Ili uenyekiti wa CCM uwe uliotaka Magufuli omba kura ya siri ujue ukubwa wa tatizo ndani ya chama

RingaRinga

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
1,041
510
Ili Mh. Rais uweze kujua hali halisi ilivyo ndani ya CCM nakushauri uombe kupigiwa kura ya siri ili uijue CCM yako na ili pia ujue unafanya kazi na watu wa namna gani.Kama hawatakuchagua hewala kwa kuwa itakurahisishia zaidi utendaji wako kwa kazi moja tu ya urais ingawa hiyo itakuwa ni zahma kwa CCM, ila kama watakuchagua kwa namna yoyote usisite kukisafisha chama maana kinahitaji mfagio tena wa shaba, maana ni bora kuanza upya kuliko kuliko kuendelea na njia iendayo upotevuni.
 
Ili Ndugu Rais uweze kujua hali halisi ilivyo ndani ya CCM nakushauri uombe kupigiwa kura ya siri ili uijue CCM yako na ili pia ujue unafanya kazi na watu wa namna gani.
Kama hawatakuchagua hewala kwa kuwa itakurahisishia zaidi utendaji wako kwa kazi moja tu ya urais ingawa hiyo itakuwa ni zahma kwa CCM, ila kama watakuchagua kwa namna yoyote usisite kukisafisha chama maana kinahitaji mfagio tena wa shaba, maana ni bora kuanza upya kuliko kuliko kuendelea na njia iendayo upotevuni.

Ninavyoelewa mimi siku zote Mwenyekiti wa CCM huchaguliwa kwa kura ya siri
 
Uchaguzi wenu mnataka waTanzania wote watege masikio huko ,hivi inawahusu nini maana wakimchague wasimchagu 2020 kama mtafika tunawatoa kimzobemzobe ! Tunaona sasa wanavyopapatika kama samaki waliotolewa kwenye maji wakawekwa nchi kavu,mara majipu,mara vidonda juzi jana wameitana wezi na kuachichwa ukurugenzi wanaingia wengine kuchukua chao mapema,siku zenu CCM zinakaribia ukingoni.
 
Back
Top Bottom