Ikulu lawamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu lawamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Aug 19, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  • Yafuja mamilioni kwa chakula cha jioni
  * Watafiti bado waitilia shaka kwa rushwa


  Na Edward Kinabo - Tanzania Daima


  WAKATI baadhi ya wadadisi wa mambo wakihoji faida gani taifa lilipata kwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa uchumi wa dunia (WEF), imebainika kuwa Ofisi ya Rais - Ikulu ilifuja fedha za umma takriban sh milioni 367 kwa hafla ya chakula cha jioni kwa wajumbe wa mkutano huo.

  Mkutano wa uchumi wa dunia ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano ‘Mlimani City’ jijini Dar es Salaam, kuanzia Mei 5 hadi 7, mwaka huu.

  Taarifa za uchunguzi kutoka kwenye mfumo wa ufuatiliaji rushwa ulio chini ya shirika lisilo la kiserikali la ‘Agenda Participation’, zimethibitisha Ikulu kutumia vibaya fedha za umma katika hafla hiyo ya chakula cha jioni.

  Aidha, ukubwa wa bajeti ya chakula hicho cha jioni na mkataba mzima wa tukio hilo baina ya Ikulu na kampuni ya waandaaji, vyote kwa pamoja vimeashiria kuwapo kwa mazingira ya rushwa katika maandalizi ya tukio hilo, hasa kutokana na kujumuishwa kwa mahitaji mengi yasiyokuwa na ulazima, licha ya kuwa yaligharamiwa kwa gharama kubwa.

  Tanzania Daima linayo nakala ya mkataba wa maandalizi wa tukio hilo ulioingiwa na Ofisi ya Rais - Ikulu na Kampuni ya ‘Round Trip Event and Production Tanzania’, inayoonyesha vipengele kadhaa vya makubaliano vilivyotiliwa shaka kubwa na watafiti hao wa rushwa.

  Mkataba huo ulitiwa saini Machi 31, mwaka huu na Katibu Mkuu wa Ikulu akishuhudiwa na Ofisa mwingine wa ofisi hiyo anayefahamika kwa jina la Mussa M. Makuya, huku mtia saini wa kampuni hiyo akiwa Prashant Powar.

  Moja ya mambo yanayodaiwa kutoa mwanya kwa matumizi mabaya ya fedha za umma katika tukio hilo ni mkataba huo kuwa na mlolongo mrefu wa bidhaa mbalimbali bila kuonyesha bei mahususi za kila bidhaa na badala yake jumla kuu kuwekwa bila hata kuchanganuliwa jinsi ilivyofikiwa.

  Kwa mujibu wa mkataba huo, mialiko kwa waliohudhuria hafla hiyo iliigharimu serikali sh 8,250,000, mapambo na ukumbi sh 85,800,000, muziki na vipaza sauti sh 19,800,000.

  Matumizi mengine ni taa maalumu iliyogharimu sh 39,600,000, mfumo maalumu wa video sh 13,200,000, graffiti maalumu sh 6,600,000, burudani ya kawaida sh 13,200,000, burudani za jukwaani sh 15,180,000 na sh 3,300,000 zilizotumika kwa mawasiliano.

  Pia sh 26,400,000 zilitumika kulipa watendaji kazi wote waliohusika na menejimenti ya tukio hilo, sh 33,000,000 gharama ya usimamizi wa tukio na sh 27,060,000 zilitumika kwa vitu vya ziada na dharura.

  Hata hivyo, upembuzi wa kawaida wa orodha ya mahitaji hayo ulionyesha wazi kuwa baadhi ya bidhaa na huduma zilizotolewa hazikuwa na ulazima wowote.

  Kilichowashangaza zaidi wafuatiliaji wa masuala ya rushwa ni jenereta la kufua umeme kukodiwa kwa sh 19,800,000 wakati uongozi wa ukumbi wa Mlimani City ulikwisha kutoa umeme na jenereta la dharura.

  “Kwa mfano, jukwaa la kuchezea lililonyanyuliwa na tingatinga, maonyesho kwenye makabati ya maonyesho na mfumo wa mawasiliano, viliwekwa kwenye bajeti wakati hakukuwa na ulazima huo, kwani ukumbi ulikuwa umewekwa vizuri na hakukuhitajika nyongeza hizo, hususan kwa lengo la kurahisisha uchezaji wa muziki,” ilifafanua sehemu ya taarifa hiyo.

  Kibaya zaidi, baadhi ya bidhaa na huduma zilizokuwa zimeorodheshwa ziliwekewa mabano kuashiria kwamba zingetumika tu kama zingehitajika, hali iliyotia shaka kujua zilizolipiwa na zile ambazo hazikulipiwa, wakati mkataba ulisainiwa ukionyesha idadi kuu ya pesa ya bidhaa zote zilizoorodheshwa.

  “Swali la kujibiwa ni je, kwa huduma zile ambazo hazikutumika au kuhitajika, nini kilifanyika ?” ilihoji sehemu ya utafiti huo.

  Gazeti hili lilipowasiliana na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kupata majibu yake juu ya mkataba huo na matumizi hayo makubwa ya fedha za walipa kodi, alikataa kulizungumzia suala hilo kwa sababu ya kile alichokieleza kuwa yupo likizo.

  “Sasa bwana hilo suala mimi siwezi kukujibu…nipo likizo, umesikia…nipo likizo,” alisema Luhanjo na kukata simu.

  Serikali imekuwa lawamani mara kwa mara kwa matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma, yakiwamo yale yahusuyo safari na mikutano ambayo baadaye mafanikio yake kwa taifa huwa vigumu kuonekana au kuelezeka.

  Huko nyuma serikali iliwahi kushutumiwa kwa kutumia mamilioni ya shilingi kugharamia mkutano wa Sullivan mwaka 2008.

  Mkutano huo uliofanyika Arusha uliwakutanisha zaidi ya wajumbe 500, ambapo wengi wao walitoka Marekani ya Kaskazini.
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Unbelievable!
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Ndo kawaida, unadhani kwa utawala huu nini kitaendelelea, hakuna kuwajibishana.

  Wanakula tu, mifupa wanawaachia wapambe uchwara waliovamia jamvi...
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nimeisoma habari hii katika Tanzania Daima. Ingekuwa ni Rwanda ama Ghana, kitu cha namna hii heads zinge-roll. kama Ikulu kwenyewe maafisa wanafanya uchafu wa aina hii na Mkulu akaa kimya, jee huko ngazi za chini? I am quite certai half of the money ended into officials' pockets!

  Kinachoudhi zaidi ni kwamba Mkulu anasema hawezi kuwalipa wafanyakazi Shwanachodai kwani hana hela hizo. Lakini anazo za kuliwa na maafisa wake. Sijui wanamgawia?

  Jamani, hivi hatuweziu kujitutumua na kumuweka mpiganaji wet Ikulku kuondoa uozo huu ambao haipiti siku bila kusikia?
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,129
  Trophy Points: 280
  chakula cha jioni kumbe ni ule mkutano wa mlimani city!!!!
  ikulu pia huwa inafuja kwa ajili ya chakula cha jioni cha futari ktk kipindi km hiki cha mfungo wa sisi waislamu.......mko wapi waandishi?
   
 6. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmmh nakumbuka siku moja nilikuwanapita barabara ya Mazense nikamwona mtoto kama wa miaka 8 amesimama pembeni ya muuza miwa anokota maganda maganda wa miwa anakula kwa bidii ..jua lilikuwa kali...amezungukwa na nzi...nakumbuka pia kule kijijini ulanga nilipita nikiwa na shughuli za kikazi katika health centre fulani mara akatokea dada mmoja ametoka kujifungua ana miaka 14 tu na mume wake ana kama 17yrs wamekuja kuripoti kwenye health centre baada ya kujifungulia wanakojua wao...dada hana hata nguo za kumsetiri...amelowa damu anatembea kwa aibu...sikuelewa kwa urahisi kama wana ndugu ama hawana...haraka nikachukua nguo yangu na kumfunika...nesi aliyekuwepo ndani akawaita kwa ukali ......na maneno ya kejeli ....

  ninaposoma ubadhirifu huu...inaumiza sana ......

  mix with yours
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Serikalini that is how things go, kwa mwezi unaweza kukuta kuna upuuzi kama huo X 100
   
 8. M

  Mutu JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  rais anawajibika hapa asipo wawajibisha watu wake ,au ndio wana balance hela za uchaguzi!!
  ok wekeni maswali ya uchaguzi hayo.
   
 9. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mkataba ulisainiwa na Musa M. Makuya huyu ni ndugu wa mke wa mkuru sasa unafikiri kuna hatua yoyote itachukuliwa hapa, ikulu sio mahari pa kupeleka waswahili swahili panahitaji watu serios wenye uwezo wa kufanya maamuzi
   
 10. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unbelievable ni soo
  mix with yours
   
 11. D

  Dina JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ndio maana tunaamini viongozi wetu sio kwamba wanashindwa kutuletea mabadiliko, nia ndio ambayo hawana, coz mafungu yapo!
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye nyekundu pameniumiza sana! Hawa ni watoto - wanahitaji kusaidiwa.
   
 13. thetowerofbabel

  thetowerofbabel Senior Member

  #13
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 17, 2010
  Messages: 112
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  asa watanzinia si bado tuna penda ujinga wacha wale tuu
   
 14. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Mke yupi fafanua?
   
 15. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WOS nilitamani kulia hasa nesi yule alivyotuambia bila haya kuwa 'kaja hapa na uchungu tukamwambia kuwa hatuwezi kumzalisha mtoto wa miaka kumi na minne hapa ....tukamwambia aende hops ya wilaya...nadhani ndio ametokea huko amezaa salama anakujakuripoti ili kurejista mtot' WOS alikuwa ameshika mtoto ambaye yupo healthy wa kiume...anatembea kwa taabu ..kilichinuma ni nguo alizovaaa zimelowa da....! na hana nyingine mkononi....niliteseka siku nzima siku ile sitasahau ilikuwa 2007 november! so ukisikia taarifa za ufujaji wa namna hii na ukilinganisha hali ya watz vijijini mmmmmh acha tu
  mix with yours
   
 16. M

  Mutu JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ahaaaaaaaaaaa itakuwa mkubwa tehe tehe tehe
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi sijashangaaa....Rais mwenyewe anapenda kuwe na party kila siku huko ikulu kwake haya ni matumizi ya kawaida...WEF was nonense and Tanzania ilijitutumua tu ku host but hakuna la maana walilopata zaidi ya kutuletea foleni tu hapa mjini
   
Loading...