mzunguko sana kumjua kunahitaji akili ziada sio wakukurupukia atauza na kuwauza
 
Siasa ni propaganda...

Huenda hata jamaa anapiga porojo ili kumzamisha Zitto aonekane mamluki...

Ikija 2020, ACT ya Zitto isiwe na meno tena

CUF ya Maalimu Seif iko ACT-Waza Lendo, mleta uzi huu yuko CUF ya Lipumba, Je, ndg unategemea nini hapo? Sishangai kusoma hayo hapa muda na wakati kama huu
 
Sioni ajabu!
Wananchi wamekuwa waoga hawapiganii mageuzi ya kweli kutokana na woga tuu!
Viongozi wa vyama peke yao watafanya nini? Ni bora kutumia fursa yoyote itakayojitokeza maana hata yakitokea madhila mabaya yanawakumba viongozi wa vyama peke yao, wanachama wanaendelea na maisha kama kawaida as if hakuna kilichotokea.

Inawezekanaje kiongozi mkubwa kama Mkiti wa Chama hasa CDM anawekwa mahabusu zaidi ya mwezi halafu mambo yawe kawaida tuu? Hivi kweli Kenye wanaweza kumweka Raila mahabu? Hata kuitwa polisi tuu ni issue! Vipi hapa kkwetu?

Acha viongozi wajilipe humo humo wanateseka sana UNLESS wananchi tubadilike
 
Dah hakika dunia haina siri Yote Kwa Yote sisi tunapambania haki na usawa ndani ya nchi yetu Tanzania tupazeni Saut kwa umoja wetu jiwe mweupe mnoo Kama kalatasi.
 
Uongo mwingine uliosukwa

Si mlituambia ACT ni ya Lowasa, sasa imegeuka ya Membe?

Naona huu waraka una lengo la kuua ndege wanne kwa jiwe moja

1. Kumchongea Zitto kwamba anatumika na CCM
2. Kudai kuwa Membe siyo mwana CCM halisi bali ana hila na chama hicho
3. Kumsafisha Kitila mkumbo na Mwigamba wakati wao ndo vinara vya kuandika waraka wa mabadiriko
4. Kuigombanisha ACT na Chadema

Na bahati mbaya sana aliyeleta andiko hili ni mwanachama wa CUF - Lipumba....!!

Mpaka hapo mtu makini anaweza ku - sense ni nini malengo ya hii kitu....

Likely, anatafutwa Bernard Karmilius Membe ili labda "atetemeke" kisha akimbilie kumwomba msamaha Mzee Jiwe....

Duuh, kumbe mtu unaweza kuanza kuamini bila kupenda kuwa, siasa kweli ni mchezo mchafu kupindukia....!!
 
Back
Top Bottom