Ilikuawaje Yanga wakaweka bango la kuonesha kwamba wameifunga Simba 5 -???

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,305
33,924
Kwa zaidi ya mwezi sasa nafanya utafiti kuona kama kuna timu nyingine duniani zaidi ya Yanga, iliwahi kubandika bango barabarani kuonesha kwamba wameifunga timu nyingine, mpaka sasa bado sijapata!!

Kiliwatokea nini wana Yanga kuja na wazo kama lile!!
 
Sasa ulitaka yanga iige timu nyingine duniani... wao ndio wameamua kuanzisha wengine watafuata.
Kila kitu sio lazima kuiga heshimu maamuzi yako binafsi/taasisi
Sawa wao ndiyo waanzilishi...

walifanya vile ili iweje??
 
We uliona wapi timu inamuweka mchezaji kwenye box la maoni kama surprise ya utambulisho wake?

Kwenye Sanduku la maoni zinakaa barua tu humo hata mchwa humkuti kwasababu hali ya mle sio rafiki kwa kiumbe hai yeyote, lakini Yanga wakamuweka Okrah.

Wakati wao wakiwa na malengo ya kufanya tukio liwe na surprise ya maajabu kupitia identity ya jina la mchezaji "magic"

Lakini ajabu ambayo ilionekana mbele ya audiences ilikuwa ni kivipi binadamu akawekwa kwenye sanduku la maoni na akatoka akiwa mzima bila dhoruba yeyote??

Okrah kama aliweza kuhimili kwenye lile S.L.P basi mchizi atakuwa ni nunda nimejaribu kuangalia CV yake kama ashawahi fanya kazi kwenye viwanda vya steel kitengo cha jikoni kuopoa nondo za moto

Lakini sijapata hizo taarifa so sijajua ni kipaji tu au mchizi aliifanya kama hobby kutokana na nature ya u-hardcore
 
Kwa zaidi ya mwezi sasa nafanya utafiti kuona kama kuna timu nyingine duniani zaidi ya Yanga, iliwahi kubandika bango barabarani kuonesha kwamba wameifunga timu nyingine, mpaka sasa bado sijapata!!

Kiliwatokea nini wana Yanga kuja na wazo kama lile!!
Ubunifu wa kipekee ule...
 
Kwa zaidi ya mwezi sasa nafanya utafiti kuona kama kuna timu nyingine duniani zaidi ya Yanga
Kama ungeipata hiyo timu nyingine ungefanyaje?

Kwa hiyo kwakua hakuna timu iliyowahi kufanya ivyo basi haitakiwi Yanga kufanya ivyo?

Jambo likifanywa na sisi mnaanza kutafuta kama kuna sehemu nyingine lilishawahi kufanywa. Matatizo ya kutokujiamini
 
Ni kweli hawana akili kama ni goli tano hata zaidi ya tano Simba amewahi kumfunga Yanga maana ndio sehemu ya mchezo WA makosa kama alivyosema msemaji WA Singida. Hakuna ajabu hata timu zenye nyota WA dunia wamewahi kufungwa idadi kubwa ya magoli.
 
Makolokolo mna akili ndiyomaana mna historia ya;

* Kugongwa sana na Yanga SC kuliko klabu yoyote duniani.

* Kugoma kurudi uwanjani kipindi cha pili zaidi ya mara 2 ikiwemo mara 1 kugongwa 4-0.

* Kutokuwa na makombe mengi ya TPL isipokuwa FA pekee.

Makolokolo SC kwa Yanga ni sawa na Barcelona SC kwa Real Madrid.

Endeleeni tu kukaza mafuvu Makolokolo............

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom