Ili tuendelee


A

Adili

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2007
Messages
2,588
Likes
633
Points
280
A

Adili

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2007
2,588 633 280
Hapo zamani Mwalimu alibainisha kuwa maendeleo ya taifa letu yalihitaji
a)Watu
b)Ardhi
c)Siasa safi
d)Uongozi bora

Kwa muda wa sasa vipengele c) na d) ni debatable! Hali ya kipengele b) inatisha. Dalili za kutisha zilianzia hapo tulipo anza kumilikisha ardhi kwa wageni tukiwa na nia ya kuwafanya watanzania vibarua/manamba nchini mwao. Hasante Mzee Ruksa, BWM na Mlatino wake na sasa JK kwa kutusogeza huku.
Sheria ya sasa ya ardhi inaonekana kama nzuri lakini mwisho wake itahitimisha kuhamisha umilikaji wa ardhi kutoka kwa mwanakijiji/kijiji kwenda banki na mwisho wake kuishia kwa waliowahi.
Tujitayarishe kuwa manamba maana siku za mgiriki na mkonge ndio zinarudi.
Inawezekanaje tuna uwezo kukopa hela za kujenga National Stadium lakini tunakosa uwezo wa kukopa hela za kuwawezesha wakulima wa Handeni na Muheza waongoze kwa uzalishaji wa matunda?
Tukijua Saudia wanahitaji mchele na ngano na ardhi yetu inafaa kwa kilimo cha hayo, tunashindwaje kukopa ili tuwawezeshe wakulima wetu katika ardhi yetu wazalishe kwa ajiri ya soko hilo?
Mbona tunakopa miaka nenda miaka rudi kugharamia mambo yasiyozalisha?
 
M

Mapinduzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2008
Messages
2,427
Likes
22
Points
0
M

Mapinduzi

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2008
2,427 22 0
Ili tuendelee tunahitaji 'WINTER'
 

Forum statistics

Threads 1,215,647
Members 463,325
Posts 28,555,538