Elections 2010 Ili Dr.Slaa ashinde tunatakiwa kufanya hivi...

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Natamani sana Jumapili ijayo, yaani 31/10/2010iwe siku ya mwisho kwa Jakaya Mrisho Kiwete kuwa Rais.

Lakini ili tufike huko inabidi tufanye mambo yafuatayo ili Dr.Slaa amshinde Kikwete na awe Rais wetu wa tano.

1. Tuwatumie Meseji za simu wale wote tunaowafahamu na kuwaeleza umuhimu wa kumchagua Dr.Slaa.

2. Sisi wenyewe siku ya kupiga kura tuwe wa kwanza kwenda kupiga kura na kuhakikisha wale wote wanaostahili kupiga kura kwenye maeneo yetu nao pia wanapiga kura kwa Dr.Slaa.

3. Tujitolee kuwa mawakala kwenye maeneo tunayoishi ili tuweze kulinda kura zetu tukutufu zisiibwe na mafisadi.

4. Sisi wenye asili ya vijijini tuwasiliane na ndugu zetu walio vijijini ili nao pia wamchague Dr.Slaa na wajitolee kuwa mawakala.Kwani naamini vijiji vingi sana hapa Tanzania kwa sasa vina mawasiliano ya Simu.

5. Tuwashawishi Dada, mama, wake, girl friends, watalaka wetu, shangazi zetu na wanawake wote ambao ndiyo mtaji mkubwa wa CCM kumchagua Dr. Slaa.

Mwisho kabisa tusiwachekee CCM kwani kwa methali zetu waswahili "Ukicheka na Nyani utavuna mabua"

Solidarity Forever!!?
 
Back
Top Bottom