LGE2024 Yaliojiri upigaji wa kura za maoni ndani ya CCM Mitaa ya kata ya Msigani Ockoba 23, 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
921
1,815
Kata ya Msigani inapatikana Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Kata hii inajumla ya Mitaa mitano ambayo ni Mtaa wa Msigani, Mtaa wa Temboni, Mtaa wa Malamba Mawili, Mtaa wa Msingwa na Mtaa wa Kwa Yusufu.

Aidha kwa mwaka huu kumekuwa na muhamko mkubwa sana kwa wanachama wa CCM katika Kata hiyo kijitokeza katika upigaji wa kura za maoni ukilinganisha na miaka mingine

Hali ilivyoenda katika kupiga kura za maoni

Upigaji wa kura za maoni mchakato mzima ulienda sawa licha kulijitokeza vichangamoto vidogo kwa upande wanachama ambao hawakulidhika kwa namna Fulani hivi kupokea matokeo lakini kiukweli kulikuwa hakuna kabisa vurugu hadi kufika hatua za kuumizana kama tulivyoshuhudia baadhi ya maeneo mengine.

Na nimependa utaratibu ulikuwa ni mzuri wa wagombea kuhesabu kura wenyewe. Ambapo huu utaratibu unamfanya mgombea kukubali matokeo bila kuleta shinikizo ya kudai kuibiwa kura zake. Na hakutokea mgombe yoyote katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti kukataa matokeo. Walioshindwa walikubali na kuahidi kuwaunga mkono.

Katika baadhi ya Mitaa walikuwa wenyeviti wamedondokea pua mwaka huu katika kura hizo za maoni na mitaa hiyo ni kama ifuatavyo. Msigani, Malamba mawili

Ambapo waliondondokea pua katika kipindi cha miaka 5 walishindwa kufanya na kutimiza majukumu yao ambayo walipaswa pia kuyatimiza kwa mfano Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa katika miaka yote mitano hakuwai kuitisha mikutano ya hadhara na wananchi ambapo inawataka kila baada ya miezi mitatu kuitisha mikutano ili kusikiliza kero na kuzitatua.

Lakini hii yote imetokea na moja ya sababu viongozi wa CCM wa maeneo husika kushindwa kuwakumbusha walichaguliwa kufanya kazi kulikana na Ilani ya chama na mbaya zaidi wengi wao pia katika uchaguzi wa mwaka 2019 walipita bila kupigwa na kupelekea kujisahahu kutimiza wajibu wao kwa wananchi na hii imepelekea wanachama wa CCM kwenye Kata ya Msigani kuwapiga chini Wenyeviti wote waliofeli kuleta maendele kwa wananchi.

Soma Pia: Vurugu zaibuka Uchaguzi wa CCM Kibosha Mkoani Pwani

Lakini za ndani kabisa Kata ya Msigani na mitaa yake kwa miaka mingi CCM imekuwa na Nguvu ila tu wakati mwingine vyama vya upinzani upata nguvu kutoka kwa wanachama wa CCM kwa mfano mgombea aliyeshindwa kupata nafasi katika kura za maoni, basi kama ananguvu ya wananchama anachokifanya anawashawishi wanachama wale ukifika uchaguzi wa nje kwa maana wa vyama vyote basi wampigie mgombea wa chama fulani cha upinzani ili akishinda huyo mgombea wa chama cha upinzani basi yeye na yule alishinda ndani ya chama chake wote wawe wamekosa. Ndiyo ipo hivyo bhana
 
Back
Top Bottom