Ilianza na sinza kwa wajanja leo hii maana nzima imepotoshwa.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Miaka ya 80 katikati kuelekea mwishoni, ndipo eneo la sinza lilipoanza kupata wakazi wengi wapya, kabla ya hapo Sinza haikuwa na shughuli nyingi kama ilivyo leo. Sinza ikapewa jina la "kwa wajanja", kwani watu waliokuwa wanajenga eneo lile walikuwa ni wafanyabiashara na wafanyakazi wa serikali wenye pato kubwa.

Enzi hizo mtu akipata fedha ananunua eneo sinza na kujenga nyumba nzuri. Likaibuka tabaka la watu wa kati wenye maisha ambayo wakati wa awamu ya kwanza, hayakuwepo. Sinza kwa wajanja pakawa ni kwa wajanja kweli.

Lakini taratibu ile maana halisi ya neno "mjanja" ikaanza kupotea, kundi la wezi wanaoiibia serikali yao na lenyewe likajumuishwa kwenye hao wajanja. Kundi la mafisadi na lenyewe likawa ni sehemu ya wajanja.

Leo hii vita ya kupambana na ufisadi inabidi ifanywe kwa umakini mkubwa na haitachukua miezi miwili au mitatu kwa sababu watu wameshajenga dhana potofu kwamba kuiba ni ujanja.

Kuchora michezo michafu ya wizi wa mabenki, kunaonekana ni ujanja. Limeibuka tabaka la watu wenye dharau kwa sababu ya walichonacho lakini kimetokana na huo ujanja feki.

Maana ya neno mjanja imegeuka kuwa mtu mwizi, mwenye uwezo wa kuishi maisha yasiyofanana na pato lake.

Ujanja tunaousifu ambao umechanganyika na wizi ni mzigo kwenye hatima ya nchi yetu. Tubadilike waungwana ili neno mjanja lirudi kwenye maana iliyokusudiwa awali.
 
Usihofu hii ndo Bongo hakunaga lililo kuwaga na mwanzo likakosaga kuwa na mwisho
 
Back
Top Bottom