Ikitokea ukafumaniwa guest ukiwa na dada yako kama kisa hiki utafanyaje?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,543
22,050
Habari wapendwa;

Mfano Tukio kama hili likakutokea utafanyaje?

Kuna jamaa mmoja jina lake “Z” ambaye anaishi mtaa wa tatu kutoka mtaa ambao dada yake “X” kaolewa huko anayeishi na mmewe “Y” , huyu kaka mtu alikuwa na mke wake pia jina lake “K” nao walikuwa wanaishi kivyao kama mme na mke.

Huyu jamaa punde pindi mkewe alipojifungua, Hakuwa mwaminifu akawa anatoka nje ya ndoa, siku moja akaamua kwenda Guest moja hivi akiwa ametegemea atapata mrembo hukohuko wakuvinjari naye; alipofika Guest akaongea na mhudumu kwamba amwitie mwanamke yeyote wa fasta aje avinjari naye;

Yule mhudumu kutokana na sifa za mrembo alizotaka yule jamaa, ikabidi atafte katika orodha wa wadadapoa walioacha namba zao pale kwa ajili ya showfasta;

Mhudumu akawa kampigia dada mmoja hivi aje, pasipo kujuwa kumbe ndiye mdogo wake na Yule jamaa- yaani dada mtu, na bahati mbaya huyo dada mtu pindi alivyokuwa anapigiwa simu na Yule mhudumu wa pale Guest house kuhusu dili,Basi mme alisikia mlio wa simu na ilipopokelewa akawa anasikia haya mazungumzo akiwa dirishani kwa nje ikabidi asikilizie

Sauti “ Hello shoga nambie,. [respond]..huyo bwana anahela asiwe miyeyusho tu [respond].. si hiyo guest mpya hapo kona ya …… ? [respond] unasema ana tsh ngapi?.[respond] ..mhh shoga, mme wangu anachelewa sana kurudi wewe nipe dili tu…[respond]… sasa hapo na chako kimo humo humo au? [respond]…haya najiaanda nakuja sasa hivi, kwahiyo huyo bwege yupo chumba gani? [respond]..ooh chumba cha ngamia, ok, kwahiyo mlango wa nyuma upo wazi? [respond] poa naja asahivi shoga nilikuwa nimefuriaje?...[respond] poa dk 15 nafika.

Yule mme kusikia hivo daah, akajuwa tayali kumbe naibiwa, hakuingia ndani akaamua kutangulia kulekule gest mpya ili akafumanie, wakati anakwenda bahati nzuri akawa kakutana na mkewe “Z” anatoka kazini, akamwambia kuna mahali anaenda anaomba amsindikize ili akaone mke wake anavyo mtesa kwa usaliti. Wakaandamana mpaka gest mpya, yeye jamaa akazunguka nyuma akajipanza kuona kama kuna mtu anaingia mlango wa nyuma je ni mkewe? Na kule mbele aliweka walinzi wake kuwa wakimwona mkewe anazama wamsitue;

Kweli; baada ya dakika kadhaa mkewe akapita na kuingia gest, naye jamaa “Y” akaingia punde na kwenda hadi kile chumba, akawa kawaita na wenzake ili kufumania,

Wakati huko ndani kukikwa na mtu na dada yake wakiulizana umefata nini hapa, na dada mtu ana muuliza kaka yake umefata nini hapa; wakasikia mlango unagongwa kwa nje; ile kufungua , ni sura uso kwa uso na mmewe (shemeji mtu). Na mke wake kamkubwa “Z”

Swali; Je; Kama ungekuwa ni wewe umefumaniwa hivi ukiwa na dada yako guest ungejiteteaje hapo? karibu
 
WAKUU HUU MUDA MNAOPOTEZA HAPA MNGESOMA ZILE POST ZA JAMII INTELIGENCE BILA HATA KUPOST MNGEFIKA MBALI SANA
 
Back
Top Bottom