Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Huwa kila nikiamka nafatakari sana juu ya hatima ya Tanzania na suala zima la uongozi na usalama wa nchi yetu. Kuna mambo makubwa yanatokea lakini tunajifanya kama hatuyaoni na hatutaki hata yajadiriwe kwa kina. Tunakuwa kama mbuni ambaye anadhani amefisha aibu ya makalio yake yaliyo wazi kwa kufukia kichwa kwenye mchanga, na katika kufanya hivyo anainama na kuyafanya makalio yake yaliyo wazi kuonekana hata zaidi!
Hebu tujiulize, hivi kweli Tanzania tumefikia hatua ambapo tunaona haya matukio makubwa yanayotia shaka uongozi bora, amani na utulivu wa nchi yetu kuwa si ya msingi sana?
Hebu tujiulize, hivi kweli Tanzania tumefikia hatua ambapo tunaona haya matukio makubwa yanayotia shaka uongozi bora, amani na utulivu wa nchi yetu kuwa si ya msingi sana?
- Suala la katiba lililozikwa kimya kimya kwa utashi binafsi wa Raisi tofauti na utashi wa mamilioni ya wananchi wa Tanzania
- Suala la kikundi cha utekaji na mauaji cha "wasiojulikana" ambao hadi sasa kusema hatujui ni nani ni katika kujifanya hatuelewi ukwel wa mambo
- Suala la ubabe na uonevu dhidi ya wabunge wa upinzani bungeni, ambao wapo kikatiba kama wawakilishi wa sehemu ya wananchi wa Tanzania
- Suala la upendeleo wa wazi wa wilaya ya Chato anakotoka Raisi wetu katika mipango ya maendeleo na matumizi ya fedha za taifa kwa ujumla nje ya taratibu za Bunge
- Suala la ukiukwaji wa katiba ya nchi katika shughuli za vyama vya siasa nchini
- Suala la uminywaji wa haki za binadamu kutia ndani na udhibiti usio haki wa vyombo vya habari na uhuru wa kutoa maoni
- Suala la kuporomoka kwa biashara kubwa na ndogo nchini kutogona na maamuzi yasiyo na hekima
- Suala la jeshi la polisi kutumika kama chombo cha chama tawala mara kwa mara
- Suala la Jeshi la Wananchi kujiingiza katika mambo ya usalama wa ndani ya Tanzania kwa kutoa matamko na kauli ambaz sio wajibu wao, na hata kutishia wakati fulani kuchukua silaha dhidi ya wananchi wa Tanzania katika tishio la maandamano ya nchi nzima
- Suala la migongano ya mara kwa mara na balozi za nje na taasisi za kimataifa kutia ndani Ofisi ya Umoja wa Mataifa, Benki ya Dunia, Jumuiya ya Nchi za Ulaya nk