Ili ufanikiwe maishani kipi kitangulie gari, nyumba au ndoa?

busness

Member
May 1, 2014
27
9
Niko job of sin kuna Mfanyakazi mwenzangu kaja na fomu ya mkopo wa bank nilipojaribu kuisoma kujua mashariti Tao nimegundua kipengele cha dhumuni la mkopo ikanibidi ma Mimi nivae viatu vya muhusika nikafikiria mambo matatu ya kuanza nayo maishani napenda sana kuwa na gari pia napenda kuwa na familia yaani mke na watoto tatu napenda kuwa na kwangu yaani nyumba yangu haya yote yanahitaji maandalizi yaani pesa njia panda yangu ni kwamba kipi kikianza kitanipa urahisi wa kupata mawili yaliobaki nikianza na mke nitapata gari na Nyumba maana matumizi yataongezeka au nikianza ujenzi nitakaa muda bila kuoa naomba ushauri kipi nianze nacho.
 
Fursa uliyonayo ina nafasi kubwa. Nyumba inahitaji uwekezaji mkubwa, kama fursa inakuruhusu ukianza na nyumba ni kutu kizuri zaidi. Lakini kama ni vigumu anza familia maana unaweza kusubiri sana kutimiza ndoto ya nyumba. Hata hivyo, kuna uwezekano wa kupata mkopo wa kukuwezesha kujenga halafu ukahamia kwako kisha mengine yakafuata (kumbuka mkopo nao ni fursa). Ni raha sana ukioa unaishi kwako na gari unapaki kwako ... sio kupaki CCM!
 
Hapo inategemeana na malengo yako mwenyewe uliyoyapanga,kuna wengine walianza kujenga na wamefanikiwa wengine wameanza familia na wamefanikiwa na wengine walianza na gari wamefanikiwa pia ila unatakiwa uangalie income yako inaruhusu lipi kuanza,kama ni ya kawaida anza na mawili kati ya kutengeza familia au gari maana kujenga inahitaji uwekezaji mkubwa na wa muda mrefu lakini kama una kipato kkubwa then anza kujenga kwanza
 
Cha kwanza kabisa ni uhakika wa kula na kushiba,inakuja ndoa kisha nyumba na vingine kufuata

"utakapo kula na kushiba kisha ukajenga nyumba nzuri usimsahau Bwana Mungu wako...."

 
Inategemeana na kipato chako,mfano me nilipata mkopo wa milioni nane nikaamua kununua gari kwanza nikaifanya tax bubu nikawa naendesha mwenyewe,nikadunduliza nikafungua kijiwe cha kuziba pancha nilipomaliza mkopo nikachukua mwingine nikanunua kiwanja na kuoa, tuneshirikiana vyema na mamatoto niko kwangu,just mipango na malengo na unayatimiza vp.
 
cha KWANZA NI MUNGU......
tuliza akili mimi baba angu alisema wekeza kwenye ARDI as u can...nunua kiwanja kwanza tafta pesa ya kujeng then nunua gari ambalo litakusidia hta kubebea vifaa vidogo dogo wenye buti kwa ajili ya ujenzi

mwanamke weka mbali...timiza malengo ndo ufikirie suala la kuoa na kuwa na familia
best wishers
 
Mi nimeanza na nyumba nilianza mwaka jana mwezi wa 12 na sasa mwezi huu napaua, ila nitasimama kwanza nioe, ila natamani sana kua nagari kabla ya kuoa ili nijiongezee heshima, maana ukioa huku una gari heshima inaongezeka. ushauri usijenge kwa kutumia mkopo nyumba haitaisha labda ukope zaidi ya milion 50. na usijenge kwa kutumia mshahara utatumia miezi 50 kama utakua unatumia milion 1 kwa mwezi. Tumia mkopo kufanya biashara na biashara ndio ijenge na kununua Gari .


selfish
 
...kila mtu na mapenzi yake duniani

wengine magari

wengine majumba

wengine Mungu

wengine ni furaha maana unaweza kuwa na gari nyumba pesa ila huna furaha

wengine ni amani tu ya moyo, hata akiishi nyumba ya udongo mradi ana amani anaishi kwa furaha

wengine mradi anakula, akiumwa anaenda hospitali kwake yeye ni mafanikio tosha
 
Mi nimeanza na nyumba nilianza mwaka jana mwezi wa 12 na sasa mwezi huu napaua, ila nitasimama kwanza nioe, ila natamani sana kua nagari kabla ya kuoa ili nijiongezee heshima, maana ukioa huku una gari heshima inaongezeka. ushauri usijenge kwa kutumia mkopo nyumba haitaisha labda ukope zaidi ya milion 50. na usijenge kwa kutumia mshahara utatumia miezi 50 kama utakua unatumia milion 1 kwa mwezi. Tumia mkopo kufanya biashara na biashara ndio ijenge na kununua Gari .


selfish

Nimeupenda ushauri wako.
 
Back
Top Bottom