Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,973
- 831,536
Kuna kitu kinaendelea lakini bado hakijawa wazi sana. Ngoja mshtuko wa habari za kifo utulie... Kuna mengi yatajitokeza.
Wiki iliyopita kuna binti aliuawa gesti Chalinze... ALINYONGWA.... Lakini muda mchache kabla ya mauaji kufanyika alipigiwa simu na ndugu yake wakati wauaji wakiwa tayari chumbani kwake... Akiwasiliana kilugha na huyo ndugu yake alimwambia kuna wanawake wanne wamemvamia chumbani lakini watatu anawafahamu.
Baada ya hapo simu zake hazikupatikana tena! Maiti yake iligundulika siku ya pili. Katika kufuatilia undani wake ikaonekana alikuwa kwenye mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya. Na kulikuwa na tatizo kati yake na hao wauaji wake.
Hii ilitokana na mawasiliano yaliyofumwa kwenye simu yake
Mchana wa siku aliyouliwa kulikuwa na majibizano kwa njia ya maandishi
Yeye aliandika kuwa kwakuwa wao wamemwaga mboga basi yeye atatoboa sufuria kabisa naye akajibiwa kuwa hatasubiri afanye hivyo watamfuata huko huko juu.
Baada ya mazishi kaka yake mmoja akapigiwa simu kupewa pole na kuambiwa kila kilichotokea pale msibani mpaka kuzika. (Kwahiyo wauaji walikuwepo msibani) kisha akaambiwa kuwa MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI.
Baada ya kama siku tatu za mauti yake binti mwingine akakutwa kauliwa kwa kuchomwa visu mwili mzima (alikuja Kutambuliwa kama mmojawapo aliyeshiriki mauaji ya kwanza), na mwingine naye akaponea chupuchupu akiwa keshakula visu vya kutosha na sasa hajulikani alipo.
Scenario nzima inaonesha ni mauaji ya visasi kati ya makundi mawili na kuna kitu kikubwa kinafichwa!!!!
Ni vigumu kwasasa kulink kifo cha Agnes na hayo mauaji mengine lakini tayari kuna watu wameshaanza kutuhumiwa.
Agnes Masogange amekuja kuwa maarufu zaidi baada ya kuja kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya. Tuhuma dhidi ya madawa ya kulevya zilipelekea akamatwe na kufunguliwa kesi.
Ni juzi tu hapa mwezi uliopita alikutwa na hatia na kuhukumiwa kulipa faini au kifungo. Alinusurika kifungo kwa kulipa faini iliyolalamikiwa na wengi
Mabush lawyer wengi walisema kuwa kesi kama ile kama huna watu wazito nyuma yako unaondoka na maji.
Kwanini kifo chake kimeacha mashaka!?
Mitandao ya hizi biashara haramu., haipatani kabisa na kitu kinaitwa polisi... Kwa baadhi ya nchi watuhumiwa hufuatwa na kuuliwa huko huko jela au mahabusu.
Masogange akiwa tayari kwenye spotlight ya polisi... Nini ingekuwa future yake!? Kumbuka ni vigumu tena kumtumia kwenye hiyo biashara.. Tayari ana file.. Hivyo keshakuwa ndege mweupe!
Lakini je anafahamu mangapi!? Je hawezi kuropoka?
Je, ni nani aliyekuwa tayari kugharamia maisha yake ya anasa wakati sasa hawezi tena kuzalisha!?
Risk ni zipi akiachwa hai?
Risk ni zipi akinyamazishwa!!?
Je, baada ya kesi kwisha alikuwa na madai kwa washirika wake kibiashara!?
Kifo hupangwa na Mungu kwa wale waamini. Lakini nyuma yake kuna sababu za kifo. Naamini siku moja ukweli utajulikana.
RIP ⚰ Agnes!