Ili tufikie malengo chadema tumstaafishe bujoro

ISMAIL MKIMBIZI

Senior Member
Jan 13, 2013
192
23
Siku zote katika miaka ya nyuma nikiwa Masomoni Dar nilisikia sifa nzuri za Mwenyekiti wa CHADEMA Kasulu Bw. Rajabu Bujoro. Nilivorejea Kasulu, nilikuta mambo yamebadilika wanamageuzi wakimtuhumu kuchukua hongo toka kwa Daniel Nsanzugwanko aliyekuwa mbunge wa CCM amsaidie Kampeni 2010. Ni jambo ambalo sikuliamini lakini makamanda walinihakikishia kuwa ni kweli na ndio maana alikuwa akimsema jukwaani kwa kula na kupulizia.

Hivi Karibuni kumetokea uvumi kuwa anahamia CCM, uvumi ambao mimi sikuuamini hata kidogo na baadaye yeye mwenyewe kwenye mkutano wa hadhara akakanusha na kudai CCM wao ndio walimfuata na kumuahidi hongo ya milioni kumi na tano ajiunge nao. Jana CCM wamefanya mkutano wa hadhara na kujibu tuhuma zake. Katika majibu hayo moja ya maelezo ya wanaccm yalinifanya niamini kuwa ni kweli BUJORO alinuia kuhamia CCM mambo yakavurugika.

Akisimulia kisa hicho Katibu Mwenezi wa CCM Kasulu Bw. Masoud Kitowe alisema Bujoro alifanya nao mawasiliano akilaumu amekitumikia CHADEMA kwa muda mrefu bila faida yoyote ".... na kwamba chama hicho kimemkosanisha uelewano na wananchi wa Kasulu,wazee wamemchukia kukamatwa watoto zao na kuwekwa ndani eti wamemtupia mawe Dr Slaa, na vijana wanamchukia sasa chadema ....akatupa masharti ili ajiunge na CCM kuwa tumsaidie kupata tenda Halmashauri.... uchaguzi wa madiwani agombee Kata ya kasulu Mjini ....tulimpa masharti ili apokelewe na kumtimizia hayo kwanza apite kwenye vijiwe vya Kahawa ambapo amekuwa akitufitinisha na wananchi awaeleze kuwa yeye na CHADEMA sasa basi...."

Katika pita pita zangu vyanzo vya habari vya kuaminika vinasema aliwahi kuzungumza hivyo kahawani akilaani kuwa chadema haimsaidii kitu bora ahamie CCM. "... si mara moja sema amekuwa akiongea kijanja sana.." Alisisitiza mzee mmoja mmiliki wa kijiwe cha kahawa. Na habari ya kuilaumu chadema kuwa haimsaidii kitu sana sana inamtia hasara aliwahi kuniambia akasema ni vema hata awanyang'anye nyumba yake iliyofanywa ofisi za wilaya apangishe na akafanya hivyo. Pia aliwahi kuniambia hana ushirikiano mzuri na viongozi wenzake hawamuheshimu ispokuwa katibu wake tu. Na mimi binafsi nikiongea nae nashangaa kuona haishi kumsifia Daniel Nsanzugwango. Hivi karibuni namnukuu, "...Nzanzugwanko akigombea 2015 Kasulu mjini hana mpinzani..." Najiuliza ana nini na Nsanzugwanko? CHADEMA hatuna mgomea mwenye sifa mpaka amfagilie fisadi?

NB: Ni kweli ana kauli mbaya kwa wananchi hasa wenye mtazamo hasi juu ya maoni yake na amekuwa akiwatukana jambo ambalo linapelekea wananchi kumchukia yeye na CHADEMA na ikija habari ya uchaguzi tunaanguka vibaya sana. Ataafishwe uenyekiti, awe mzee mlezi wetu wa chama kama walivyo akina mzee Upendo aachie nafasi walio na uwezo wa kujibu hoja na misimamo hasi kistaarabu. Mwisho niombe radhi kwa kuahidi uzi ungeofuatia ule uliopita ingekuwa diwani wa CUF anavyoichangia CCM michango mbalimbali lakini hii nimeona itangulie.
 
Back
Top Bottom