IKULU: Waziri Mkuu Mstaafu, Lowassa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli; akiri Rais anafanya kazi nzuri

Ngoyai ni mtu mzima sasa, Mzee mwenye busara zake. Kuna kosa gani kwenda upande wa pili kujulia khali? Siasa sio uadui. Pili mimi binafsi naamini hatua hii itasaidia kupunguza tensions za kisiasa. Ngoyai kaweka utaifa mbele, sio uchama wala ukanda. Tunahitaji viongozi wenye vision kama mzee huyu . hatuhitaji watu wenye short sight syndrome kama Hao wanao laumu laumu kila kitu.
nani kaleta hiyo tension?

kinacholaumiwa hukioni!!
 
Inabidi awe mkweli na akubali kosa lake la kumkaribisha huyu.

Mbowe hawezi kuongoza Kikao cha Kamati kuu Chenye kuazimia kumfukuza Lowassa

Anajua wakimjadili Lowassa kumfukuza kuna Watu watataka kujadili alikujaje ghafla na kupewa fursa ya kugombea, hapo Mbowe hatochomoka
 
Mbowe hawezi kuongoza Kikao cha Kamati kuu Chenye kuazimia kumfukuza Lowassa

Anajua wakimjadili Lowassa kumfukuza kuna Watu watataka kujadili alikujaje ghafla na kupewa fursa ya kugombea, hapo Mbowe hatochomoka
Bashite lowassa hafukuzwi bali atawekwa grade ya shibuda ha ha ha
 
Ngoyai ni mtu mzima sasa, Mzee mwenye busara zake. Kuna kosa gani kwenda upande wa pili kujulia khali? Siasa sio uadui. Pili mimi binafsi naamini hatua hii itasaidia kupunguza tensions za kisiasa. Ngoyai kaweka utaifa mbele, sio uchama wala ukanda. Tunahitaji viongozi wenye vision kama mzee huyu . hatuhitaji watu wenye short sight syndrome kama Hao wanao laumu laumu kila kitu.
Ameamua kwenda kwa mafisadi menziwe hana utaifa zaidi ya tumbo lake
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa ametembelea Ikulu na kuonana na Rais Magufuli leo hii. Mh. Lowassa amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu 5.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 09 Januari, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Edward Ngoyai Lowassa amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na ametaja baadhi ya maeneo ambayo kazi kubwa imefanyika kuwa ni kutoa elimu bila malipo, ujenzi wa mradi wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), ujenzi wa viwanda na ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambavyo vinazalisha ajira nyingi kwa Watanzania.

“Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo.

“Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira, na kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira, Stiegler;s Gorge ni kujenga ajira na mingine ya aina hiyo, lazima kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba tunajenga ajira, jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha elimu katika mambo yako unayofanya, hili nalo lazima lisemwe vya kutosha, kwa kweli nakushukuru Mhe. Rais, you made my day” amesema Mhe. Lowassa.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Edward Ngoyai Lowassa kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali na amesema Mhe. Lowassa ni mmoja wa viongozi ambaye kwa wakati wake ametoa mchango wake katika nchi.

Mhe. Rais Magufuli ameongeza kuwa Mhe. Lowassa ni mwanasiasa mzuri kwani hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita ambao naye aligombea kiti cha Urais, hakuwahi kumtukana.

“Mhe. Lowassa ameniomba mara nyingi nikutane nae, na leo nimekutana nae, tumezungumza mambo mengi, ameniambia ya kwake na mimi nimemwambia ya kwangu, kwa ujumla Mhe. Lowassa ni mwanasiasa mzuri na tuendelee kuwaenzi wazee hawa ambao kwa nyakati fulani walifanya mambo mazuri, na mimi napenda kumpongeza Mhe. Lowassa ambaye kama alivyosema hapa kuwa tumefanya mambo mazuri mengi.

“Ametaja miradi mbalimbali tunayotekeleza, ametaja mradi wa Stiegler’s Gorge utakaogharimu zaidi ya Shilingi Trilioni 7, amezungumzia juu ya elimu bure, amezungumzia juu ya maji ambayo kwa bahati nzuri yeye alikuwa Waziri wa Maji na anafahamu sasa tumefikia wapi, amezungumza juu ya umeme tulivyosambaza katika vijiji mbalimbali, elimu bure, huduma za hospitali na mengine” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

09 Januari, 2018




Aaaahahahahahahahah Angekuwa Sio Lowasa utasikia amenunuliwa aaaaahhahahaha kweli siasa mchezo wake hautaji hasira
 
Punguza hasira BAK please! hajatangaza kuhama
Sasa atampongezaje rais aliyeko madarakani halafu baadaye eti aje asimame jukwaani kum-challenge? Wapinzani makini huwa hawazungumziii mazuri ya serikali bali huangalia mabovu tu ya kupinga; iwapo serikali ikifanya mazuri basi wametekeleza wajibu wao hakuna haja ya kuwapinga lakini siyo kazi ya upinzani kupongeza serikali hata sikumoja
 
Haiwezi kuwa suluhisho wala mwanzo wa kuijenga cdm. Ila ni kinyume. Labda iondoke uongozi mzima wa chama. Coz wao ndio waliokinajisi. Wanajiita makamanda labda wa kuongoza nyumbu. Viongozi wa cdm ni sawa na viongozi wa yanga na simba. Maneno mengi akili ndogo na vichwa panzi. Wepesi kusahau waliyosema jana. Wapo kimaslahi zaidi.
WATU WEWEEEEEEEEE...vuta mkwanja tulia fanya yako
 
Hata Dar haikujengwa siku moja Hata sasa bado inajengwa
Dar ya sasa haijengwi upya..inafanyiwa repairing kule palipokaa vbaya panarudshiwa kwa ubora zaid..ubaya n kwamba lichama la ndugu yetu MANGI linahitaji kujengwa upya..yani fresh kuanzia MSINGI...maana mkandarasi wa hyo nyumba alikula hela walahi..nyumba saivi imejaa nyufa kila mahali:D:D:D
 
Pale rais wetu Mh.Joseph Pombe Magufuli walipokutana na Mh. Lowasa ikulu aliposema kuwa Lowasa ni mwanasiasa mzuri,hapohapo ndege wale tausi wa ikulu walillia mara mbili.Tukiwa sisi ni waafrika na mila zetu hii inaashiria nini ?
 
Back
Top Bottom