SoC04 Ili kutunza Mazingira na kuongeza ajira, serikali iweke mashine za recycle kila mtaa au kila kata

Tanzania Tuitakayo competition threads

JOHN MAXWELL

Member
Feb 26, 2024
33
67
Ili kutunza Mazingira na kuongeza ajira ,serikali iweke mashine za recycle kila mtaa au kila kata.

Utangulizi
Jukumu la kutunza mazingira ni langu na ni lako hivyo tunaweza kutumia fursa ya kutunza mazingira kwa kuongeza ajira, hii itafikiwa baada ya kuchakata taka kwa kutumia mashine za recycle ambazo serikali inaweza kuziweka kila mtaa au kila kata.

Ili kuifikia 'Tanzania tuitakayo' lazima tuwe na mazingira safi kila sehemu na tuwe na Miundombinu ya kutufanya tuishi katika Mazingira safi.

Hivyo serikali pamoja na wadau wa mazingira kwa pamoja tunaweza kuifikia Tanzania tuitakayo kwa kuweka Miundombinu ambayo itawezesha kuwepo kwa mashine za uchakataji wa taka katika kila mtaa au katika kila kata.

Zifuatazo ni faida ambazo zitapatikana baada ya uwepo wa mashine za uchakataji wa taka katika kila mtaa au katika kila kata.

1. kuboresha mazingira na kuwa katika mwonekano mzuri, hii itafikiwa baada ya kuwepo mashine za recycle katika eneo husika.

2. kuongezeka kwa ajira, serikali kupitia kuweka mashine za kuchakata taka, kazi ya ukusanyaji wa taka itakuwa kazi rasmi ambayo itakuwa na tija kwa mtu yeyote kuifanya na kujipatia kipato.

3. Kupanua wigo wa fursa katika kada nyinginezo Kama kilimo, mfano baadhi ya taka kama (Garbage) baada recycle huweza kutumika Kama mbolea mashambani.

4. Kuifanya kazi ya ukusanyaji wa taka kuwa na tija, kazi hii imekuwa ikifanywa na watu ambao hutafsirika kuwa wamekata tamaa na Maisha hivyo baadhi ya watu kuogopa kuifanya na kuidharau hii kazi.

5. Kupunguza athari kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko, kupitia kuwepo kwa mashine za uchakataji taka katika kila mtaa au kila kata serikali itaweza kupunguza athari za magonjwa ya mlipuko Kama , kipindupindu n.k.

Serikali inaweza kufanya mambo yafuatayo ili kuifikia hii hatua ya uwepo wa mashine za uchakataji taka kila kata au kila mtaa.

1. Kuwashirikisha wadau wa mazingira kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa mashine za uchakataji taka katika maeneo yote nchini ili kulinda na kutunza mazingira.

2. Kutoa Elimu kupitia majukwaa mbali mbali ili kuwafanya watu kitambua kuwa taka sasa ni fursa.

3. Kuunganisha ushirika kati ya wawekezaji na serikali, ambao watapenda kuwekeza katika uwekaji wa mashine za uchakataji taka.

Hitimisho

Hapa nchini zimekuwepo mashine za uchakataji wa taka Ila kuhusu taka ambazo huitwa garbage bado hazipo kwa wingi na mitaani uchafu unaosumbua ndo huo huitwa garbage hivyo naomba wazo hili likawe la ukombozi wa kuhakisha tunaifikia Tanzania tuitakayo ikiwa katika mazingira safi na salama yenye kumfanya kila mtu kuishi kwa furaha.
 

Attachments

  • Screenshot_20240509-083110_1715232885001.jpg
    Screenshot_20240509-083110_1715232885001.jpg
    222.3 KB · Views: 2
  • Screenshot_20240509-082831_1715232914315.jpg
    Screenshot_20240509-082831_1715232914315.jpg
    165.5 KB · Views: 2
Nimekupigia kura kwa sababu tunafanana mawazo linapokuja suala la usafi wa mazingira. Ninachukizwa kupita maelezo na uholela wa takataka mitaani. Ninatamani siku moja nianzishe uzi humu wa kukutanisha wadau wenye mawazo ya namna tunaweza kuja na suluhu ya kudumu ya waste management tukianza na Dar es Salaam.
 
Nimekupigia kura kwa sababu tunafanana mawazo linapokuja suala la usafi wa mazingira. Ninachukizwa kupita maelezo na uholela wa takataka mitaani. Ninatamani siku moja nianzishe uzi humu wa kukutanisha wadau wenye mawazo ya namna tunaweza kuja na suluhu ya kudumu ya waste management tukianza na Dar es Salaam.
Hakika mkuu upo sahihi Sana .
 
Sawa kabisa, tunahitaji mipango kama hii kuboresha udhibiti wa taka mitaani.

Kuna maeneo mfano Mbeya kulikuwepo na madampo, yakaachwa ukabaki mpango wa magari ya taka lakini kinachendelea sasa hivi baadhi ya maeneo huduma ya taka imebaki binafsi bila mifumo.

Kuchakata tena taka kutasaidia sana kupunguza athari za kutupwa taka kiholela
 
Back
Top Bottom