Ilichokisema NSSF kuhusu mafao ya walioachishwa kazi

Bedui la bongo

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
297
306
Dar es Salaam. Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limesema limeanza kutekeleza maelekezo ya Rais John Magufuli na wanachama wake watakaopoteza ajira kupewa mafao yao kulingana na utaratibu wa mfuko huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Januari 6, 2019, meneja kiongozi wa matekelezo wa NSSF, Cosmas Sasi amesema fao la kutokuwa na ajira katika mfuko huu linaendelea kulipwa kama kawaida.

Amesema malipo hayo ni kwa watu ambao mikataba yao ni ya muda mfupi na ambao si rahisi kupata ajira nyingine baada ya kuachishwa.

"Kwa wanachama wetu ambao wanafanya kazi za muda mfupi kama ujenzi katika mradi fulani baada ya mradi huo wanaweza kuchukua michango yao na riba kidogo hata wale wenye ajira katika kampuni, ajira zao zikisitishwa wataweza kupata mafao yao," amesema Sasi.

Amesema kwa watu ambao mikataba yao ya ajira inasitishwa lakini ni wataalamu na wana ujuzi fulani endapo watakuwa wamechangia kwa miezi 18 watapata pensheni ya kutokuwa na ajira kwa miezi sita ambayo ni theluthi moja ya mshahara waliokuwa wakipata, na baada ya hapo endapo itathibitika kuwa amekosa ajira atapewa michango yake yote pamoja na riba.

Amesema utaratibu huu utawahusu wanachama ambao ajira zao zitakoma au watakaoachishwa kazi na si walioamua kuacha wenyewe na watalipwa baada ya mfuko kujiridhisha na hali zao za ajira kwamba kweli wamekosa kazi.



Sent using Jamii Forums mobile appiphone
 
endapo itathibitika amekosa ajira ...hapo ndo upigaji unaanzia hapo ikiwemo rushwa kwa watendaji wa hii mifuko.
 
Back
Top Bottom