Ili nchi itajirike inahitaji nini hasa?

mbongokazi

Senior Member
Dec 31, 2015
110
23
Ndungu wanajamvi, kilio kikubwa cha nchi zinazoendelea ni umaskini. Wanasiasa wengi wamekuwa wakitoa ahadi lukuki za kufuta au kupunguza umskini kwenye nchi zao, lakini mpaka wanamaliza mihula yao ya uongozi umaskini unabakia pale pale. Hii Inamaana kwamba hili dude linaloitwa umaskini halieleweki zaidi kwa nchi zinazoendelea tu. Je, umaskini ni mini hasa? Je, kunaumskini wa raslimali, IQ ya watu? , Elimu, viwanda, umaskini wa kufikiri kitajiri?

Mwalimu Nyerere ( Hayati) alisema kuwa ili watanzania tuendelee tunahitaji, watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Je, yote haya tunayo na sasa tunaongezea madini. Je , nini hasa kimepungua ili nchi yetu iweze kuondokana na umaskini? Je ,watu wetu wanayo hata Elimu yakusoma na kuandika? Wasojua kusoma na kuandika wamefikia asilimia ngapi sasa? Je , wliosomea Elimu ubunifu ni asilimia ngapi ya watanzania wote? Au Elimu yetu ni ya kutaka kuajiriwa tu hasa kuwa wanasiasa? Tutatokaje hasa kwenye hili dimbwi la umaskini ambalo nchi nyingi zimeshalipiga kikumbo?

Nani alaumiwe mwananchi, mwanasiasa alioko madarakani au wote wawili?

Nani aongoze mwenzake kutoka kwenye ndimbwi hili???

Je tutatoka?????

Kama diyo, kwanjia gani????

Itatuchukua miaka mingapi???

Mwanajamvi karibu tutafakari wote!
 
Back
Top Bottom