Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini hapa jana alisema tukio hilo lilitokea Januari 11 mwaka huu saa 4 asubuhi
Alisema Joyce alikamatwa na polisi baada ya kumpiga fimbo mtoto wake huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu sehemu mbalimbali za mwili na kusababishia kifo chake, kitendo ambacho ni kosa la jinai
Kamanda Msangi alisema siku ya tukio, mtoto huyo alimkatalia mama yake kwenda shule na kusema hataki shule tena, ndipo mama huyo alipopatwa na hasira na kuanza kumpiga fimbo sehemu mbalimbali za mwili na kusababishia kifo muda mfupi baadaye
Alisema baada ya mtoto huyo kufa, wananchi waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi na polisi walifika mapema kwenye eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa
"Mtuhumiwa yupo katika mahojiano na polisi, pindi uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani, mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na timu ya Madaktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure na tayari umekabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya maziko".alisema
Kufuatia tukio hilo la kusikitisha, Kamanda Msangi ametoa wito kwa wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema na nidhamu kwa kuwaelimisha mambo mazuri na mabaya ili kuepusha kutoa adhabu za vipigo kwa watoto kwa kujenga familia bora isiyo na ukatili.
Chanzo : HabariLeo