Ili Usitoe Pesa kwa trafick police fanya hivi!

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
624
hii njia nimeitumia mara tatu na naona inalipa sana.
1)Kama kweli umekosa kubali kosa, omba msamaha (lazima atakataa na kudai pesa), mwambie akuandikie notification na utalipa hata kama iwe laki moja (huwa wanataja figure kubwa kukutisha

2.)Usianze kubargain, mwache ajikanyage kanyage, akikuambia anakupunguzia makosa mwambie kwa unyenyekevu NASHUKURU LAKINI HAPA SINA HATA SENTI TANO, NIANDIKIE TU NOTIFICATION NITALIPA, akikuuliza utalipa lini mwambie SIKU YEYOTE NDANI YA SIKU SABA LAKINI SIO LEO, KWA SABABU SINA HELA SASA HIVI

hapo askari anajua unaelewa mambo, anakasirika lakini anakuachia fasta!
 
JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,900
3,226
Mkuu sina ufahamu sana juu ya hizi notification, je kuna sheria inayotaka ulipie papo kwa papo, au trafik akiamua tu kukutesa, niliwahi kukamatwa na trafiki mikumi akaniandikia 20000 nilipomwambia nitaenda kulipia DSM akakataa akataka nipeleke gari kituoni hadi nitakapolipa hiyo fine, ilinibidi nilipe ili niendelee na safari. Sasa hapo ni kweli yule trafik alikuwa sahihi??/
 
Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
624
alichemka saaaana, pale pale katika kitabu chao cha notification kuna maelezo, unatakiwa ulipe nadani ya siku saba! narudia siku saba! just a common sense, unapoendesha gari sheria iko wazi lazima ubebe leseni ya kuendeshea lakini hutakiwi kubeba pesa just incase umekamatwa. . . .HUYO TRAFIC ALICHEMSHA!

mi nimekamatwa mara nyingi lakini sijawhi kutoa pesa! isipokua kama uko na haraka mara nyingine inasumbua b'se anachofanya askari ni kukupotezea muda na kujaribu kukuonyesha ni jinsi gani hako kajikosa (inaweza kuwa hujafunga mkanda, huna fire ext au triangle) eti ni hatari
 
Amoeba

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
3,292
763

Umeeleza sahihi kabisa mkuu, isipokuwa hiyo sentensi yako ya mwisho haijakaa vizuri. Kutofunga mkana, au kutokuwa na fire extinguisher inayofanya kazi kunaweza kusababisha "kifo au vifo"-kuna hatari zaidi ya hiyo?
 
Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,133
17,103
mkuu sina ufahamu sana juu ya hizi notification, je kuna sheria inayotaka ulipie papo kwa papo, au trafik akiamua tu kukutesa, niliwahi kukamatwa na trafiki mikumi akaniandikia 20000 nilipomwambia nitaenda kulipia dsm akakataa akataka nipeleke gari kituoni hadi nitakapolipa hiyo fine, ilinibidi nilipe ili niendelee na safari. Sasa hapo ni kweli yule trafik alikuwa sahihi??/

alikunyanyapaa

akuna sheria inayolazimisha kulipa hapo hapo mkuu ni ndan ya siku saba top
 
Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,618
2,120
Alafu kitu kingine jamani kama ulilipa iyo 20000 badala ya receipt wakakupa notification sasa huoni kuwa huo ni uhuni?
Hawa matrafic huwa wananikera sana nkiwaga na muda huwa nakomaaga nao sana
 
Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,133
17,103
Kwa kuongezea labda ukiwa kwenye gari akikisha

umefunga mkanda

uko na fire ext

uko na license

uko na kedi yao ya nenda kwa usalama

uko na zile triangle

taa zinawaka zote,

ukitimiza hiki ataishia kuuliza fungua buti kama inafunga vizuri ...wengi ukiwa navyo hivi anakwambia safari njema,,tukubali wengi wanatembea na makosa barabarani na si awajui wanajua kutokuwa na triagle faini ,license shida na bado unaendesha si upaki kama huna rl,ins unangangana na nini...kesi zake kubwa
 
Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,618
2,120
Huwa nabeba mpaka first aid kit kwa jinsi ninavyokerwa na trafic ila issue ni overspeeding hasa ukifika iringa kama unaambaa naDSM- Tunduma highway
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,214
22,991
Traffic police hawezi kuomba rushwa asipokukuta na kosa.
So.. ondoa rushwa barabarani kwa kufanya yaliyo sahihi humo barabarani!
 
Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,681
7,245
Kwa kuongezea labda ukiwa kwenye gari akikisha

umefunga mkanda
:embarrassed:

uko na license

uko na kedi yao ya nenda kwa usalama

uko na zile triangle

taa zinawaka zote,

ukitimiza hiki ataishia kuuliza fungua buti kama inafunga vizuri ...wengi ukiwa navyo hivi anakwambia safari njema,,tukubali wengi wanatembea na makosa barabarani na si awajui wanajua kutokuwa na triagle faini ,license shida na bado unaendesha si upaki kama huna rl,ins unangangana na nini...kesi zake kubwa

Mkuu vipi na ile stika ya faya eksitinguisha?
 
Avocado

Member
Aug 23, 2010
97
4
Wadau issue ya traffic ni ngumu sana kuwafanya watende kazi zao kwa haki,mambo matatu amabayo haytaondoa rushwa ni haya:
1.Uelewa mdogo wa sheria kwa watanzania wengi,si madereva tu !
2.Ubovu wa magari.
3.Mtandao wa rushwa ndani ya jeshi la polisi.
Nikizungumzia jambo la kwanza ni kuwa watanzania wengi hatukupta nafasi ya kufundishwa sheria ambazo zinaweza kutupa ufahamu wa wajibu wetu na haki zetu,kama jinsi wadau wengi walivyo changia juu ya suala la NOTIFICATION hii imekuwa silaha kubwa sana kwa matrafiki wengi kuwamailiza madereva wasiojua nini kimeandikwa katika karatasi ile,na bahati mbaya sana bado tumekikumbatia kiingereza katika sula zima la sheria,ile karatasi ya notification ina maelezo ya wazi kabisa ambayo endapo yangeandikwa kiswahili yasingeleta utata,kuna makosa 39 yaliyoainishwa wazi japo unweza kubambikiwa hata kosa ambalo hailmo kisheria kutokana na kutokuelewa lugha,pi ni wazi kuwa ndani ya siku saba unatakiwa uiulipe faini ya kosa ulilotenda.
Pili kuhusu ubovu wa magari hili ni jambo ambalo hata jeshi la polisi hawalikazii sana kwani nao wanaamini endapo hakuta kuwa na magari mabovu hawata kuwa na ulaji,najua kabisa kama wangetaka magari mabovu yasiwepo barabarani wangeweza kuyaondoa,na sisi wadau tunatakiwa tujue kuwa uzima wa gari lako ndio usalama wa maisha yako na ya wadau wengine,kwani ukiwa na gari bovu unaweza kuwasababishia ajali wadau wengine pia.
Tatu mtandao wa rushwa ndani ya jeshi la polisi ambapo askari hupewa malengo ya makusanyo na wakubwa wao,na hata sehemu za kufanyia kazi hupewa watu kwa vigezo vya makusanyo mazuri utakayo yawakilisha kwa wakuu wako.Kama huamini waulize madereva wa mbasi ya abiria ya mikoani na daladala watakuambia,na hizo pesa ni lazima utoe ili uendelee kufanya biashara,kwa siku daladal inaweza kutoa hadi sh 10,000 hiyo haijalishi kama gari bovu au zima hiyo ni rushwa ya lazima,waulize wadau wa mbeya watakuambia. Kilichopo ni kwa wadau wote kutafuta njia muafaka wa kumaliza tatizo hili vinginevyo tunakoenda hali itakuwa mbaya sana !
 
mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,916
5,079
Post nzuri sana hii, na je traffic kuchukua leseni kabla ya kulipa na kudai atakurudishia ukishalipa faini ndivyo sheria inavyosema?
 
Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,133
17,103
Post nzuri sana hii, na je traffic kuchukua leseni kabla ya kulipa na kudai atakurudishia ukishalipa faini ndivyo sheria inavyosema?

traffic aruhusiwi kuchukua chochote ndugu na kama unamwachia leseni yako basi hata mke atabaki nae..nini maana akichukua anampiggia mwenzake wa mbele anakulamba kama yeye na wa mbele anapigiwa unakuta kutokana na kutoelewa unafinywa kijinga..mi kwanza nikisimamishwa swala la kwanza nalock gari zima na kuhakikisha vioo vyote viko juu kasoro changu na ananifwata na si kumfwata naongea nae nusu kioo...wengi wanawapa nafsi ati anasimamisha anafungua kama anaenda TUONANE GUEST HOUSE na huku anataka hela ...tujue sheria akuna atakaetutesa na ahuku ukihakikisha akuna kosa kwenye gari yako
 
Avocado

Member
Aug 23, 2010
97
4
Wito wangu ni kwa madereva kujifunza, kuzijua na kuzifuta sheria za usalama barabarani na kutembea na magari mazima hilo ndilo suluhisho.Hakuna atakae kubabaisha :teeth:
 
Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,685
13,198
Humu kuna ndugu na marafiki wa mapolisi sasa hizi technicks si watajua haraka sana ?........................siamini km kuna namna ya kuwakwepa hawa jamaa zaidi ya kuwapa ganji nawe ukajikata fasta kwani wanapotezea sana muda.............makosa yenyewe mengi sana na pesa za kulipia hatuna sio kwamba hatutaki ila maisha bora hayapatikani.......na wao wanchukia zaidi km wewe unataka kulipa faini kamili.....anyway...sijui cha kufanya
 
Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,469
722
hii njia nimeitumia mara tatu na naona inalipa sana.
1)Kama kweli umekosa kubali kosa, omba msamaha (lazima atakataa na kudai pesa), mwambie akuandikie notification na utalipa hata kama iwe laki moja (huwa wanataja figure kubwa kukutisha

2.)Usianze kubargain, mwache ajikanyage kanyage, akikuambia anakupunguzia makosa mwambie kwa unyenyekevu NASHUKURU LAKINI HAPA SINA HATA SENTI TANO, NIANDIKIE TU NOTIFICATION NITALIPA, akikuuliza utalipa lini mwambie SIKU YEYOTE NDANI YA SIKU SABA LAKINI SIO LEO, KWA SABABU SINA HELA SASA HIVI

hapo askari anajua unaelewa mambo, anakasirika lakini anakuachia fasta!

Mkuu sasa vipi akisema twende kituoni na leseni yako kachukua si ukifika kule lazima wakugombanie kama hujamalizana nae?
 
Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,604
1,065
kwa waendesha pikipiki tunakerwa zaidi. Road licence inatakiwa ibandikwe ndani kwenye kioo - pikipiki haina kioo
Insurance sticker hivyo hivyo. Ukinunua kale kaholder kamoja, vitu hivyo viwili tayari kamejaa. Bado sticker ya nenda kwa usalama, siijui nayo utaibandika wapi. Inaonekana sheria za magari zimepelekwa moja kwa moja kwenye pikipiki bila kuangalia utekezaji wake. Utaona hata road licence ya pikipiki ni 50,000! kwani imewekwa katika cc 1-500. Kama una pikipiki ya 750cc utalipia 100,000 na gari la over 2500cc linalipiwa 200,000 (semi trailler, buses etc) Rationale iko wapi hapo?
 
sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,259
641
Post nzuri sana hiii nadhani hata kama humu kwenye jf kuna askari atapeleka taarifa kuwa watanzania wa sasa siyo wale wa zamani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom