Ikulu yanuka ukabila?


Iringa ni kabila ama mkoa?Iringa kuna wahehe,wabena nk....Kwahiyo weka wazi kama ni upendeleo wa aina gani,kama wote waliopendelewa ni wahehe,ama wote ni wabena,then hilo linakuwa ni ukabila moja kwa moja.Kama waliopendelewa ni mchanganyiko wa makabila hayo,basi huo ni upendeleo based on mkoa wanaotoka na hapo si ukabila moja kwa moja.
 
Upuuzi mtupu! magazeti ya Bongo jamani tafran tupu. Sasa ikiwa hawa wafanyakazi Ikulu ni watu kutoka Iringa inahusiana vipi na Ukabila yaani mtu akitoka Iringa basi lazima awe ni kabila fulani linaloleta Ukabila!

Mkandara.. ndio maana wakati fulani nilihoji ukabila ni nini hasa? Kwenye mawazo ya watu wengi (kama inavyoonekana kwenye MwahaHalisi) ukabila ni Idadi! NI sawa kabisa na wale wanaoenda TRA na kukuta wachagga wakadai ni ukabila, wakaenda JWTZ na kukuta kuna wakurya wengi watasema ukabila na wakienda Mwanza, na kukuta wasukuma wengi kwenye ofisi mbalimbali wakasema ni ukabila, Ukabila ni vitendo vya kupendelea au kutoa fursa ya upendeleo kwa watu wa kabila lako huku ukipuuzia makabila mengine. Kwa mfano kwenye mada hiyo hatujui ratio ya watu wa mikoa mingine in relation to hao wa Iringa.

pointi umeitoa nzuri siyo wote wanaotoka Iringa ni Wahehe au Wabena..
 
Possibly those figures in red were typed wrongly, siamini kama hakukuwa na typing error......ila kama ni kweli hasa ile ya Dolari 11,000 basi kweli Maisha Bora kwa kila Mtanzania yanawezekana.

Sasa ndo naamini Mshauri Mkuu wa Ikulu (yupo Back office) LAZIMA atakuwa huyu hapa

 
Hivi kama kweli NHC watamlipa $11000 kwa mwezi huyu mtu ,is this GOOD VALUE FOR MON
Kama ni private company hapa sawa,lakini kama NHC iko chini ya serikali ,this is really stupidity!
 
Mpaka karne hii jamani bado tunaongelea ukabila...tutafika? mbona kama tunarudi nyuma
 
Mpaka karne hii jamani bado tunaongelea ukabila...tutafika? mbona kama tunarudi nyuma
Kama Ukabila upo usiongelewe? Mi nadhani the best way to abolish this stupidity ni kuwaweka hadharani wote wenye vitabia tabia kama hivi vya ukabila. Kama ambavyo tunafanya kwa majambazi, wala rushwa, wasambaza ukimwi kwa makusudi na wengineo. Unapoukalia kimya eti kwa kuhofia utaambiwa unarudi nyuma ni kutokujua wajibu wako.
 
Hivi kama kweli NHC watamlipa $11000 kwa mwezi huyu mtu ,is this GOOD VALUE FOR MON
Kama ni private company hapa sawa,lakini kama NHC iko chini ya serikali ,this is really stupidity!


It is not stupidity kumlipa hivyo kama kweli shirika lina tija. ILO ilifanya tahimini tanzania wafanyakazi inatakiwa walipwe at least laki 5 kama sikosei.


Tujiulize KCC hapo NHC wanalipwa shilinngi ngapi? na je kwa nini wasilipwe zinazowatsoha kwa level yao.Kuliko kulalamika Nehemia anapata mshahara mmkubwa tulamikie wa KCC wanaopata mdogo.
 
Kama hao watu wanasifa zinazofaa na wanachapa kazi vizuri tatizo lipo wapi?
 


Naomba niongezee hii Definition ya M. Mwanakijiji:
Ukabila ni vitendoi vya kupendelea au kutoa fursa ya upendeleo kwa watu wa kabila lako wasiokuwa na uwezo huku ukipuuzia watu wa makabila mengine wenye uwezo.

Nimeongeza maneno machache ili kuiimarisha zaidi maana ya ukabila. Mimi ukiniambia kuwa wasukuma au wamasai ndio wazuri katika kusimamia mradi fulani na taifa likapiga hatua, sitakuwa na shida hata kama shirika lote litakuwa na wasukuma au wamasai watupu.

Kwa miaka mingi Jeshi letu la wananchi limekuwa na watu wengi kutoka mkoa wa Mara na limeendelea kuwa na nidhamu ya hali ya juu. Ukiniuliza mimi juu ya ukabila jeshini nitakuona una wendawazimu. kuna tatizo gani? Uwezo wanao na hakuna wengine wameonyesha uwezo wakaacha kupewa nafasi.

Ukabila wa siku hizi.
Ni mtandao, kila anayepata nafasi anataka aweke watu wake sehemu nyeti hata kama hawana uwezo. Matokeo ni nchi kwenda mrama kwenye kila idara. Matatizo yote tunayoyaona leo ni mtandao, hakuna ambaye yuko tayari kumkemea mwana mtandao mwenzake, kumfukuza mwanamtanadao mwenzake, kumkaripia mwanamtandao mwenzake, sasa tatizo liko mpaka kwenye vyombo muhimu kabisa katika uendeshaji wa nchi. UKABILA WA MTANDO NDIO UKABILA MBAYA KABISA KWA NCHI YETU KWA SASA. unauwa uwajibikaji na kuleta kujipendekeza.
 

Atayepata kazi hiyo malipo ni usd131,000/year=Tsh170, 000,000/year. Hivyo basi Price water kulipwa million82 utaona ni fair kabisa kwa kulingana na hiyo hadhi ya watu wanaowasahili.
Hata hivyo nashangaa kwa nini mishara yetu ipo juu kiasi hicho na bado hilo ni shirika la umma.
 

Naona huna points za kutetea hoja yako. Hata kama Kubenea ni muongo, hapo amepanga matukio kama inavyotakiwa na kamuweka wazi Luhanjo.

Muokoe kwa kutumia points. Usieme huyu mchapa kazi yule ni kijana na ... so what? procedure hazikufuatwa, period.

Luhanjo amecheza mara nyingi rafu za aina hii. faida kwake ni udhaifu wa serikali tu lakini kama si hivyo, he is no useful to this country. Mpeni ubunge maana nasikia anautafuta.
 

1. Naunga mkono wanaosema Iringa sio kabila ni Mkoa Mkubwa tu na una makabila mengi, kuna Wahehe, Wazungwa, Wabena, Wawanji, Wakinga, nk nk nk.
2. ni ratio ipi ya ku justfy kuwa Ikulu imejaa watu wa Iringa? 80% impossible!

hili tatizo la kuongelea ukabila linaturudisha nyuma sana. linaleta maana kama mhusika hawezi kazi aliyopewa na kuwa aliingizwa kwa kubebwa. Ila kama mtu aliomba mwenyewe na ana vyeti? na anaiweza kazi inakuwaje anahusishwa na ukabila?? hivyo utafiti ufanyike na si mtu kuamka tu na kubwabwaja.

ukabila?? ukabila?? ukabila??
BADO TUNAONGELEA UKABILA MPAKA MIAKA HII YA LEO
wenzetu wanakimbia sie tunarudi nyuma
 
Sioni kosa kama watu wame qualify kufanya kazi hizo Ikulu.Tukumbuke pia kwa jinsi ilivyo TZ leo, kuna makundi mengi ambayo interest zao zinapoonekana kukwama wanatafuta jinsi ya kuwatengenezea wapinzani wao skandali.
What is important ni kuangalia kila habari katika dimensions zote, hata ikibidi three dimensions ili kuwa na uhakika kujua ukweli.
 
Na Saed Kubenea

“I will not talk with you for anything (Sitazungumza lolote na wewe).”
Source: Mwanahalisi, Issue No 181
tehetehe......!1!
hahahahaha........!!!
haaaaaaaaaaah!!!!
Mambo ya ung'eng'e wa KMK! Bora kiswahili kitumike kufundisha tu
 
Jina lako wala haliendani na hoja ulizozijenga hapa natamani jina lako lingekuwa udaku badala ya kuwa facts. Ikulu imetukana tusi gani katika hizo rangi ulizoweka? Hao wote waliopo kwenye hizo nafasi umewaassess ukagundua hawana qualification? Umeangalia vyeti vyao ukaona kwamba hawakustahili kuwa huko. Tuache kuleta hoja zisizo na msingi bwana, hangaika na wewe tengeneza CV yako nzuri, ukaombe kazi Ikulu. Bila shaka utapata, siyo kujiingiza kwenye malumbano ya kidaku kama ya Kubenea.
 
Hivi ni hoja gani aliyoijenga Kubenea inayoonyesha kwamba Luhanjo ameshiriki kuweka watu Ikulu? Wewe umeisoma hiyo habari na kuielewa? Luhanjo ameshiriki kumfanikisha Mfugale apate tenda ya kuendesha hotel milenium tower sasa huko ni Ikulu? Ni wapi Kubenea amethibitisha kwamba kuna mfanyakazi wa Ikulu yupo pale kwa sababu ya Luhanjo? Au ni mahali gani panaposema Luhanjo ndo amemteua Mkurugenzi wa NHC. Huu ndo wehu tunaousema siku zote?? Wewe unajenga hoja kutokea wapi? Au unaangalia tu kichwa cha habari ambacho kinaonyesha kabisa kimeandikwa kisiasa na kwa fitina? Huyu Kubenea sasa hivi keshapoteza mwelekeo, anafaa sasa kuandika habari kwenye magazeti ya uwazi, ijumaa na risasi.
 

Tunahitaji kweli mabadiliko lakini mabadiliko yasiyofata taratibu ni uhuni ambao hauwezi kuvumilika.Kabla ya kuanza kumtetea huyo CEO mpya wa NHC ni nzuri ungejua hao wengine waliopigwa chini wanauzoefu na elimu ya kiwango gani.Tusipende kutetea vitu kwa sababu vinahusu vijana!
 

Ebu fikiri wewe....yaani elimu hizo wanazo watu toka Iringa tu nchi hii....yaani watu toka Iringa ndo wana-CV nzuri....ebu kuwa serious.Yaani kwa mfano TRA inapokuwa na wachaga kuanzia juu mpaka mtendaji wa kawaida kabisa tuseme nini.....yaani kuwa hao ndo watu pekee wanaostahili kufanya kazi TRA au ndo wao wanakuwa wanajua majibu ya interviews zote in advance?

Kwanini hiwe kwa Luhanjo....mbona nafasi hiyo hiyo alikuwa nayo Lumbanga,Rupi mbona hapakuwa na malalamiko hayo.Penye moshi........lisemwalo.....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…