Ikulu yakanusha tuhuma ya Rais Magufuli kupunguza ulinzi kwa marais wastaafu

pierre buyoya

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
476
163
Baada ya kuchapisha gazeti lenye kichwa cha habari "RAIS MAGUFULI AWAPUNGUZIA ULINZI MARAIS WASTAAFU" Serekali imewataka Jambo leo kukanusha Taarifa hizo haraka kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa . . .

3c360316fddbd9a89b1a695e5283e422.jpg

====================

Update;

Ikulu yakanusha habari hii

============

Gazeti la JAMBOLEO, toleo namba 2381 la tarehe 15 Machi, 2016 limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho "Magufuli awapunguzia ulinzi marais wastaafu". Taarifa yake kamili ipo katika ukurasa wa nne, na inaeleza kuwa Mheshimiwa Rais John Magufuli amewapunguzia ulinzi Marais wastaafu na imewataja marais hao kuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.

Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa taarifa hizo sio za kweli na inalitaka gazeti hilo kukanusha habari hiyo mara moja, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha, Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa utaratibu wa ulinzi wa Marais wastaafu haujabadilishwa.
8cd529ec016959c962bdacde6d7da3b5.jpg
 
Screenshot (25).png
 
Sasa haieleweki
Gazeti ni la Rizwan au Juma Pinto au Yusuf Manji?

Kwa nini wananchi na wasomaji hawaambiwi ownership, management na structure ya gazeti ikoje?

Baada ya mani kulinunua tutegemee editorial yenye mlengo upi?
 
Back
Top Bottom