Iko Wapi CCM Yetu? John Malechela Tujibu, au Alli H. Mwinyi tujibuni

Iko Wapi CCM Yetu? John Malechela Tujibu, au Alli H. Mwinyi tujibuni

eedoh05

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Posts
632
Reaction score
237
Iko wapi CCM yetu?
Iko wapi ile CCM tuliyosoma katiba yake sekondari?
Iko wapi CCM yetu?
Ali H.Mwinyi tuambie iko wapi CCM yetu?
CCM ile iliyotufanya tujisikie fahari zama zile,
Tulipokuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama ngazi ya Shina tulipokuwa JKT
Tukilitumikia Taifa kwa mujibu wa sheria.Iko wapi?
Jonh Cigwemisi Malechela mumeipeleka wapi CCM yetu?
CCM iliyotufanya tujisikie fahari kila majina ya viongozi wazalendo wapigania uhuru wa Afrika yalipotajwa!
Ndani ya CCM ile likitajwa jina Edward Mondolane, Steve Biko tuliona ndugu yetu katajwa;
Akitajwa Samora Machele tulijiona tumetajwa CCM wote.
Iko wapi CCM ile?
Kingunge Ngombale Mwilu jitokeze hadharani tuambie iko wapi CCM yetu?
CCM iliyotukuka, CCM iliyotuwezesha kutembea kifua mbele;
CCM iliyotutia hamu ya kutamka majina ya Kina Ben Bela, Patrick Lumumba, Sekeo Toure, Nnandi Azikiwe, Dedan Kimathi, Abeid Karume, Sam Nujoma,Quetire Masire, na wengine wangi.Iko wapi CCM ile?
Benjamin William Mkapa hebu jitokeze mbele za watanzania utuambie iko wapi
CCM aliyoiacha Mwl.Julius Kambarage Nyerere?
Pius Msekwa jitokeze ututoe kwenye sintofahamu hii utupe majawabu mwafaka; Iko wapi
CCM ya akina Paul Sozigwa, Daud Mwakawago,Horace Kolimba na wengineo,iko wapi?
CCM hii siyo ile tuliyokulia ndani yake toka vijijini mwetu. CCM yenyewe iko wapi?
Iko wapi CCM iliyovitia nidhamu vyombo vya dola, Polisi, Magereza, Usalama wa Taifa,Uhamiaji,
Mgambo na JWTZ Vikawa vyombo vya wananchi. Siyo ilivyo sasa, vyombo hivi vimekuwa kama mali ya mafisadi,Waroho na wenye uchu wa madaraka, wauaji, wasingiziaji, wabambikizaji wa kesi kwa wasio hatia.
CCM yetu ya wakati ule ilitufanya tufurahie kuona parade la vikosi hivi kila wakati wa sherehe za kitaifa.
Jaji Lusinde Warioba iko wapi CCM yetu aliyowaachia Mwalimu muilee? Iko wapi?
CCM ya sasa inatawala serikali ambayo polisi wake wanauza bangi! Hakuna akemeaye kabisa!
CCM ya leo inaunda serikali ambayo polisi wake wanauza risasi na bunduki kwa
Al-Shababu.
Silaha hizo hapana shaka zinawafikia Boko Haramu, pengine zinanunuliwa na Al-Quida…nani ajuaye? Na nani anajali?
CCM inamiliki serikali yenye jeshi la polisi lililoanza kugeuka Boko Haramu, likielekea kuwa Al-Shababu.
John Cigwemisi Malechela, Pius Msekwa, Benjamin Mkapa, jaji Warioba, Kingunge Ngombale Mwilu Hebu jitokezeni mbele za watu mtueleze iko wapi CCM yetu aliyoiasisi Mwl. Nyerere?

CCM ya Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye, Abdalahiman Kinana sio ile aliyotuachia Mwl. Nyerere. Iko wapi CCM yetu jamaniiiiiii? Hii ni CCM ya serikali ya piga tu,..piga tu. Hailindi haki za binadamu, inavunja katibaya nchi.

CCM ile ya zama zile ilijitahidi kutuletea Mawaziri Wakuu waliopima maneno yao kabla ya kuyatamka. Mashujaa wa kudhibiti hasira zao.

CCM hii ya leo ina serikali inayosimamiwa na Waziri Mkuu aliyeruhusu wananchi kuwauwa wauaji wa albino;
tena baadaye akakasema litakalo kuwa na liwe mtu akatekwa; juzi kati hapa kasema polisi piga tu..piga tuuu
Mtwara, Mbeya, Arusha, Iringa, Tarime, Singida, Kigoma, Igunga...Pigeni tu...pigeni tu!

Wajukuu zetu tutawaambia niniii? Tutawaambia tuliipeleka wapi CCM iliyotukuka Afrika, Uchina, Cuba, Urusi na kwingineko? Iko wapi CCM ambayo Mzee Nelson Mandela alikuja miaka ya 1990 kuwasalimia, kuwaona na kuwashukuru waasisi wake? Iko wapi CCM yetuuuu?

Hii ya leo nikama vile kundi lingine la Al-Shababu, maana polisi wa serikali yake wanauza risasi na bunduki kwa Al-Shababu.

Malechelaa, Kingunge,Mwinyi, Mkapa, njooni mbele mtupe majibu, tuondokane na sintofahamu hii iko wapi CCM Yetuuuu?.

 
Ilishakufa.Pole ndugu yangu.Na kati yao wote hao hakuna atakayeweza kukueleza iko wapi.
 
Wote hao uliowataja walikwishabadilika kuwa wezi na manyang'au baada ya kifo cha Nyerere. Hakuna mwenye mbavu za kukujibu!!!!
 
"CCM siyo baba yako" hata hivyo soon itabaki historia hata mabaki yaliyopo yataondoka kabisa. Kwa ufupi hakuna atakayekupa majibu
 
Mkuu umenena yote, bahati mbaya tukohoji ile ccm ya wakulima na wafanyakazi, ile ya watu wote, ile iliyoipa fahari nchi yetu kote duniani, tunaambiwa wapinzani, magaidi, tunapigwa na kuachiwa ulemavu kama sio kuachwa yatima
 
kikwete ndo anayo siku hizi hiyo ccm na mwigulu na nape ukiitaka watafute hao ndugu utaiona
 
Nakupenda ccm!

Nikweli ila unaijua CCM? CCM ni chama kinacho amini WATU na MAENDELEO yao .... je ndio hiki hiki au kilishabadilika wewe bado hauna habari....CCM ni chama kilichotokana na AZIMIO LA ARUSHA! waliohodhi madaraka ndani ya chama (CCM) wanaamini azimio la Arusha limepitwa na wakati .... nashngaa eti wamelizamisha Baharini Zanzibar wakaja na MALENGO YA MELINIA kama mbadala wa AZIMIO hivyo dira na mwelekeo wa chama sasa hautokani na mawazo ya wanaCCM bali UMOJA WA MATAIFA .... ndio maana kila mwanaCCM we kweli haelewi kwanini viongozi wa sasa wa CCM hawafikirii tena kama zamani ila ni sababu hii ya kusaidiwa ufikiri na UMOJA wa mataifa....!
 
CCM ya kiukweli ilienda na mwendazake Nyerere. Iliyopo sasa ni chama kilichovaa ngozi ya kondoo ikiitwa "CCM" kwa maana halisi ya vyote hivi: Chukua Chako Mapema; Chama cha magamba; Chama cha Mafisadi; Chama cha manyang'au, Chama cha Maangamizi n.k. n.k. Usipoteze muda wako kuwauliza hao maana hutapata jibu ulitakalo wewe. Lililobaki songa mbele na kutafuta chama mmbadala.
 
"I'm sad to say I'm on my way
Won't be back for many a day
My heart is down, my head is spinning around
I had to leave a little girl in Bagamoyo town" by Dhaifu
 
Back
Top Bottom