Manyerere Jackton
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 2,438
- 4,463
Hivi kwani hao watu walioondolewa hizo nafasi waliandikiwa na Mungu kwamba ni zao tu?? Kuna watanzania wengine wanaweza kujaza nafasi hizo tusing'ang'anie watu na kukuza mambo yasiyo na tija kwa wananchi. Uwajibikaji na uwajibishwaji ni jambo la kawaida, tatizo limetokea wakiwa kwenye nyadhifa hizo na kujiuzulu au kubadilishwa vitengo ni mojawapo ya uwajibikaji. Kama wametolewa sio issue. Waziri mkuu wa Korea kusini kajiuzulu baada ya kivuko kuzama sembuse hawa wakurugenzi wa maliasili Tz?? Nini tunataka???
Wana jf, salaam. Waziri wa maliasili na utalii, lazaro nyalandu ameshinda vita. Kwa ghiliba na ushawishi wenye nguvu zisizo kifani, amefanikiwa kuwabadili mawazo wakuu wa ikulu akiwamo katibu mkuu kiongozi. Kwa nguvu hizo, profesa songorwa na profesa kidegesho sasa wanahamishwa wizarani na kupelekwa katika taasisi mbalimbali. Juzi, katibu mkuu kiongozi alimuita nyalandu na wakakamilisha mpango huo. Nyakandu amewaandaa watu wake ili bajeti yake ikwamishwe ktk bunge. Wanaotajwa kusimamia mpango huo ni wabunge wanne. Lengo lao ni kuhoji kwanini maazimio ya bunge yamepuuzwa kwa maprofesa kurejeshwa wizarani. Wanaotajwa ni lugora, lembeli, shelukindo (keshajilipua), sendeka na ndugai. Nchi hii imekufa! Wanaodai uraia wa nchi mbili wameona mbali. Nguvu za pesa zimeshinda.
Nilipanga nisichangie baada ya kusoma mawazo pevu ya Mgalanjuka (hapa chini). Ila niongeze kwa kushangaa kwanini hiyo iwe issue ya wewe kuikuza kiasi hicho. Kama unadhani hao Maprofessor ni wadilifu sana na wachapakazi mahiri (na nakubaliana na wewe-inawezekana); please come out of the box na uamini kwamba kuna Watanzania wengine wengi sana wenye hizo sifa, na kuzidi. Usikuze mambo ya kawaida kiasi cha kitaja kwa kufikirika "vita ya pesa" bila takwimu, kithibitisho, wala kielelezo. Watakie kila la Kheri hao Ma-Professor katika majukumu yao mapya. Nchi itaendelea kuwepo na nyumbu wataendelea kwenda maasai Mara na kurudi serengeti, nothing strange will happen.....
Sawa tu nyie ongeeni as if mnajua muongeacho
Hivi kwani hao watu walioondolewa hizo nafasi waliandikiwa na Mungu kwamba ni zao tu?? Kuna watanzania wengine wanaweza kujaza nafasi hizo tusing'ang'anie watu na kukuza mambo yasiyo na tija kwa wananchi. Uwajibikaji na uwajibishwaji ni jambo la kawaida, tatizo limetokea wakiwa kwenye nyadhifa hizo na kujiuzulu au kubadilishwa vitengo ni mojawapo ya uwajibikaji. Kama wametolewa sio issue. Waziri mkuu wa Korea kusini kajiuzulu baada ya kivuko kuzama sembuse hawa wakurugenzi wa maliasili Tz?? Nini tunataka???
Hii ngoma huijui mjomb kaa kimya tu!
mkuu, wakati mambo
yanaharibika hata nyalandu alikuwepo na alikuwa pamoja na waziri
aliejiuzulu. Sasa kwa mantiki yako wotewanatakiwa watoke!
Sawa tu nyie ongeeni as if mnajua muongeacho