ILI MWANADAMU AKAMILIKE LAZIMA APITIE SHIDA

ILI MWANADAMU AKAMILIKE LAZIMA APITIE SHIDA

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
245
Reaction score
314
ILI MWANADAMU AKAMILIKE LAZIMA APITIE SHIDA

Hakuna kitu kinakamilisha ubinadamu kama shida. Ndio maana hata mitume na manabii ilipitia shida ili utume na ubinadamu wao ukamilike. Mungu aliwapa ulofa ili wanyooke. Watu wakawaadhibu watakavyo. Haikuwa bahati mbaya bali ili wakamilike. Ni natural law. Ndio maana dhahabu lazima ipitie kwenye moto. Hata Nabii Adam na Hawa walipoasi walipewa shida ili wakamilike.

Sheria hii ya asili bado inafanya kazi. Jaribu kuwatizama watoto Wa tajiri au Wa masikini jirani yenu. Utaona ukweli huu. Watoto wengi Wa masikini huwa wamekamilika. Watoto wengi wa matajiri huwa mawaa. Hawakamiliki.

Sheria hii ya asili inafanya kazi yake vizuri kwa nchi za dunia ya kwanza. Kwa kukosekana kwa shida watu hawakamiliki ubinadamu wao. Haswa vijana na watoto. Huko kwa wenzetu hakuna kazi ngumu kwa wenzetu kama kulea au kufundisha. Watoto na vijana hawakamiliki.
Hakuna suala linaloonyesha kutokamilika kwa wasio na shida kama haya masuala ya LGBT. Ndio wapo masikini ni LGBT lakini wengi wao ni wafuata mkumbo. Wahusika haswa ni wasio na shida. Ni watu aina ya Waziri Mkuu Wa Luxembourg! MTU toka azaliwe ni RAHA tu. Hajawahi kulala njaa, kuumwa na mbu, kuvuta vumbi, kuchapwa shuleni, etc. Anajitahidi aidha aonje shida au atende jambo litakalomletea maadui. Aonje walau karaha!
Hata nchini Tanzania waliojitokeza waziwazi kutetea ushoga ni walioishi kwa RAHA toka utotoni! NA wanatumia hoja ileile ya waziri mkuu Wa Luxembourg! Haki za ubinadamu!
Wanasahau haki ya MTU inakufa pale inapodhuru haki ya wengine. Hivi wazazi Wa Waziri Mkuu Wa Luxembourg hawana haki ya kuwa na wajukuu? Watawapataje wakati Mtoto kaoa mwanaume mwenzie? Wazazi wake wametamka hadharani hawakubaliani naye Ila wanaheshimu uamuzi wake! Hivi wananchi wrote Wa Luxembourg wanakubali kuongozwa na Basha? Hawa haki yao wataipataje? Hivi Sikh ataamua au ataalikwa kuizuru Tanzania itakuwaje? Tutamkamata 'mkewe' kwa kuwa ushoga ni kosa la jinai Tanzania? Tutamruhusu "mke" Wa Waziri Mkuu Wa Luxembourg aandamane na mke wa raisi wa Tanzania kwenda kutembelea kituo cha watoto yatima? Tutamtambulisha vipi mbele ya watoto wetu?
Tabia hii ya ambao hawajawahi kupata shida tunaiona hata kwenye mavazi. Vijana wa wenzetu wanaitafuta shida! Wanavaa suruali inayowapa shida! Suruali inayowazuia kutembea! Wengine wanatamani ngui zilizo na matobo. Wanatengenezewa nguo mpyaaa lakini ina matobo ili wa test shida! Masikini majuha yetu! na yenyewe unayakuta yameiga! Jitu limezaliwa shida tupu eti nalo lina test shida! Basi na barabara zetu zilivyo mbaya unakuta linatembea kwa shida kwelikweli! Suruali inataka kuanguka kwa njaa ya kweli kweli!
Ndugu sie tumezaliwa kwenye shida tunatakiwa ubinadamu wetu ukamilike. Tuwaache wazungu wa test shida! Hawajakamilika.
Ningetamani siku moja Waziri Mkuu wa Luxembourg na "mkewe" wazuru Tanzania ili tushuhudie ujinga uliokamilika!
 
Kweli nimekuelewa Sana mtoa maada.yote haya vitabu vitakatifu vilieleza kwamba nyakati hizi za mwisho wa mfumo wa mambo ilihitajika mwanadamu apotoke hata ZAIDI kwenye suala la mienendo ya kingono.tupo kipindi cha utimizo wa unabii huo
 
Back
Top Bottom