Ilani za Uchaguzi zinakosa mambo mengi ya msingi

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
Nimetumia muda kusoma ilani ya Uchaguzi ya CCM, sio kwa ubaya lakini nawaza inakuwaje kama mtu unakuwa na maswali dhidi ya utekelezaji wa Ilani. Maana kikubwa kilichopo ni ahadi za kuleta ajira, kukuza utalii na kuongeza mikopo nk. Lakini mambo yote haya hayajaweka ni kwa namna gani vitu hivi vitatimizwa.

Mathalani, suala la kujenga barabara haijaweka hizo hela zitapatikana wapi? Je ni wananchi watatozwa kodi zaidi au tutakopa zaidi na vizazi vije vilipe hela hizo kwa kodi kubwa. Aidha masuala ya utu hayajatafsiriwa kwamba hiyo "kazi na utu" utu unakuzwaje?

Ahadi nyingi zilizoweka hazijaweka gap, kwamba uhitaji ukoje, changamoto ni nini na itataliwaje. Bali imewekwa tu tutajenga barabara, tutajenga madarasa na hospitali.

Yote hii inarudi kwenye msingi wa kukosa falsafa ya kutimiza ahadi hizi. Yaani CCM akisema anajenga Barabara, na ACT akasema anajenga barabara, wananchi wanawezaje kuichagua ilani husika ikiwa haiko wazi kwenye mpango wa kutimiza mambo yaliyoahidiwa. Hapo ndipo unapokuta utapeli.

Nadhani vyama ambavyo havijatoa ilani vijikite kwenye kuonesha gap lililopo na namna watakayotumia kutatua changamoto zilizopo badala ya kuweka ahadi bila kuwa na mpango wa namna gani ahadi hizo zitatimizwa.

Nawasilisha.
 
Ilani ni danganya toto tu hakuna kitu hapo.

Kutekeleza yote au baadhi ya yaliyomo kwenye Ilani ni utashi wa Rais na si vinginenyo....

Ingekuwa Ilani ni Ilani kweli Tanzania sasa hivi isingekuwa na tatizo la ajira maana Ilani ya CCM ya 2020-2025 ilisema itatengeneza ajira milioni 8. ZIKO WAPI ?

ILANI NI KUWARUBINI TU WATANZANIA.
 
Nimetumia muda kusoma ilani ya Uchaguzi ya CCM, sio kwa ubaya lakini nawaza inakuwaje kama mtu unakuwa na maswali dhidi ya utekelezaji wa Ilani. Maana kikubwa kilichopo ni ahadi za kuleta ajira, kukuza utalii na kuongeza mikopo nk. Lakini mambo yote haya hayajaweka ni kwa namna gani vitu hivi vitatimizwa.

Mathalani, suala la kujenga barabara haijaweka hizo hela zitapatikana wapi? Je ni wananchi watatozwa kodi zaidi au tutakopa zaidi na vizazi vije vilipe hela hizo kwa kodi kubwa. Aidha masuala ya utu hayajatafsiriwa kwamba hiyo "kazi na utu" utu unakuzwaje?

Ahadi nyingi zilizoweka hazijaweka gap, kwamba uhitaji ukoje, changamoto ni nini na itataliwaje. Bali imewekwa tu tutajenga barabara, tutajenga madarasa na hospitali.

Yote hii inarudi kwenye msingi wa kukosa falsafa ya kutimiza ahadi hizi. Yaani CCM akisema anajenga Barabara, na ACT akasema anajenga barabara, wananchi wanawezaje kuichagua ilani husika ikiwa haiko wazi kwenye mpango wa kutimiza mambo yaliyoahidiwa. Hapo ndipo unapokuta utapeli.

Nadhani vyama ambavyo havijatoa ilani vijikite kwenye kuonesha gap lililopo na namna watakayotumia kutatua changamoto zilizopo badala ya kuweka ahadi bila kuwa na mpango wa namna gani ahadi hizo zitatimizwa.

Nawasilisha.
unadhani wazee wa kuchota wanaelewa hii...kapige kura urudi gengeni nawe uokoteokote miambili ya ugali
 
Ilani haonyeshi waliyopanga 2020 yaligharimu kiasi gani, changamoto walizopata nafasi za kugombea kinsi watajavyo fanikisha ilani hii.
 
Nimetumia muda kusoma ilani ya Uchaguzi ya CCM, sio kwa ubaya lakini nawaza inakuwaje kama mtu unakuwa na maswali dhidi ya utekelezaji wa Ilani. Maana kikubwa kilichopo ni ahadi za kuleta ajira, kukuza utalii na kuongeza mikopo nk. Lakini mambo yote haya hayajaweka ni kwa namna gani vitu hivi vitatimizwa.

Mathalani, suala la kujenga barabara haijaweka hizo hela zitapatikana wapi? Je ni wananchi watatozwa kodi zaidi au tutakopa zaidi na vizazi vije vilipe hela hizo kwa kodi kubwa. Aidha masuala ya utu hayajatafsiriwa kwamba hiyo "kazi na utu" utu unakuzwaje?

Ahadi nyingi zilizoweka hazijaweka gap, kwamba uhitaji ukoje, changamoto ni nini na itataliwaje. Bali imewekwa tu tutajenga barabara, tutajenga madarasa na hospitali.

Yote hii inarudi kwenye msingi wa kukosa falsafa ya kutimiza ahadi hizi. Yaani CCM akisema anajenga Barabara, na ACT akasema anajenga barabara, wananchi wanawezaje kuichagua ilani husika ikiwa haiko wazi kwenye mpango wa kutimiza mambo yaliyoahidiwa. Hapo ndipo unapokuta utapeli.

Nadhani vyama ambavyo havijatoa ilani vijikite kwenye kuonesha gap lililopo na namna watakayotumia kutatua changamoto zilizopo badala ya kuweka ahadi bila kuwa na mpango wa namna gani ahadi hizo zitatimizwa.

Nawasilisha.
Ilani siyo mpango wa maendeleo! Ilani ni muhtasari wa sera na dira ya maendeleo!
 
Back
Top Bottom