Elisha Chuma
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 275
- 262
Sehemu kubwa ambayo bado kama taifa na mtu mmoja mmoja tunafeli sana ni kwenye eneo la ujenzi wa ufahamu kwa watoto na vijana,Asilimia kubwa ya fahamu zetu zimekariri ushindi sana kuliko hatua za ushindi.
Hii haiko kwenye biashara tu bali hata kwenye maisha yetu ya kawaida,mahusiano,uchumi na kila kitu.
Fahamu zimejengwa kila unachofanya tegemea kushinda tu,lakini pia hata washauri pia ama motivational speaker tumejikuta katika wimbi lile lile kuwaambia watu mbinu za ushindi tu lakini uhalisia wake ni kushindwa.
Hauwezi kujua kama umeshinda iwapo hujui kushindwa,hakuna safari isiyokuwa na vikwazo,ikikosa vikwazo inapunguza umuhimu wake,ndio hata maisha ni taratibu za kutatua changamoto siku baada ya siku na ukifanikiwa unaita ushindi na unapata furaha.
Mafanikio yanagharama yake na moja ya gharama ni vikwazo na kufeli ili upate thamani ya mafanikio halisi,hivyo katika kila unalolifanya tegemea kuna kufeli ama kufanikiwa hata kama ufahamu wako umeuelekeza kufaulu lakini jipange na ikitokea umefeli ili isikuvunje nguvu.
Leo hii wajasiriamali wengi wanafeli sokoni sababu walijiandaa kufaulu tu,ndoa nyingi zinavunjika sababu zilijiandaa furaha tu,mahusiano mengi hayadumu sababu yanataka raha tu.mikopo inakuwa shida marejesho sababu hakuna kujipanga na iwapo ikitokea nimekosa nitafanya nini, karibia kila kitu kinasababishwa na kutokujiandaa kwa matokeo hasi.
Badilisha mtazamo wako na fungua ufahamu wako,changamoto ndio ukuaji,changamoto unayoipata leo ndio itakayokuimarisha kesho.tatua na endelea jenga ufahamu vizuri kwa kizazi chako pia.
Ili ufanikiwe unahitaji kufeli ili uione gharama na hadhi ya kufikia mafanikio.
Elisha Chuma.