Ile issue ya TAKUKURU dhidi ya mama sita imeishia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ile issue ya TAKUKURU dhidi ya mama sita imeishia wapi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Anold, Aug 17, 2010.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Wiki kadhaa zilizopita tuliambiwa na TAKUKURU kuwa wamemdaka mama sita katika mazingira ya kutaka kutoa rushwa, hata vivyo mama sita pamoja na mzee sita walipinga vikali na kuielezea jamii kuwa hizo ni njama tu na hakukuwa na kitu cha namna hiyo. TAKUKURU kwa masikio yangu nilisikia wakitoa tamko kuwa wao wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na hawawezi kumuonea mtu yeyote pia hawajali cheo au nafasi ya mtu hivyo kutuhakikishia kuwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili Mama sita zilikuwa ni za kweli. Kitu ambacho kinanishangaza ni kimya ambacho kimetanda kuhusiana na suala hilo, sipati jawabu na kichwa changu kimegeuka bunge dogo ambalo kila wakati linaibua hoja na muda wote nimeshindwa kujua au kupata jawabu sahihi dhidi ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili mama sita. sielewi kuwa TAKUKURU wamechunguza na kubaini ukweli kiasi cha kujiridhisha kimyakimya au imekuwaje, mkwala waliopiga TAKUKURU ulikuwa mkubwa na walitueleza kuwa wana uhakika na ushahidi juu ya tuhuma na kwamba kama mama sita anadai anaonewa ataieleza mahakama. Nashindwa kujua mkwamo uko wapi? mbona muda unakwenda hakuna lolote ni uchunguzi gani huo TAKUKURU wanaufanya wakati walijagamba kuwa walimdaka mama sita live? sitaki niamini kuwa mama sita alibambikiziwa tuhuma. sitaki niamini kuwa mama sita amedhalilishwa, amesikitishwa na kuvunjiwa heshima kwa makusudi na TAKUKURU,sitaki niamini kuwa TAKUKURU wamepigwa stop kushughulikia suala hili, ninachotaka niamini ni kuona kauli za TAKUKURU zinafanywa kwa vitendo. Kama ilikosea au kuelekezwa vibaya basi imsafishe mama sita!! haiwezekani jambo hili walimalizie hewani, huku ni kumharibia mama huyu mwenye heshima zake. Inawezekana TAKUKURU walimsafisha sijasikia, naomba kama kuna mweye A-Z ya ishue hii anifahamishe ili suala hili nilitoe kichwani nishughulikie maswali mengine ambayo bado ni utata mtupu kuhusiana na siasa hizi tunazoshuduhudia kipindi hiki.Naomba kuwasilisha.
   
Loading...